Naomba niwatahadhali kitu kimoja kuwa, siasa za maswa ni ngumu sana kwa sasa na hasa ukizingatia mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea nchini.CCM kule maswa haina chake na hii ni kutokana na uwepo wa Shibuda kama mbunge wa CDM.Ikumbukwe pia kuwa ni Shibuda aliyesababisha Mzee BUKOYE kada wa CCM kuhamia CDM na ndiye alikuwa mmoja wa nguzo za wazee wa CCM maswa.Ukisikia mzee Bukoye maana yake ni siasa za Maswa.Shibuda lazima tumpe credit kwa kubadilisha siasa za Maswa, na leo hii huwezi kufikiria kuwa itatokea mgombea wa CCM kwangazi yoyote atashinda maswa hiyo sahau hataka kama atagombea yeye Shibuda hatashinda hiyo ndiyo Maswa ya leo.Kwa hiyo wale wanaofikiria kuwa shibuda anajipendekeza kwa JK na CCM wanapoteza muda bora wajadili mengine.
Tabia halisi za wasukuma:
Wasukuma wana tabia ya ukarimu na ubinadamu kwa kiwango kikubwa (isipokuwa fisadi che*****), kwa hali hiyo ndiyo maana ni kabila pekee lenye watani wengi hapa tz.Kule usukumani kuna ngoma za kienyeji za WAGALU na WAGIKA zinafanyika sana wakati wa mavuno, inapofika wakati wa ngoma mawasiliano kati ya haya makundi huwa yanakoma kwa muda hadi ngoma ziishe mara ngoma zikisha na mshindi kupatikana mahusiano huwa yanalejea kama kawaida na hata kukopesha na kuazimana vitu kunafanyika.
Nimalizie kwa kusema kwamba anachofanya Shibuda ni asili yake ndivyo wasukuma walivyo hawana adui, ila wakati wa majukumu ya kimaslahi hawana aibu ya kumuharibu au kumuua adui.Maswa kwa sasa ni ya CDM na shibuda anajua hilo msipoteze muda yeye na kikwete ni watani.