Shetani ni dude zito ambalo wanadamu hatuliwezi

Clever505

JF-Expert Member
Jul 27, 2020
1,077
1,971
Miaka michache iliyopita wakati nipo sekondari tulipoanza kuchagua masomo kulingana na kazi tunazozipenda nilishangaa kuona kazi ya ualimu ilikuwa inahitaji upate angalau D kwa kila somo. Kupata D ni kukaribia kufeli kabisa, nikawaza; hawa ambao wapo mwishoni kabisa ambao kidogo tu wapate F wataweza kweli kufundisha wanafunzi wapate A? Na kuna wimbo wa msomi mmoja anaitwa Bonta unaitwa 'tokomeza zero' nae amejiuliza swali kama hilo langu.

Juzi kati hapa kuna msichana mmoja aliniomba nimfundishe lugha (English) nilipoanza kumfundisha nikajikuta kuna mambo marahisi tu ila nilikuwa nimeyasahau, kwa msaada wa Google nikayakumbuka ila baada ya hapo sidhani kama nitayasahau tena. Kupitia tukio hili, nimekuja kupata jibu mwenyewe la kwa nini wanaopata D wanafaa kabisa kuwa walimu na wanao uwezo mzuri kabisa wa kumfanya mwanafunzi akapata A.

Jibu ni kwamba, kwanza kupata D inaonyesha we sio mbumbumbu kabisa na kuna uwezekano ukirudia mtihani unaweza kutusua vizuri tu. Sasa, unapopewa nafasi ya kuwa mwalimu ni kwamba unavyoendelea kufundisha mara kwa mara ndivyo ambavyo na wewe unaendelea kuyajua na kuyahifadhi zaidi hayo unayoyafundisha. Baada ya miaka michache mbele uwezo wako unakuwa mkubwa sana hata kuliko waliokupita kwenye mtihani wako wa form 4 ambao hawakuendelea kujifunza zaidi.

Narudi kwenye point yangu sasa, shetani ni kiumbe mzito sana wanadamu hatumuwezi. Huyu kiumbe yupo tangu wanadamu hawapo ni wazi kwamba lazima ana uwezo mkubwa na mbinu nyingi za kumfanya mwanadamu amuasi Mungu. Chukulia mfano mtu Kama kaini mtoto wa Adam angekuwa hai hadi leo na aamue kutudanganya na kusema hivi vitabu tulivyonayo sasa vinavyomzungumzia Mungu ni vya uongo na akakileta chake akaelezea maisha ya wanadamu yalivyokuwa tangu mwanzo hadi leo ni nani angeweza kumpinga?

Mfano mwingine, mtu kama mama Maria mke wa Nyerere ambae ameishi nae muda wote, leo hii akiamua kuleta habari yoyote kuhusu Nyerere ambayo haijawahi kuandikwa popote ni nani atapinga?

Sasa, uwepo wa shetani kwa miaka yote hii ni wazi kwamba hashindwi hata kidogo kutufanya sisi wanadamu kuasi sheria za Mungu, shetani huyu huyu ambaye tayari alikuwa ameshafukuzwa kwa Mungu ila bado tunaona kwenye biblia anaongea na Mungu Ayubu1:7 mazungumzo mazuri tu kama hawana bifu vile, sasa we mwanadamu utamshinda kweli kiumbe huyu? Anaijua dunia kindakindaki, historia ya vizazi vyote anaijua we ni Nani hasa akushindwe? Ni lazima kabisa akunase kwenye mitego yake.

Shetani alipata nafasi nzuri kabisa ya kuongea na Yesu Mathayo4:5-10 waliongea vizuri tu bila tatizo. Kulingana na masimulizi tunayoyapata, wanadamu wote wamewahi kutenda dhambi isipokuwa Yesu peke yake, kwa hiyo ni kwamba shetani ameshawahi kuwatumbukiza dhambini wanadamu wote na kumshindwa mmoja tu ambaye ni Yesu pekee. Nasema shetani hakumuingiza Yesu kwenye dhambi kulingana na masimulizi yaliyopo,, sasa sijui kama Yesu aliwahi kufanya dhambi kwa sababu hamna sehemu yoyote kwenye biblia panapoonyesha alifanya kosa lolote.

Shetani huyu ambaye aliweza kumfanya Adam amuasi Mungu we utamkwepa? Shetani ambaye aliweza kuwafanya watu wa karibu na Yesu wakamsaliti we ni Nani hasa asikunase? Huwa nashangaa sana kuona kuna vijitu vidogo ambavyo hata umri wao hauzidi nusu karne eti vinakaa kikao vinamkemea na kumdiss shetani vikifikiri vimemuweza. Shetani ye yupo zake huko anawachora tu. Eti anakuja mpumbavu mmoja hapa ambaye amejitajirisha kwa kuiba pesa ya kanisa na kusema ameonana na Yesu akampa ufunguo akafungue watu, anatudanganya tu..

Shetani aliweza kuvuruga mipango ya Mungu kwa Adam na Hawa, hapo huoni kwamba jamaa ana nguvu kubwa? Mungu anatuma watu duniani waje kumtangaza yeye na anawaahidi mambo mazuri mengi wale watakaotii amri zake ila shetani hajawahi kuumba mtu na kumtuma aje amtetee na bado nasikia motoni kutakuwa na watu wengi kuliko peponi. Sasa hapo tafakari, shetani ambaye inasimuliwa kwamba wanaomfata wataingia kwenye moto kwa nini ana wafuasi wengi kuliko Mungu ambaye ameahidi mambo mazuri?

Shetani hana kitabu kinachomsifia ila mwisho wa siku atavuna watu wengi licha ya kuwa wanadamu wanampenda Mungu ila bado wanaunga mkono matendo ya shetani. Shetani aliweza kuwashawishi ⅓ ya malaika na wakamuelewa na wakamuasi Mungu, we ni nani asikuweze? Huyu jamaa anadeal na watu wote mpaka vitoto vidogo. Alimshawishi gwaji amle mwanamke ambaye si mkewe kisha akamwambia hiyo haitoshi jirekodi kabisa, halafu shetani huyo huyo akaja kumwambia kataa sema video sio yako ile kandamizia kusema ule mkono ni wa baunsa. Hapo bado hujaamini tu kwamba huyu jamaa ni mzito na hatumuwezi?

Jamaa akichorwa anawekwa na mapembe ili awe wa kutisha ila bado hata wewe mwanaJF ni mfuasi wake japo unajua kumfata ni kujipeleka motoni ila bado upo nae. Anasingiziwa mambo mengi na hatumuoni akijitetea lakini wafuasi wake wanaongezeka tu. Kuna jamaa kule Arusha ni mwalimu wa madrasa ila alivinyandua vivulana vidogo zaidi ya ishirini akijua wazi kufanya vile ni kumuunga mkono shetani kwenye kazi zake lakini hakujali hilo yeye akatekeleza amri ya shetani.

Shetani amebadili mipango mingi ya Mungu, Mungu aliumba malaika wampende ila shetani akashawishi wengine wasimpende, aliumba bustani ya Eden ikaliwe na Adam na Hawa shetani akaharibu mpango, aliumba wanaume waoe wanawake ila shetani amebadili baadhi wanaoana madume kwa madume, bado huamini kwamba shetani ni mzito?

Namalizia kwa kusema, shetani hatumuwezi. Kwa maoni yangu naamini siku ya mwisho Mungu atatusamehe wote na kutuingiza peponi kwa sababu anajua wazi kwamba huyu kiumbe alishindikana tangu mwanzo na sisi kama wanadamu hatuna nguvu ya kumshinda.
 
Siku nilipoamini shetani ni noma ni pale Yesu alipomuongelea huku akilia machozi.
 
No way kaka tuzidi kupambana tuu... Maandiko yanasema duniani kuna dhiki nyingi lakini sijui nn mbelee huko ila tutashinda
Shetani utamshinda kweli? Shetani alileta vurugu kwa Mungu, atashindwa kukuvuruga wewe? 😂😂 Kama ambavyo vitoto vidogo vinaenda peponi free Mungu atuangalie na sisi tuende free tu😭
 
Shetani utamshinda kweli? Shetani alileta vurugu kwa Mungu, atashindwa kukuvuruga wewe? 😂😂 Kama ambavyo vitoto vidogo vinaenda peponi free Mungu atuangalie na sisi tuende free tu😭
Nothing to worry bro Mungu kashatupa assurance we kwann usiamini
 
Shetani si sifa na siyo kiumbe hata binadam unaweza ukawa shetani
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom