Mjaribu shetani hamwogopi mwombaji mzuri

Mjaribu shetani hamwogopi mwombaji mzuri

Samson Ernest

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2014
Posts
1,206
Reaction score
1,695
Mt 4:3 SUV
[3] Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate.

Yesu akiwa kwenye maombi ya siku 40 ya kufunga, alikutana na mjaribu shetani. Tukio ambalo linatupa mshangao na kushtuka kidogo, maana tulitegemea mtu akiwa kwenye maombi mazito namna hiyo asingeweza kusogelewa na Shetani.

Nataka ujifunze jambo hapa, hasa ukiwa mwombaji mzuri, baadhi hufikiri shetani hawezi kutusogelea na kutujaribu wakati tupo kwenye maombi makali.

Ukiwa mwombaji Sana, utakutana na mjaribu, tena wakati ambao upo karibu sana Mungu wako.

Kukutana na mjaribu shetani haimaanishi kuna mahali umekosea mbele za Mungu.

Mjaribu anakuja kwako ili umkosee Mungu wako, na si kana kwamba umekosea ndio maana amekusogelea.

Tunapata funzo kubwa sana hapa kuwa tunapaswa kujaa neno la Mungu, ndipo tutaweza kukabiliana na mjaribu.

Mt 4:4 SUV
[4] Naye akajibu akasema, Imeandikwa, Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.

Mtu asiye na neno la Mungu la kutosha, anaweza akaingia kwenye mtego wa mjaribu, na akiwa kwenye maombi yake.

Nasema hivyo kwa sababu sio ajabu ukamkuta mwombaji amenasa kwenye mtego wa dhambi.

Narudia shetani haogopi waombaji kama unavyofikiri, anaogopa mwombaji mwenye neno, ambaye hawezi kumdanganya na kumwingiza kwenye mitego yake miovu.

Mjue Mungu unayemwomba na kumwamini kupitia neno lake, ili ajapo mjaribu asiweze kukutoa kwenye mstari wa ki-Mungu.

Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana
 
Kwakizazi hiki hiki !! shetani huyu huyu anayejua ya mbele yako na nyuma yako..Hapo labda Mungu mwenyewe akuchague upambane naye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom