Shetani nakuchukia Kwa Moyo wangu wote

Shetani nakuchukia Kwa Moyo wangu wote

Kuna dada mmoja hapa mbeya from sai,ni 25 yrs old alijikuta kwenye mkasa kama wako,akipanda kwenye daladala au anatembeatembea barabarani au sokoni watu walikuwa wanamsalimia ...shikamoo bibi....kuna siku moja iliyomfanya akimbilie kwenye maombi ni pale kaingia kwenye daladala iliyojaa,Mara akasikia konda akiwaambia abiria "mwoneeni huruma huyu bibi akae jamani!"😳😂😂😂😂
🤣🤣🤣Daah!Nimecheka kama mazuri vile!
 
Wakuu naandika huu Uzi Kwa majonzi Sana na masikitiko ya hali ya juu.

Wale mliosema kwamba ulimwengu wa roho haupo mko wapi???

Ngoja nianze kuelezea kisa changu,wakuu BIla shaka inatakiwa tukubali kwamba vita vyetu sio vya kimwili Bali ni vya kiroho na hapa ndipo shetani anapoamua kukutesa anatesa kweli kweli.

Leo hii Mimi nimekuwa kijana ambaye sionekani katika jamii.Najua mnajiuliza kivipi? Ni hivi, nimegundua ya kuwa Kila ninapoenda mgahawani na kukaa kwenye viti na kusubiria kupata huduma kutoka Kwa watoa huduma basi sipatii chochote.Kwa mara ya kwanza nilidhani kama utani lakini nimejaribu kufanya hivi na migahawa mbali mbali lakini naona hali ndyo IPO hivyo hivyo.Mgahawa wowote ninaoingia watu wananikuta na wakifika tu watoa huduma wanawachangamkia na kuwauliza wanachotaka BIla hata ya wao kuwaita Ili Mimi nipo pale pale naangaliwa kama kinyago.Yawezekana nimerogwa.

Nilijaribu kwenda na bar Moja wapo nikakaa kwenye kiti kusubiria huduma lakini hali ni Ile Ile.Mtoa huduma aliponiona badala ya kunihudumia alicheka.Nashindwa kuelewa Nina mkosi gani.

Ewe shetani kwanini unanitesa hivi nimefanya nini kukukosea.Wewe ni Mbaya kweli umekuja kuua kuiba na Kuharibu.
Nyie si mnasemaga hakuna mungu, shetani, majini, malaika sasa hapa unamzungumzia shetani yupi?
 
Back
Top Bottom