Shetani hajawahi kuwepo, Acheni uoga na masingizio!

Shetani hajawahi kuwepo, Acheni uoga na masingizio!

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Posts
7,450
Reaction score
10,804
...Asubuhi moja nilipelekwa kwenye pori nene, kigiza kilikuwa kinaanza na mvua kidogo kidogo ilikuwa inamwagika! Ile misauti ilitisha ila ndani mwangu nilikuwa vizuri na sikuteteleka! Wale jamaa walioniongoza walitisha kwa muonekano ila niliona kama ni maigizo tu! Yes, nilitaka nihakikishe ni nini wenzangu wanaamini kuhusu shetani na niliambiwa nitamuona live!!!

Ha ha haaaa, nilichokiona nilikuja kujua kuwa "shetani ni dhana tu, nothing serious"

Ndugu zangu, imani ni namna unavyoilazimisha nafsi yako kuogopa "a hidden future, fear of unknown" wote hatujui kuwa tukifa kama kuna maisha baada ya kifo. Dini kwa miaka mingi imetuhadaa eti kuna maisha Spiritual baada ya kifo, SI KWELI. Nani amewahi kufika huko? Anatupa evidence gani kuwa kuna moto wa kuchoma watu wa shetani na paradiso tamu kwa watu wa Mungu?
Kwa nini Mungu aumbe watu ambao anajua atawaumiza kwa mateso makali wakifa? Alishindws kweli kuwafanya wote waingie mbinguni?

Huyo Mungu alishikndwa kumtiisha shetani akabaki kuwa malaika mtakatifu na asitese watu walioumbwa na Mungu?

Kibaya zaidi wanadamu "wana akina Mungu tofauti ila shetani ni wa aina moja japo ana majina kibao"

Acha hofu, kutenda uovu ni hulka, hakuna shetani ati anawafanya watu watende uovu.

Shetani never existed! Tenda Mema, wasaidie wahitaji, wapende watu wote, ukifika muda wa kufa u gonna just decay like pundamilia na ndio mwisho wako!!
 
Sasa unasaidia hao wahitaji nani kakutuma, ilhali kila mtu kaja hapa duniani kimpango wake!!!

Tofauti yako na ambaye hatasaidia ni nini???, maana hamna wa kusahihisha.
 
Sasa kama nikifa ndio mwisho huo wema nafanya kwa manufaa gani? Kuna haja gani ya wema?

Uwepo wa viumbe na dunia/ulimwengu kuna nadharia kubwa mbili ya kisayansi na ya uumbaji (hapa ndipo kuna Mungu na Shetani)

Kwa usomaji na mafundisho niliyopitia nadharia zote mbili hazijitoshelezi hasa ya kisayansi ndio kabisa eti mwanadamu alikuwa nyani why manyani hawawi watu siku hizi?

Mwisho ni bora ukayaacha mambo yalivyo tu ukashughulika na mambo yanayokupa maisha tu ukatii sheria za nchi na dunia maisha yaendelee.
 
Sasa unasaidia hao wahitaji nani kakutuma, ilhali kila mtu kaja hapa duniani kimpango wake!!!

Tofauti yako na ambaye hatasaidia ni nini???, maana hamna wa kusahihisha.
Tenda wema nenda zako!
 
Sasa kama nikifa ndio mwisho huo wema nafanya kwa manufaa gani? Kuna haja gani ya wema?

Uwepo wa viumbe na dunia/ulimwengu kuna nadharia kubwa mbili ya kisayansi na ya uumbaji (hapa ndipo kuna Mungu na Shetani)

Kwa usomaji na mafundisho niliyopitia nadharia zote mbili hazijitoshelezi hasa ya kisayansi ndio kabisa eti mwanadamu alikuwa nyani why manyani hawawi watu siku hizi?

Mwisho ni bora ukayaacha mambo yalivyo tu ukashughulika na mambo yanayokupa maisha tu ukatii sheria za nchi na dunia maisha yaendelee.
Dini ndo inapotosha uhalisia kuliko Sayansi. Sayansi imefanya makubwa unquestionable kuliko hizi dini.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom