Mipango yoyote ile inayopangwa na mawakala wa shetani dhidi ya ustawi wa Demokrasia nchini Tanzania haitafanikiwa , Mungu siyo fala na anaona kwa macho yake kinachofanyika nchini Tanzania .
Baada ya utafiti wa Twaweza kuonyesha poromoko kubwa sana la Dr Magufuli , kutoka kukubalika kwa 96% hadi kiwango cha aibu cha 55% juhudi zilizosimamishwa za ununuzi wa binadamu baada ya karipio kali la Maaskofu zimerejeshwa tena kwa kasi ili kujaribu kuziba ombwe la kukataliwa na wananchi.
Labda niwakumbushe wadau wa demokrasia nchini , haya mambo hayakuanza leo na hakuna mahali uchafu huu ulifanikiwa , Chama cha KANU nchini Kenya kabla hakijakufa na kuoza kilinunua kila kiliyemtaka kutoka upinzani , akiwemo msaliti Raila Odinga ambaye alipewa cheo cha Katibu Mkuu wa KANU , Leo KANU iko wapi ? Demokrasia ni mpango wa Mungu mwenyewe aliouweka ili kupokezana madaraka ya nchi , hakuna mtu yeyote atakayeondoa hii na akafanikiwa.
Njama yoyote ya kishetani dhidi ya Mipango halali ya Mungu haitafanikiwa .