Sheria zinasemaje kuhusu miziki ya bar kwenye makazi ya raia?

M_kara

JF-Expert Member
Jan 9, 2016
385
293
Mimi ni mkazi wa kitongoji cha Moshono, Arusha. Ninakaa about 2km kutoka kwenye Bar inayo itwa Siara Pub. Kwenye bar hii muziki unapigwa hadi 10 usiku kila siku (sasa hivi ni 3:49am) na unasikika miles away. Hapa ni nyumbani kwangu lakini sina amani usiku mzima kwa sababu kuna mtu is getting a dime kwenye biashara isiyo nihusu. Kuna viongozi wa mitaa na madiwani ambao pengine hawapati usingizi kama mimi. What's wrong na sheria za serikali za mitaa? Watoto wa shule jirani ya bar hawawezi kujisomea usiku kwa utulivu wanaotaka? Jamani, can someone tell me nini cha kufanya? Na wewe mmiliki wa Siara Pub na wengine wa aina hiyo, mnadhani mnatenda haki kwa raia kama mimi eti kwa sababu mnatafuta rizki!!
 
Bado kuna wagonjwa wanahitaji utulivu, muarobaini wa hii kitu ni kurudi kwenye sheria za mipango miji
 
M-kara unaishi 2km kutoka Siara pub ama mita 200? Sikatai kwamba kuna bar za aina hii nyingi mtaani na zinasumbua raia ila kinachonishangaza hapa ni distance iliyopo kati ya eneo A na eneo B, kama ni hivyo wapo wengi wanaopata usumbufu na kelele za hio bar, cha muhimu hapa ni nyie wakazi wa maeneo jirani kufikisha malalamiko yenu kwa uongozi wa serikali za mitaa.
 
hiyo ni noise pollution

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), limeanza kung’ata kwa kutumia kanuni ili kudhibiti uchafuzi wa mazingira kwa kelele na mitetemo. Kwa sasa mtu akitaka kufanya sherehe mtaani, kupiga muziki kwa kelele, kuendesha ngoma za kukesha za nusu uchi (vigodoro) au ‘bai koko’ au kufanya ibada kwa kelele mitaani, atapaswa kulipa Sh milioni 10.

Pia, baa na kumbi za starehe za usiku zitakazopiga kelele, zitapaswa kulipa kiasi hicho.
 
Mimi ni mkazi wa kitongoji cha Moshono, Arusha. Ninakaa about 2km kutoka kwenye Bar inayo itwa Siara Pub. Kwenye bar hii muziki unapigwa hadi 10 usiku kila siku (sasa hivi ni 3:49am) na unasikika miles away. Hapa ni nyumbani kwangu lakini sina amani usiku mzima kwa sababu kuna mtu is getting a dime kwenye biashara isiyo nihusu. Kuna viongozi wa mitaa na madiwani ambao pengine hawapati usingizi kama mimi. What's wrong na sheria za serikali za mitaa? Watoto wa shule jirani ya bar hawawezi kujisomea usiku kwa utulivu wanaotaka? Jamani, can someone tell me nini cha kufanya? Na wewe mmiliki wa Siara Pub na wengine wa aina hiyo, mnadhani mnatenda haki kwa raia kama mimi eti kwa sababu mnatafuta rizki!!
Kawaloge,maana hiyo Pub ni ya katibu CcM mkoa!Loga ianguke kwa upepo
 
2km? Huo mziki sio mchezo
Hata mie nashangaa, hao walioko M100 sijui wanapumzika vipi. Cha msingi ni kumshauri Diwani na Baraza la Madiwani kutunga sheria ya kuheshimu "Quite Hours" kama haipo. Kama ipo, ni kuhanikiza utekelezaji wake kwa vitendo.
 
Back
Top Bottom