Sheria zetu ziwe kwa lugha ya Kiswahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria zetu ziwe kwa lugha ya Kiswahili

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by MziziMkavu, May 16, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  May 16, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Maoni ya katuni  Taifa hili limekuwa likijitumbukiza katika mkanganyiko usiolazima kila wakati hata katika vitu ambavyo kimsingi viko wazi, hali ambayo ama imeathiri ufanisi au uelewa wa watu wetu katika nyanja nyingi.
  Katika siku za hivi karibuni mjadala wa matumizi ya lugha ya Kiswahili umepamba moto miongoni mwa wadau mbalimbali, hasa baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo kutoa kauli ya serikali bungeni juu ya ulazima wa watumishi wa serikali kuitumia lugha hiyo katika kutekeleza majukumu yao.
  Mjadala wa matumizi ya lugha ya Kiswahili pia umekuwapo katika kushawishi itumike kama lugha ya kufundishia katika utoaji wa elimu kuanzia ngazi ya shule za sekondari na elimu ya juu; mjadala huu hata hivyo haujazaa matunda tarajiwa kwa kuwa kuna hoja zinajengwa na wale wanaunga mkono matumizi hayo na wale wanaopinga. Mjadala bado unaendelea.
  Hata hivyo, pamoja na kuwapo kwa mijadala ambayo haijakamilika juu ya matumizi ya Kiswahili kama lugha ya kufundishia, kuna utaratibu wa serikali kutumia Kiingereza badala ya Kiswahili katika kutunga sheria. Sheria zote zinazotungwa na Bunge zinakuwa katika lugha ya Kiingereza ingawa wakati wabunge wanajadili muswada wa sheria husika hutumia Kiswahili.
  Sheria hizi zikishapitishwa huendelea kubakia kwenye lugha hiyo hiyo, hivyo kuwa vigumu kwa wananchi waliowengi kutambua maana yake kwa kuwa si siri Kiingereza ni lugha ya wachache nchini.
  Hali hii ndiyo inakabili sheria nyingi za nchi hii ikiwamo ambayo kwa sasa serikali inakimbizana nayo ya Gharama za Uchaguzi. Sheria hii imeanisha nini kinaruhusiwa na kukatazwa katika kugharimia uchaguzi mkuu, baada ya kusainiwa na Rais mbele ya kadamnasi. Ofisi ya Waziri Mkuu imekuwa katika harakati za kuandaa kanuni za matumizi ya sheria husika.
  Hakuna ubishi kwamba sheria hii ndiyo itatumika kwa ajili ya uchaguzi mkuu mwaka huu, lakini bado iko kwenye lugha ya Kiingereza hali ambayo inakuwa vigumu mno kwa wagombea wengi kuisoma na kuielewa vema ili wasijekutumbukia kwenye vitendo ambavyo kisheria haviruhusiwi katika uchaguzi huo.
  Tunatambua kwamba uchaguzi ni mchakato, huhitaji muda na rasilimali nyingine kama fedha, watu, vyombo vya aina mbalimbali vikitambuliwa kama vitendea kazi; hivi vyaweza kuwa vyombo vya usafiri na vitu vingine vyote vinavyorahisisha mawasiliano baina ya mgombea na wapigakura.
  Mchakato huanzia mbali, kwanza mtu kujitambua kwamba anasukumwa ndani ya nafsi yake kuomba kuchaguliwa kuongoza kupitia chama cha siasa, kutafuta kuungwa mkono na wanachama wa chama chake na mwisho kujinadi kwa wapigakura; mambo haya yote katika sheria ya Gharama za Uchaguzi yameanishwa na yatafafanuliwa kwenye kanuni zinazosubiriwa kutolewa.
  Wakati wagombea wamekwisha kuanza kujipitisha huko na huko kutafuta kuungwa mkono kwa nia zao za kutaka uongozi, wengine hata hawajui sheria hii inasema nini kwa maana ya kuisoma wenyewe na kuielewa bila kutafuta mkalimani kwa kuwa iko katika lugha ambayo ni ngeni kwa wengi. Kwetu tunaona ni udhaifu mkubwa kwa sheria zetu kuwa kwenye lugha ambayo si inayozungumzwa na wananchi waliowengi.
  Ndiyo maana tunasema matatizo mengi ambayo yatakuja kugundulika baadaye uchaguzi ukishafanyika, kama vile watu kupinga matokeo ya uchaguzi labda kwa sababu za matumizi ya vitu ambavyo vimeharamishwa kwenye sheria ya Gharama za Uchaguzi, yangeweza kabisa kuepukwa kama sheria hiyo ingekuwa katika lugha ya Kiswahili kuanzia siku ya kwanza kabisa ya kutungwa kwake.
  Ni jambo la habati mbaya kwamba hata kwa baadhi ya wabunge sheria hii watakuwa wameipitisha si kwa sababu walijua wanafanya nini, ila kwa sababu tu waliwajibika kufanya hivyo; huu ni udhaifu kwetu kama taifa kwa sababu ni jambo la kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwamba tumejaliwa kuwa na lugha ya moja ya taifa inayozungumzwa na kila mwananchi, msomi na asiyemsomi; wa mijini na wa vijijini sawia.
  Kwa hali hii kuendelea na kasumba hii ya ukoloni mamboleo ya kuamini kwamba bila sheria kutungwa kwa Kiingereza haitimizi sifa za kisheria, ni kurudisha nyuma juhudi za kujitegemea za taifa hili, lakini zaidi sana kuzidi kuminya fursa ya watu wetu kupata elimu kwa wepesi na haraka zaidi kama tungeendesha mambo mengi kwa lugha ya Kiswahili; ikiwa ni pamoja na kutunga sheria kwa kutumia lugha ya taifa.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  May 22, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo ukimaliza masomo kwa kiswahili ukitaka kwenda kusoma nje unaanza kwanza kusoma English Course?
   
 3. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2010
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Kila kitu na chanzo chake mdau.Kama kiswahili kinaleta utata itakuwaje tukiatafsiri sheria hizo? This is a noble profession bwana!
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwa kweli kwenye sheria zitafriwe kiswahili kwani kiengereza cha sheria kigumu kweli yani
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  May 26, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sheria zitafsiriwe halafu wanafunzi wa vyuo vikuu lugha ya kufundishia ni Kiingereza, sasa watasomaje ndugu? Na lugha ya kufundishia ikibadilishwa kuwa ya kiswahili, wahitimu wakitaka kuajiriwa nchi za nje zinazoongea Kiingereza si itakuwa kichekesho? Pamoja na kwamba tunasoma kiingereza toka Shule za Msingi hadi Chuo Kikuu lakini kinatupiga chenga waTZ, hicho cha English Course tutakiweza? Tuache vichekesho jamani, tutalifanya taifa liwe isolated from the international affairs unnecessarily!
   
 6. Marry Hunbig

  Marry Hunbig JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2013
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 1,509
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Mapendekezo yango ni kwamba, Sheria ile ile moja iandikwe kwa lugha mbili, iandikwe kwa kiswahili na kwa kiingereza, hivyo wale wanaojua kiingereza wataisoma kwa kiingereza, na kutakuwa na liberty ya wasiojua kiingereza kuisoma kwa kiswahili, pamoja na kwamba wanasheria wote maadam wamepitia chuo kikuu watakuwa wanajua kiingereza na watasoma pande zote mbili kwa uelewe bora zaidi. cha kuelewa ni kwamba, mahakamani, nikianza na mahakama hizi za wilaya na mkazi, hata kama zinaendeshwa kwa kiswahili mara nyingi (pamoja na kwamba lugha za mahakama hizo ni mbili, and one can use either of them, kiswahili au kiingereza), mahakim kwenye majalada yao hata kama huendeshwa na kiswahili,wao wanarekodi kwa kiingereza, na hukumu kila kitu zinaandikwa kwa kiingereza, waendesha mashitaka hati zao za mashitaka zimeandikwa kwa kiingereza pamoja na kwamba wanasoma kwa kuzitafsiri kwa kiswahili etc. hata hivyo, kuna umuhimu sana wananchi wa kawaida kujua baadhi ya sheria, walau kidogo. kutojua kiingereza isiwe barrier kwao kuzisoma sheria, hivyo tukiziweka ziwe pande mbili, tutakuwa tumesaidia sana katika hili.

  ILA Hatuwezi kukwepa kuandika sheria kwa kiingereza, the only option is to put them in both languages, swahili and english. LUGHA YA MAHAKAMANI, KWA MAHAKAMA YA MWANZO NI KISWAHILI, MAHAKAMA YA WILAYA NA MKAZI NI KISWAHILI NA KIINGEREZA, ILA LUGHA RASMI YA MAHAKAMA KUU NA MAHAKAMA YA RUFANI NI KIINGEREZA PAMOJA NA KWAMBA KUNA MAZINGIRA YAMEONYESHA WAKATI WA KUHOJI MASHAHIDI KIKATUMIKA KISWAHILI, KISWAHILI KIMETUMIKA PIA KWENYE VIKAO VINGI VYA MAHAKAMA KUU., so we should put our laws into both languages that we use in our courts.
   
 7. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #7
  Jun 2, 2013
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kuandika Sheria kwa lugha mbili, maana yake ni kutafsiri toka lugha moja kwenda nyingine, fair enough! Ikitokea mgongano kati ya Kiswahili na Kiingereza lazima mahakama zi-resort kwenye "Controlling Version" ambayo ndiyo Bunge lilitunga Sheria kwayo!
  Kwa kifupi ni kwamba Bunge haliwezi kutunga Sheria kwa lugha mbili, lazima lugha moja itakuwa tafsiri ya nyingine!
  Mfano wa Sheria zilizotungwa kwa lugha moja (Kiingereza) na kutafsiriwa kwa lugha nyingine ni:
  1. Sheria ya Ardhi ya Kijiji, 1999,
  2. Katiba ya JMT, 1977 (Hii imetafsiriwa toka Kiswahili kwenda Kiingereza),
  3. Ward Tribunals Act, 1985,
  4. Islamic Restatements Act, nk.
  Pamoja na Sheria hizo kutafsiriwa, Mahakama zimekuwa zinatumia "Controlling Versions" zaidi kuliko Tafsiri. Kwa maana hiyo tatizo la lugha ya kisheria kuwa ngumu bado liko pale pale pamoja na Sheria kutafsiriwa kwa Kiswahili!

  Well, siafiki move yoyote ya kuandika Sheria kwa lugha mbili kwa kuwa moja haina kazi Mahakamani!

  After all, Sheria iko kwenye "spirit" na sio "letter," ndio maana inahitaji wanasheria kuitafsiri, hata kama ingeandikwa kwa lugha gani!
   
 8. Marry Hunbig

  Marry Hunbig JF-Expert Member

  #8
  Jun 17, 2013
  Joined: Sep 4, 2012
  Messages: 1,509
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
 9. I

  IDUNDA JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2013
  Joined: Oct 31, 2013
  Messages: 458
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  hahaha, u re very right, huwezi kuandika sheria kwa kiswahili pekee, kusoma tunasoma kwa kimombo, sheria pia lazima ziwe za kimombo. lakini nashauri katika kila sheria,kuwe na tafsiri mbili, tafrisi ya kiswahili na tafsiri ya kiingereza. hii itasaidia hata wasio wanasheria kuelewa baadhi ya mambo kwa kujisomea wenyewe. bofya hapa SHERIA KWA KISWAHILI
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Nov 16, 2013
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Kifupi, Kiswahili hakifai kuandikia sheria/hakina maneno ya kutosha na yanayojitosheleza.
   
 11. iparamasa

  iparamasa JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2013
  Joined: Nov 14, 2013
  Messages: 13,439
  Likes Received: 14,098
  Trophy Points: 280
  Sheria inapata ladha kama imeandikwa kwa kiingereza, kujua sheria sio kusoma vifungu tu, kuna case laws, authoritative citations,common law,rules of interpretion na mengineyo, kiswahli chenyewe ni somo na hatuna historia ya kufaulu kwa maksi za juu, na inasemekana hata nje ya nchi waalimu ni wakenya.
   
 12. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #12
  Nov 16, 2013
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Safi sana Maria. Mapendekezo yako ni murua kabisa.
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Nov 16, 2013
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Si kweli. Maneno yanaweza kuazimwa na hata kutungwa.

  Mbona hata Kiingereza kimeazima maneno mengi tu ya Kilatini hususan yale yanayotumiwa kwenye sheria na utabibu. Unadhani 'in flagrante delicto', 'habeas corpus', au 'certiorari' ni maneno ya Kiingereza hayo?

  Tuache uvivu na kujiona hatuwezi. Sheria zinaweza kabisa kuandikwa kwa Kiswahili au hata kwa lugha zote mbili.

  Tatizo ni kwamba tayari tulishalishwa ujinga wa kuona kwamba Kiingereza kina hadhi ya juu kuliko Kiswahili wakati si kweli hata kidogo.
   
 14. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #14
  Nov 16, 2013
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Ama kweli sisi Miafrika hakuna jambo lolote lile zuri ambalo tunaliweza ikiwa hata kutunga sheria zetu wenyewe kwa kutumia lugha yetu wenyewe hatuwezi!

  Kazi yetu kuiga iga tu ya wengine. Hatuna vya kwetu. I mean, sheria ni zetu wenyewe halafu tunashindwa hata kuziandika kwa kutumia lugha yetu? Quintessential unadulterated dumbassness.

  Africans are too dumb!
   
Loading...