Bwana Kheri
Member
- Oct 31, 2018
- 26
- 49
Leo ni Siku ya Uhuru. 9 December. Ni siku muhimu sana kwa nchi yetu. Pamoja na umuhimu huo, nawakumbusha Watanzania wenzangu. CCM na msiokuwa CCM. Chadema ama CUF, sote kwa pamoja tunapaswa kuuchukia muswada mpya wa vyama vya siasa kwasababu unatugawa Watanzania na hauna tija. Ingawa muswada huu utapigiwa debe sana na watu wa CCM, lakini CCM wanapaswa kujua kwamba nchi yetu sio mali binafsi ya CCM na wana CCM.
Itakapotokea siku CCM imeanguka, chama hiki kikongwe kitashindwa kujiendesha kwa sababu ya kupitisha sheria ngumu na kandamizi kwa sababu ya kuvihujumu vyama vya siasa vya upinzani. Hivyo CCM na wafuasi wake wakiwamo wabunge wao waupitishe muswada huu kama wanajua chama chao kitatawala milele, la kama kuna siku CCM itakuwa chama cha upinzani, please, Watanzania wenzangu tusikubali kabisa muswada huu upite kwa maslahi mapana ya nchi yetu bila kuangalia itikadi za vyama vyetu. Tanzania ni bora kuliko vyama vyote vya siasa.