Sheria za pesa ili ufanikiwe

Elisha Chuma

JF-Expert Member
Jul 22, 2013
282
272
15870990914c0d44a464b3a13d31fbb8.jpg



Tumekaririshwa sheria inapatikana mahakamani na kwa wanasheria lakini ukiangalia kwa undani kila siku tunatimiza sheria na kanuni za maisha,chakula ,mazingira,kazi kila kitu lakini kwenye pesa kwa vile huwa pesa ni mtatuzi wa matatizo watu husahau kama pia pesa inasheria zake ambazo zinatakiwa zifuatwe na ikiwa unahitaji kufanikiwa ni lazima uzifuate na bahati mbaya zaidi sheria za pesa huwa zinabadilika, kuna sehemu unatakiwa kubana matumizi na kunasehemu unatakiwa utoe pesa ndio upate pesa lakini pia kuna sehemu ambapo unatakiwa kuweka tu na malipo ama hiyo pesa itarudi kwako baadae ( Uwekezaji), Ukizikosea njia ama mbinu hizi mwisho wake utajikuwa sehemu ya kutoa pesa ili upate umebana matumizi na sehemu ya kubana umetoa.

Mfano: Katika biashara yako ni mfano wa sheria ya kutoa pesa ili upate pesa, lakini katika matumizi yako binafsi ni sehemu nzuri ya kubana matumizi,ila katika uwekezaji wako ni sehemu nzuri pia ya kuweka kwa muda mrefu.

Hivyo ni lazima kutambua haya ili utembee katika sehemu husika na ile ambayo itakufikisha kwenye malengo yako stahiki kwa wakati sahihi.

Elisha Chuma
Mwalimu/Mshauri wa Chapa, Ujasiriamali,Biashara na Uchumi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom