Sheria za mkopo wa benki

Swelana

JF-Expert Member
Sep 24, 2016
418
1,259
Habari,
Jamani naomba kusaidiwa kiushauri kuhusu mkopo niliochukua benki fulani ambayo kwa sasa imefilisiwa na serikali.
Mkopo nilikopa mwaka 2012 kwa makubaliano ya kulipa miaka mitatu yaani mpaka 2015,mkopo wa mil 5
Wakati nachukua mkopo nilidhaminiwa na mwajiri wangu ambapo sehemu niliyofanya kazi ilikuwa ni shule ya mmliki wa hiyo benki pamoja na hati ya kiwanja changu ambacho lengo ilikuwa kukopa ili niongezee pesa niliyokuwa nayo na nijenge nyumba na kweli nikafanikiwa nikajenga.

Nilianza kulipa mkopo huo mwaka 2012 mpaka 2013 mwishoni kwa kukatwa kwenye mshahara,bahati mbaya tukashindwana na mwajiri na akawa ameninyima mkataba tena hivyo nikawa kitaa kwa muda kama miezi 8 bila kibarua hivyo sikuwa nimepeleka marejesho wakati huo nimeshalipa kama mil 3.2 na imebaki kama mil 4.8 kwani nilipaswa kulipa mil 8 kwa mkopo wa mil 5.
Sasa baada ya kukaa bila kupeleka marejesho kwa muda wa miezi kama 8 deni likapanda tena mpaka mil 5.4.
Wakati nimeanza kujiajiri nikawa nimefanikiwa kupunguza mpaka likafika mil 4.8 na ghafla ikatangazwa benki hiyo imefilisika so nikaenda kujua hatma ya mkopo nikaelezwa ni lazima niendelee kulipa sawa nikaendelea.
Lakini sasa nina muda kama wa miezi 4 kila nikipeleka marejesho hawanipi risiti za mashine tofauti na fomu ya kujaza kuweka hela na pia wananiambia niendelee kulipa watanipa balance ya kiasi kilichobaki badae kila nikipeleka wananiambia watanipa balance badae.

Sasa waungwana na GT wa Jf limekaaje hili?
Hivi benki iliyofilisiwa kwa waliokopeshwa huwa inakuwaje?
Msaada tutani na sitaki kebehi za kipuuzi.

Swelana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bank ikifilisika inawekwa chini ya msimamizi au mfilisi au inabaki chini ya uangalizi wa benki kuu. Kazi yao ni kukusanya madeni ya benki iliyofilisika, unachopaswa kufanya ni kujua mfilisi wa benki yenu ni nani, kama ukishindwa kumpata nenda benki kuu watakupatia taarifa zote zinazohusu benki yenu.
 
You are right
 
Asante mkuu,sasa na hili la kulipa bila kupewa balance nifanyeje?

Back
Top Bottom