Sheria za kufuata unapotaka kumuacha Mke kwa talaka

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
523
1621935170903.png

BAADHI YA MWASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU WA JF
Ndugu WanaJamiiForums naomba mnisaidie katika hili swala. mimi ninamwanake ambaye nimeishi naye muda wa miaka 6, tukabarikiwa kupata mtoto mmoja ana miaka 5.

Tuliishi kwa shida sana maana nilimuoa nikiwa nasoma lakini Mungu akatubarikia mpaka mwaka jana mwezi September niliondoka kuja kimasomo shahada ya pili. Kabla sijaja huku nilikuwa nimeajiriwa Wizara ya Maji na Umwangiliaji kipindi kile

Kutokana na kuwa nina familia niliondoka nikaenda NMB, mshahara wangu unakopitia nikaweza kupata form ya kujaza na kwenda mahakamani kuapa ili mshahara wangu mke wangu awe anachukua kama kawaida kwa kutumia account yangu.

Tangu kipindi hicho kulikuwa hakuna tatizo lakini karibuni nilianza kupata tuhuma mke wangu ana madeni mengi sana nikajaribu kumuuliza kilichofuata hapo ni matusi na kejeli za kila aina, ndipo nilipo amua kuacha yote ili niendelee na masomo mpaka December au January mwaka kesho nitakapo kuja likizo.

Nilikuwa nataka niachane naye maana siwezi ishi na mwanamke anaye tukana wazazi wangu na hata mimi.

Vitu tulivyo navyo ni kiwanja na tumejenga kijumba cha vyumba viwili na sebule. Naomba ushauri wenu wakisheria maana amekuwa akiandika hata sms za kutaka kumuua mtoto hata wakati mwingine kupiga simu nakuongea haya maneno ndio maana nimekaa kimya siwezi hata kuwasiliana naye na sms hizo ninazo hapa.

Je, ustawi wa jamii watakubaliana na mimi kuchukua mtoto akakae hata na mama yangu? Maana kunauwezekanao akamuua mtoto wakati wowote maana mimi bado nasoma naniko mbali sana.

Natanguliza shukurani zangu na MUngu awabariki sana.
Ndugu zangu ndoa sasa hivi inawaka moto nimeishi na shemeji yenu miaka kumi ila sasa naona ni wakati sahihi kila mtu achukue time yake.

Naomba msaada wa kisheria ili tuachane kiamani kila mtu akafanye mambo yake kuanzia utaratibu wa kutoa taraka mpaka mwisho wa mahakama na kuchukua cheti changu cha talaka.
Naomba kujua ndoa ya kiislam ili ihesabike imevunjika rasmi huwa ktk stage gani ya talaka? Talaka tatu na maana zake kila moja
Wananzengo!!
Tushauriane jinsi ya kumsaidia huyu dada, ameachwa. Scenario iko hivi:

Kuna scenario kwamba watu walioana kwa ndoa ya kanisani kisha wakaingia mgogoro ndani ya miezi michache tu, mke akatoroka, akarudi kwao. Kisha baada ya miezi kadhaa akafuata mali zake kwa mumewe (zake/walizochuma pamoja), mumewe akubali kumpa kwa sharti la kwamba pawepo na mashahidi. Mke akatafuta mashahidi na mume akatafta mashahidi pia (miongoni ni wazazi wa mume na mke). Aliitwa pia polisi na balozi wa mtaa kusimamia usalama kwakua palikua na tishio la kuibuka kwa ugomvi wakati wa kugawana vitu.

Mume akaweka sharti mbele ya mashahidi kwamba waandikishane kwanza kila mali atakayochukua mwanamke na ikadraftiwa "hati ya kugawana mali" pale nyumbani na hati ikaeleza wazi kwa maandishi kwamba mke kachukua chake kwasababu "ndoa imevunjika"....wanandoa na mashahidi, polisi na balozi wakaweka sahihi zao na kila mmoja (mme, mke na polisi) wakapata nakala.

Kisha mke akaondoka na vitu vyake akarudi kwao na mume nae akaendelea na maisha yake, hawakuwa na mawasiliano tena. Lakini talaka ya mahakama haijatolewa mpaka sasa na wala hawajafanya mchakato wa kwenda mahakamani, ni mwaka tangu wamegawana mali.

Maswali:
1. Je, ndoa bado ipo kisheria? Kwanini?
2. Je bado wanandoa wanayohaki ya kuenforce ndoa yao (eg. Kukamatana ugoni)
3. Nani anayohaki ya kufungua shauri lolote kuhusu status hii. (e.g mke kudai arudi/ mume kudai mkewe)
4. Kuna makosa yoyote kisheria?

UFAFANUZI WA KISHERIA KUHUSU TALAKA TANZANIA
Talaka kisheria
Neno talaka linaweza kuwa mojawapo ya maneno yaliyozoeleka midomoni au masikioni mwa watu wengi katika ulimwengu wa sasa.

Kwa lugha nyepesi, talaka ni kitendo cha wanandoa kuachana na mahusiano ya kindoa yaliyokuwa baina yao.
Lakini kisheria, ingawa maana ya talaka inaakisiwa na maana hii ya Kiswahili, lakini katika maana ya sheria kuna mambo mengine zaidi ya kuzingatia.

Tafsiri ya sheria ya ndoa ya Tanzania, sura ya 29 ya marekebisho ya sheria ya mwaka 2002, talaka ni kitendo cha mahakama yenye mamlaka katika shauri linalohusika, kutoa tamko la kuivunja ndoa iliyokuwapo, kwa sababu mbalimbali.

Hivyo, tukiangalia kwa mtazamo wa kihistoria, ndoa kwa mujibu wa sheria ya Kiingereza (common law) ambayo imeakisiwa sana na sheria ya ndoa ya Tanzania, ilikuwa haitambui sababu ya aina yeyote katika kuivunja ndoa kwa msingi wa talaka.

Lakini baada ya miaka mingi kupita, sheria ya talaka ilianza kutumika nchini Uingereza baada ya sababu kadhaa za kisheria za kuvunja ndoa kwa talaka kuanzishwa.

Sheria ya Talaka (The Divorce Act) ya mwaka 1969 ilianzishwa nchini Uingereza kufuatia ripoti ya askofu Kent wa nchini humo.

Mwaka mmoja baadaye yaani mwaka 1969 serikali ya Tanzania kupitia tamko la serikali (Government Notice) namba 1 ya mwaka huo, iliyojulikana kama White Paper ilichukua msimamo na mtazamo huu wa sheria ya Kiingereza juu ya talaka.

Hadi mwaka 1971 tulipochukua msimamo huu wa sheria ya Uingereza juu ya talaka, mabadiliko makubwa ya kimsingi ya sheria juu ya talaka yalitokea katika sheria yetu hapa nchini nayo ni pamoja na kuwa na sababu moja tu inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na mahakama kwa tamko la talaka, sababu hiyo ni kuwa mahakama itakapothibitisha kwamba ndoa hiyo imevunjika kabisa na haiwezi kurekebishika kutokana na kasoro zisizo weza kurekebishika.

Hivyo, sheria ya Tanzania katika hili nayo ikachukua sababu moja inayoweza kuifanya ndoa kuvunjwa na talaka.
Hata hivyo, wakati tunaangalia sheria hii, tunatakiwa kujua kwamba sababu moja ya kuivunja ndoa kwa talaka ipo Tanzania bara pekee.

Baadhi ya watu wanadhani sababu za kuvunja ndoa ni zile zinazoelezewa na sheria hii kama hali au mazingira ya kuthibitisha kwamba ndoa hiyo ina tofauti zisizorekebishika.

Sababu hizo ni pamoja na uzinifu nje ya ndoa, ukatili pamoja na kumkimbia/kumtelekeza mwanandoa mwezako. Uzinifu ni mojawapo ya sababu zinazoipa mahakama mamlaka kisheria kuivunja ndoa yoyote. Hata hivyo, unatakiwa kujua uzinifu una maana nyingi kutegemea na eneo husika.

Kimsingi uzinifu ni kitendo cha mwanandoa mmoja kufanya ngono nje ya mahusiano yake ya ndoa iliyo halalishwa.
Hapa katika kuondokana na wasiawasi wa kuweza kushindwa kuthibitisha uzinifu, sheria imetoa dhana kwamba pale tu itakapokutwa mume na mke wamelala pamoja na wako watupu, basi dhana hapa ni kwamba wametoka au wanataka kufanya ngono.

Dhana hii kama ilivyoanzishwa na mahakama katika shauri la Denise dhidi ya Denise, Jaji Single anasisitiza kwamba dhana hii ni ngumu kuipinga isipokuwa kama itathibitika kwamba mwanaume aliyekutwa ni hanithi au mwanamke huyo ni bikira. Na uthibitisho wa uzinifu nje ya ndoa ni kama uthibitisho wa katika kesi ya jinai ambapo anayelalamika anatakiwa kuithibitishia mahakama pasi na shaka kwamba uzinifu umetokea.

Kwa upande wa Uingereza, kama itathibitika kwamba kulikuwa na uzinifu na kwamba mtoto alizaliwa nje ya ndoa, pia atahesabika ni mtoto haramu na hivyo kukosa haki zake zote kwa mzazi wake wa pili.

Hata hivyo, mara nyingi uzinifu unaweza kuthibitishwa na ushahidi wa mazingira kama vile mmoja wa wanandoa kuwa na ugonjwa wa zinaa na kadhalika.

Kifungu cha 170(2) cha sheria ya ndoa ya Tanzania, kinatoa maelekezo juu ya ushahidi wa aina hii.

Hata hivyo, uzinifu si lazima uwe sababu ya mahakama kutoa talaka. Mahakama kwa kuzingatia mazingira ya kesi husika inaweza kuamuru mtu aliyefanya uzinifu na mmoja wa wanandoa kumlipa fidia muathirika wa uzinifu huo.

Ukatili pia ni sababu mojawapo ya sababu zinazoweza kuithibitishia mahakama kwamba ndoa hii ina kasoro zisizoweza kurekebishika.

Kuharamisha, kubatilisha ndoa katika Sheria ya Ndoa
NENO kuharamisha ni la kawaida katika lugha ya Kiswahili ambalo linalotokana na neno ‘haramu’ likimaanisha kitu kisichofaa, kwa maana iliyo nyepesi.

Aidha kuharamisha ndoa kisheria ni kitendo cha mahakama kutoa tamko kwamba ndoa ambayo iliyodhaniwa kuwa imefungwa haikufungwa wala haikuwapo.

Hapa tunatakiwa tujue mantiki ya kitendo hiki ni kuharamisha (nullify) ndoa ambayo ilidhaniwa ni halali wakati wa kufungwa, lakini kumbe katika jicho la sheria ndoa hiyo “haipo na wala haikuwahi kuwapo”.

Hii siyo talaka kama ambavyo watu wengine wanaweza kufikiri. Somo la talaka tutalizungumzia baadae katika makala nyingine.

Kama ambavyo nadharia nyingi za sheria zetu zimetoka katika sheria za mahakama za nchini Uingereza, yaani Common law, nadharia hii imetoka huko huko, wakati wa mageuzi baada ya kuanguka kwa dola ya utawala wa kifalme wa Kirumi huko Ulaya.

Wakati wa utawala wa kirumi huko Ulaya, sheria za Kanisa Katoliki zilikuwa zinatumika kwa kiwango kikubwa, imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki ndoa ni Sakramenti iliyoanzishwa na Mwenyezi Mungu.

Hii ilikuwa na maana kuwa ndoa ni takatifu hivyo talaka ni kitu ambacho hakitambuliki katika sheria za Kanisa, kusisitiza maneno ya bwana Yesu katika Injili ya Marko 10:7-8 kwamba mwanaume na mwanamke wakiungana wanakuwa mwili mmoja na kwamba alichokiunganisha Mungu mwanadamu yeyote asikitenganishe.

Kwa mantiki hiyo, njia pekee ya watu kutoka ndani ya ndoa wakati huo ilikuwa ni kuiharamisha na si talaka, kwani ilikuwa haitambuliki kama tulivyoona hapo awali. Baada ya kuanguka kwa dola ya Rumi huko Ulaya, tawala za kifalme zikawa maarufu sehemu nyingi huko Ulaya na kusababisha sheria za kanisa (Canon law) kupotea na kwa upande wa Uingereza, sheria za mahakama za Uingereza yaani Common law zikashika kasi.

Hivyo basi athari ya sheria hizi za mahakama za Uingereza ilikuwa ni pamoja na kuleta mafundisho mengine ikiwemo kuanzisha upya talaka.

Kwa Tanzania, vifungu vya 39 na 49 vya Sheria ya Ndoa, 1971; vinaelezea njia mbili kuu za kuharamisha ndoa. Njia hizi ni zile ambazo ikithibitika mahakamani, basi mahakama itatoa tamko la kuharamisha ndoa.

Njia hizi ni pamoja na ndoa haramu (void marriage) na ndoa isiyo haramu lakini pia si halali kwa kuwa imekosa mahitaji kadhaa ya kisheria yaani ndoa batili (voidable marriage).

Kwa ndoa haramu, hii ni ndoa ambayo tangu mwanzo ilikuwa ni haramu katika jicho la sheria; wakati aina ya pili ya ndoa isiyo haramu ila imekosa kutimiza masharti kadhaa ya kisheria kuifanya iwe halali na hivyo kuifanya batili.

Kwa mfano kwa mwanamme asieweza kufanya tendo la ndoa na mkewe, ndoa yake itakuwa batili kama mkewe atakwenda mahakamani kuomba ndoa yake ibatilishwe kwa kuwa mumewe hawezi kufanya tendo hilo ambalo ni hitaji la kisheria ili ndoa iwe halali; lakini kama mwanamke huyo atavumilia hali hiyo, ndoa yao itakuwa ni halali.

Hivyo basi, kwa mujibu wa kifungu cha 39 na 49 vya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, kuna sababu mbalimbali ambazo zinaweza kusababisha ndoa isiwe halali, kwa sababu hizo mume au mke anaweza kuomba mahakama itoe tamko la kubatilisha ndoa yake.

Kwa wanandoa kushindwa kufanya tendo la ndoa wakati wameoana, kwa mujibu wa kifungu cha 39(e) cha Sheria hii, pindi mwanandoa yeyote (mwanamme au mwanamke) wakati wameshafunga ndoa na mwenzake atashindwa kufanya tendo la ndoa hiyo itakuwa sababu kwa mmojawapo kuomba tamko la kubatilisha ndoa hiyo.

Huu pia ni uamuzi uliotolewa katika shauri la Dralge dhidi ya Dralge , (1947)1 All.ER 29), la nchini Uingereza,ambapo mahakama ilitafsiri kimantiki kwamba tendo la ndoa ndilo haswa linalomaanishwa katika kile ambacho kifungu cha 39 cha Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971.

Kwa MASWALI na MAJIBU, fuatilia kuanzia post ya 2 katika thread hii. Pia, kwa ufafanuzi zaidi wa kisheria, soma viambatanishi katika PDF format kwenye bandiko hili.

MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF
Aise, pole sana ndg yangu kwa hilo, wanawake bwana!

Je, mlifunga ndoa gani?
Nenda Mahakamani ili kuvunja ndoa hiyo haraka na hizo msg usizifute ndio utakuwa ushahidi wako ukiwa mahakamani.

Kuhusu mtoto, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatakiwa kuwa chini ya mama yake ingawa mtoto kama anaweza kujieleza vizuri anaweza kutoa msimamo wake mahakamani kwamba ataishi na nani kati ya baba na mama. Lakini pia mahakama inatumia kigezo cha hali ya uchumi kati ya baba na mama ili kuamua ni mzazi yupi amtunze mtoto huyo.

Kwa kesi yako, kwa vile mama anamtishia kumuua mtoto hizo meseji usizifute kwani zitakusaidia pia wewe mahakamani kama ushahidi wako kwamba huyu mama hawezi kumtunza mtoto kwani anatishia kumuua. Aidha, kutishia kuua ni kosa la jinai
Facts ulizotoa ni limited sana kuweza kupata ushauri wa kisheria. Hatujui hata ni ndoa ya aina gani. Whatever the case, unless mkubaliane ku divorece, itakubidi uwe na ushahidi kuwa ndoa imevunjika beyond repair. Itakubidi uonyeshe kuwa kati ya sababu zifuatazo zimefanya ndo yako ivunjike.

(a) adultery committed your wife, particularly when more than one act of adultery has been committed or when adulterous
association is continued despite protest;
(b) sexual perversion on the part of your wife;
(c) cruelty, whether mental or physical, inflicted by your wife on you or on the children, if any, of the marriage;
(d) wilful neglect on the part of your wife;
(e) desertion of you by your wife for at least three years, where the court is satisfied that it is wilful;
(f) voluntary separation or separation by decree of the court, where it has continued for at least three years;
(g) imprisonment of your wife for life or for a term of not less than five years, regard being had both to the length of the sentence and to the nature of the offence for which it was imposed;
(h) mental illness of your, where at least two doctors, one of whom is qualified or experienced in psychiatry, have certified that they entertain no hope of cure or recovery;
(i) change of religion by your wife, where both parties followed the same faith at the time of the marriage and where according to the laws of that, faith a change of religion dissolves or is a ground for the dissolution of marriage.

Kama ndoa ni ya Kiislamu itabidi upate certificate toka kwa bodi husika kuwa wamejaribu kuwasuluhisha lakini iimeshindikana. Mie nafikiri hakuna haja ya kukimbilia divorce. B'se inaonyesha kabla ya kwenda masomoni mlikuwa mnaishi vizuri tuu. You need to find out yourself what exactly happened. Mambo ya divorce yatawacost sana si nyie tuu bali pia mtoto. Hapa zinahitajika busara na hekima za hali ya juu. Weka emotions pembeni. Kufanya maamuzi magumu kama haya kwa kutumia emotions ni mbaya sana.

Pia kumbuka wakati ukiwa huko masomoni mke wako kama mwanamke mwingine anakuhitaji wewe kama mume zaidi ya pesa zako za mshahara. Ushauri wangu ukirudi likizo, usimkurupushe. Kaa nae chini mzungumze kama mume na mke. Don't rush to divorce. Tofautisha kati ya irretrievable breakdown and a temporary rift. Kama anakutumia messages za kukutukana, wala usimjibu kwa kumtukuna. Wasiliana nae kama mke wako.

Pia mkuu jiangalie wewe mwenyewe unaweza ukawa ni cause ya breakdown. Lugha yako kidogo inanitia wasiwasi. Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa. Sijui kama unam-underrate kwa sababu ya yaliotokea au ndio huwa unamwita hivyo?
Laka EMT Nimekupata sana kweli sio hata mimi ninasema tuachane maana najitahidi sana kuwa nayekaribu hasa ukizingatia January mwaka huu mama yetu(i mean mama mkwe) alitangulia mbele ya haki kweli lilikuwa nipigo kubwa kwake na hata kwa familia nzima yetu ukizingatia nilikuwa mbali ndio maana ninajitahidi sana kutoa ushauri na Lugha za kumfariji kila wakati.

Tatizo nipale unapokuwa mumeongea vizuri kabisa bila hata kukwaruzana lakini baada ya muda may be 6hr. unapokea sms inanitukana tena matusi yanguoni akiakaa muda may hata siku 1 au 2 anaomba msamaha.

Ukimwuliza kwa nini uliandika sms anakujibu ni hasira, ukimuuliza hasira zinatoka wapi kama wakati tunaongea hatukugomabana anasema alipata hasira tu. Kwa mfano juzi amenitukana wee kwenye sms jana usiku akaandika sms yakuomba msamaha sasa tutaishi maisha ya aina gani? kuna mambo ambayo nahisi kuwa pengine anakunywa pombe au kama hanywi basi anaweza kuwa na matatizo ya akili kwa sasa au kunajambo alilofanya mbaya linamchanganya kwennye akili hasa niliposema naenda likizo.

"Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa" kwa hili nimekoseha mkuu haikuwa intention yangu
kaka pole sana nayaliyokupata. Kuachana sio sulihisho kabisa kaka.chakufanya Mwombe M ungu akupe uvumilivu umalize masomo vizuri na utakaporejea mweke mkeo chini muongee kama marafiki atakueleza hela alifanyia nini inawezekana ulimuuliza kwa ukali au kunakitu anachokifanya kwa siri na hizo hela nikumsihii wote muwe wawazi katika maisha yenu mtaishi kwa amani.

Suala la kutukana lazima liwe na sababu kwani kama mmeishi wote siku zote hajakutukana iweje sasa maybe ua the course men.kaeni myasuluishe kwa amani hatua mlofikia ni nzuri kimaisha haitapendeza kila mmoja awe peke yake na vlevle mtamnyima mtoto malezi bora.

Kaka ukumbuke distance maranyingi inavunja mahusiano kilichopo kua mpole kama unampenda mkeo anza kujikomba kwakwe,jishushe kabisa kaka uanze kuirejesha amani ndo mengine yatadhihirika kaka hamna siri chini ya jua.ila kuachana sio suluhisho kabisa unaweza ukapata mwingine ambaye ni nyoka.shika sana ulichonacho kaka.hiyo hela isiwaachanishe mmetoka mbali sana
Bro, kutukanana tu kwenye ndoa ni sababu ndogo sana ya kuweza kuachana, nakushauri vumilia. matusi ni kitu kidogo sana rafiki yangu. Mimi mke wangu hata akinitukana siwezi umiza kichwa sana labda kama kufumaniana hapo ndio kesi nyingine, kwani kwanza inategemeana amenitukana kwa sababu gani, pengine siku hiyo ameamka vibaya na ukizingatia umetuambia mama yake amefariki pengine inampa stress hivyo ukimgusa kwenye kovu analipuka.

Wewe ulipokuwa ulikuwa hutukani sijui ulikulia mazingira gani ambayo hayana challenges ndogondogo kama hizi, kama ulikulia maisha ya kijeshi kama sisi wengine unatukanwa unachapwa unanyanyaswa hadi inafika kipindi unakuwa sugu na kuweza kuishi maisha yeyote yale na kuishi na mtu yeyote yule ukammudu, hasa kutukanwa na mwanamke ni kitu kidogo sana na lazima kuna sababu iliyofanya akutukane.

Sisapoti kukutukana ila nasema hiyo sababu inavumilika kwa wanandoa na si sababu ya kuachana. kwa kifupi, kwa mwanaume aliyekamilika kiutu uzima na mwenye uwezo wa kukaa na familia, yote hayo uliyoyaongea ni ya kuvumilia na kurekebishana tu tena kwa maneno ya mdomo tu. ungeniambia umemfumania hapo nisingekuwa na la kusema kwani hiyo ingekuwa kesi kubwa, ila matusi tu?

kwani kwenye maisha yako hujawahi tukanwa, uyo wife wako ndio wa kwanza kukutukana? amekutukana unataka kumuacha? unafikiri huyo utakayeenda kumuoa hatakutukana? kama sababu unayotaka kuachana na mkeo ndio hii, aisee utaacha na kuoa kuacha na kuoa hata mara 20.

zaidi ya yote, mtu anayetukana sana hivyo sio yeye, ni shetani tu anamtumia, na pengine shetan ameona ndoa yenu ikiendelea mtafanikiwa sana sasa anataka akuachanishe ili mvurugikiwe wewe na mkeo na mtoto wenu.

bofya hapa kwenye link yangu SHERIA KWA KISWAHILI
Sio sahihi mkuu, kwa mujibu wa sheria ya ndoa ya Tanzania, ndoa za namna tatu ndo zinatambulika nchini kwetu nazo ni Civil Marriage (Ndoa za Kiserikali/Bomani), Customary Marriage (Ndoa za Kimila) na Religious Marriage (Za kidini na hapa hususani inakusudiwa Dini ya Kiislam). Ikiwa ndoa ya KIISLAMU inatambuliwa na Sheria basi bila shaka na utaratibu wake wa kuachana (talaka) unatambulika na kukubalika pia.

Kuna Mashauri mengi tu ambayo yanapelekwa Mahakamani na wanandoa waislamu na sheria inayotumika katika kuhumu kesi yao ni sheria za kiislamu iwapo ndoa hiyo kimsingi ilifungwa kwa taratibu za kiislamu. Kinachofanyika Mahakamani ni kwenda kutafuta Amri (Divorce Decree) tu ya Mahkama na sio kuachanishwa na hii sio lazima waislamu kuifanya, na mahkama haitoi hiyo Decree kwa wanandoa waislamu mpaka ijiridhishe kuwa tayari talaka 3 zimeshatimia kwa mujibu wa sharia za kiislamu....eg. Mahkama haiwezi kutoa Divorce Decree ikiwa mwanamke kaachwa talaka moja coz kimsingi hapo inakuwa ndoa haijawa irreparably broken down (ndoa imevunjika na haiwezi kutengemaa tena) ambapo hatua hii inafikiwa tu ikiwa talaka tatu tayari zimeshatoka.

Ukisema talaka za kiislamu hazitambuliki rasmi katika kuvunja ndoa inamaana kwamba hao wanandoa watatambulika kuwa bado ni mume na mke jambo ambalo sio sahihi kwa maana kwa mujibu wa sheria yao ya kiislamu hawana ndoa tena...kama hivyo ndivyo, sasa ni nini msingi wa kusema sheria ya bunge haitambui talaka ya kiislamu? na ilhali ama itambue au isitambue hao watu tayari wameshaachana...?

Na hii dhana yako ukiipeleka kwenye suala la mirathi iwapo huyo mume atafariki utaona kabisa inavyokufa kifo cha kawaida. Mke akiachwa hana tena haki ya kumrithi mtalaka wake, swali la kujiuliza jee, huyu mke ambae aliachwa kwa kufuata utaratibu wa kiislamu tu, lets say kwa kutamkiwa tu kuwa ameachwa na hakuwahi kurejewa tena mpka mume anakutwa na umauti, anaweza kwenda mahakamani kudai mirathi ya marehemu mumewe kwa sababu tu Talaka yake haikutolewa na mahakama hivyo haitambuliki na bado alikuwa mke halali wa marehemu? hivyo mahakama impatie haki yake ya mirathi?
Kwa maana ya ndoa ni muunganiko wa hiari baina ya watu wawili MKE na Mme , kuna ndoa aina 2 polygamous & monogamous naenda kwenye mada linapotokea suala la migogolo kwenye ndoa kuna mahakama au board inayotambuliwa na sheria inaitwa reconciliatory board ,
Hii board ni ya usuluhishi ikishindwa Ku reconcile inatoa hat ya kwamba imashindwa ndo suala linaenda mahakamani ,

Suala la talaka mahakama hai force mpaka petitioner aombe talaka na makahama ijiridhishe kuwa ndoa ime break down irreparably ili itoe talaka
Hii IPO under sec 107 sheria ya ndoa ya mwk 1971. Evidence that marriage broken down .
Na mahakama inaweza kutoa order zifuatazo yaani
1.Dicree of divorce
2,Dicree of annulment
3. Order of separation
4, Order of maintenance

Kwa scenario hiyo hao mashahidi wazazi na polisi hio inaweza kuwa kutumika tu kama ushahidi wa kugawa Mali lakini ndoa haijafa maana hakuna ushahidi unaoonyesha ndoa ime break down irreparably hao ni wanadoa bado ila wametengana tu kwa io hakuna hatua ya kisheria iliyotumika hapo ,hata kwenye reconciliatory board haijapelekwa ingekuwa kila MTU anaamua anavyojisikia hizi board na mahakama zisingekuwa na nguvu, kwaio kuzingatia sheria ndoa njia pekee yako mambo mengi sana sheria ya ndoa imeeleza kuhusiana na migogolo ya ndoa.kuna kesi ambazo zimeripotiwa mfano kesi ya bi HAWA Mohammed vs IDD self 1983 TLR 32 na kesi ya ATHANAS MAKUNGWA v DARIN HASANI 1983 TLR 132 HC.
Kwa io kesi hizi utaona umuhimu wa boards na mahakama
# Obiter dictum. #

PIA SOMA:
- Sheria ya Ndoa: Maswali na majibu mbalimbali
 
Du pole sana, wanawake tunalilia sana haki zetu, what about those who misuse them, is there any adhabu 4 them?
 
Aise, pole sana ndg yangu kwa hilo, wanawake bwana!

Je, mlifunga ndoa gani?
Nenda Mahakamani ili kuvunja ndoa hiyo haraka na hizo msg usizifute ndio utakuwa ushahidi wako ukiwa mahakamani.

Kuhusu mtoto, kisheria mtoto aliye chini ya miaka 7 anatakiwa kuwa chini ya mama yake ingawa mtoto kama anaweza kujieleza vizuri anaweza kutoa msimamo wake mahakamani kwamba ataishi na nani kati ya baba na mama. Lakini pia mahakama inatumia kigezo cha hali ya uchumi kati ya baba na mama ili kuamua ni mzazi yupi amtunze mtoto huyo.

Kwa kesi yako, kwa vile mama anamtishia kumuua mtoto hizo meseji usizifute kwani zitakusaidia pia wewe mahakamani kama ushahidi wako kwamba huyu mama hawezi kumtunza mtoto kwani anatishia kumuua. Aidha, kutishia kuua ni kosa la jinai
 
1.Ni kazi kubwa mwanamke amuue mwanawe. UWE NA AMANI.
2.Wewe nawe ulimweleza nini hadi akutukane? au nawe ulianza kumnyanyasa kwa vile anachukua mshahara wote??
3.Hata hivyo sioni sababu ya msingi ya kumuacha mkeo. VUMILIA akili yako yote iweke kwenye masomo,IWAPO ukirudi masomoni
ukakuta ana mimba au ana mtoto mwingine hapo waweza kudai TALAKA.

Nahisi kama kuna jamaa anakuchakachulia mkeo vileeeeeee???? LAKINI USIJALI MAISHA NDIVYO YALIVYO.
 
1.Ni kazi kubwa mwanamke amuue mwanawe.UWE NA AMANI.
2.Wewe nawe ulimweleza nini hadi akutukane??? au nawe ulianza kumnyanyasa kwa vile anachukua mshahara wote?...
sija mnyanya ila nilikuwa namuuliza tu kuhusu deni alilokopa kwa jamaa yangu 100000 kurudisha baada ya mwezi 1 tsh 150000 na huku anapata mshahara lakini kilichofuata hapo ni matusi na kusema kwa kuwa waliomkopesha hatawalipa maana hawana ustaarabu baada yakunieleza mimi lakini nikajitahidi nikamtumia hela ili alipe hilo deni akapeleka kwao hiyo hela kwa kisingizio kuna mgonjwa nitamsaidiaje hapo?
 
Aise, pole sana ndg yangu kwa hilo, wanawake bwana!

Je, mlifunga ndoa gani?
Nenda Mahakamani ili kuvunja ndoa hiyo haraka na hizo msg usizifute ndio utakuwa ushahidi wako ukiwa mahakamani...
nashukru sana mkuu tuko pamoja lakini mimi sio muda mrefu nitarejea kwenye likizo kwa hiyo mimi nataka nimpatie talaka ili kama kuna mtu anamdaganya wakagange maisha yao
 
jibu maswali yafuatayo↲
Je mna ndoa ya msikit au kansani?↲
Kama mna ndoa ni ngumu sana kumwacha ila unatakiwa uoneshe mahakama your marrage is not reparable ↲
Ka hukufunga ndo S.66 of Marrage Act ni presumption umemuoa so mtagawana mali kuhusu mtoto Child Act inatoa ka yupo below 7 yrz ataenda kwa mama bt unaweza shawish mahakama ikupe ni pm tuonge kirefu
 
Facts ulizotoa ni limited sana kuweza kupata ushauri wa kisheria. Hatujui hata ni ndoa ya aina gani. Whatever the case, unless mkubaliane ku divorece, itakubidi uwe na ushahidi kuwa ndoa imevunjika beyond repair. Itakubidi uonyeshe kuwa kati ya sababu zifuatazo zimefanya ndo yako ivunjike.

(a) adultery committed your wife, particularly when more than one act of adultery has been committed or when adulterous
association is continued despite protest;
(b) sexual perversion on the part of your wife;
(c) cruelty, whether mental or physical, inflicted by your wife on you or on the children, if any, of the marriage;
(d) wilful neglect on the part of your wife;
(e) desertion of you by your wife for at least three years, where the court is satisfied that it is wilful;
(f) voluntary separation or separation by decree of the court, where it has continued for at least three years;
(g) imprisonment of your wife for life or for a term of not less than five years, regard being had both to the length of the sentence and to the nature of the offence for which it was imposed;
(h) mental illness of your, where at least two doctors, one of whom is qualified or experienced in psychiatry, have certified that they entertain no hope of cure or recovery;
(i) change of religion by your wife, where both parties followed the same faith at the time of the marriage and where according to the laws of that, faith a change of religion dissolves or is a ground for the dissolution of marriage.

Kama ndoa ni ya Kiislamu itabidi upate certificate toka kwa bodi husika kuwa wamejaribu kuwasuluhisha lakini iimeshindikana. Mie nafikiri hakuna haja ya kukimbilia divorce. B'se inaonyesha kabla ya kwenda masomoni mlikuwa mnaishi vizuri tuu. You need to find out yourself what exactly happened. Mambo ya divorce yatawacost sana si nyie tuu bali pia mtoto. Hapa zinahitajika busara na hekima za hali ya juu. Weka emotions pembeni. Kufanya maamuzi magumu kama haya kwa kutumia emotions ni mbaya sana.

Pia kumbuka wakati ukiwa huko masomoni mke wako kama mwanamke mwingine anakuhitaji wewe kama mume zaidi ya pesa zako za mshahara. Ushauri wangu ukirudi likizo, usimkurupushe. Kaa nae chini mzungumze kama mume na mke. Don't rush to divorce. Tofautisha kati ya irretrievable breakdown and a temporary rift. Kama anakutumia messages za kukutukana, wala usimjibu kwa kumtukuna. Wasiliana nae kama mke wako.

Pia mkuu jiangalie wewe mwenyewe unaweza ukawa ni cause ya breakdown. Lugha yako kidogo inanitia wasiwasi. Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa. Sijui kama unam-underrate kwa sababu ya yaliotokea au ndio huwa unamwita hivyo?
 
Laka EMT Nimekupata sana kweli sio hata mimi ninasema tuachane maana najitahidi sana kuwa nayekaribu hasa ukizingatia January mwaka huu mama yetu(i mean mama mkwe) alitangulia mbele ya haki kweli lilikuwa nipigo kubwa kwake na hata kwa familia nzima yetu ukizingatia nilikuwa mbali ndio maana ninajitahidi sana kutoa ushauri na Lugha za kumfariji kila wakati.

Tatizo nipale unapokuwa mumeongea vizuri kabisa bila hata kukwaruzana lakini baada ya muda may be 6hr. unapokea sms inanitukana tena matusi yanguoni akiakaa muda may hata siku 1 au 2 anaomba msamaha.

Ukimwuliza kwa nini uliandika sms anakujibu ni hasira, ukimuuliza hasira zinatoka wapi kama wakati tunaongea hatukugomabana anasema alipata hasira tu. Kwa mfano juzi amenitukana wee kwenye sms jana usiku akaandika sms yakuomba msamaha sasa tutaishi maisha ya aina gani? kuna mambo ambayo nahisi kuwa pengine anakunywa pombe au kama hanywi basi anaweza kuwa na matatizo ya akili kwa sasa au kunajambo alilofanya mbaya linamchanganya kwennye akili hasa niliposema naenda likizo.

"Unasema una mwanamke ambaye umeishi naye muda wa miaka 6 wakati huyo ni mke wako wa ndoa" kwa hili nimekoseha mkuu haikuwa intention yangu
 
jibu maswali yafuatayo↲
Je mna ndoa ya msikit au kansani?↲
Kama mna ndoa ni ngumu sana kumwacha ila unatakiwa uoneshe mahakama your marrage is not reparable &#8626...
hatuna ndoa yakidini tuna ndoa ya kimila na mkuu nitakupataje hata contact hujatoa?
 
Du pole sana.Wanawake tunalilia sana haki zetu.what abt those who misuse them,is there any adhabu 4 them?
<br />
<br />
sure, haki yaendana na wajibu! Judging after hearing one sided story huyo mama hafai hata kumlea mtoto! Ustawi wa jamii na mahakama wataamua!

Women just like men r'nt saints!
 
kaka pole sana nayaliyokupata. Kuachana sio sulihisho kabisa kaka.chakufanya Mwombe M ungu akupe uvumilivu umalize masomo vizuri na utakaporejea mweke mkeo chini muongee kama marafiki atakueleza hela alifanyia nini inawezekana ulimuuliza kwa ukali au kunakitu anachokifanya kwa siri na hizo hela nikumsihii wote muwe wawazi katika maisha yenu mtaishi kwa amani.

Suala la kutukana lazima liwe na sababu kwani kama mmeishi wote siku zote hajakutukana iweje sasa maybe ua the course men.kaeni myasuluishe kwa amani hatua mlofikia ni nzuri kimaisha haitapendeza kila mmoja awe peke yake na vlevle mtamnyima mtoto malezi bora.

Kaka ukumbuke distance maranyingi inavunja mahusiano kilichopo kua mpole kama unampenda mkeo anza kujikomba kwakwe,jishushe kabisa kaka uanze kuirejesha amani ndo mengine yatadhihirika kaka hamna siri chini ya jua.ila kuachana sio suluhisho kabisa unaweza ukapata mwingine ambaye ni nyoka.shika sana ulichonacho kaka.hiyo hela isiwaachanishe mmetoka mbali sana
 
Nashukru sana kwa ushauri wako pia hata mimi sina ubaya naye ila tu kama nilivyoeleza kunitolea matusi hasa pale ninapotoa mchango nini kifanyike na kwa wakati gani nilijaribu kumuuliza kama mshahara hautoshi lakini hakujibu.

Na kama kunakitu anafanya kina adhiri mpaka mtoto. Maana mtoto anatakiwa kusoma lakini yeye hatunzi hata hela ya ada ya mtoto. Nimemshauri aache shughuli zingine zote akipata mshahara atumie kwa chakula, matumizi ya kawaida na kumtunza mtoto wetu hasa katika swala la shule maana yuko kwenye shule za english medium lakini kinachofanyika ni kinyume natulivyokubaliana.
 
Huyo bwana hakufai tena, we nenda likizo kafuate taratibu zote za kimahakama kisha mpe talaka, wanawake hawana jema itakuwa ana mwanamme mwingine, pole sana ndugu yangu.
 
Huyo bwana hakufai tena, we nenda likizo kafuate taratibu zote za kimahakama kisha mpe talaka, wanawake hawana jema itakuwa ana mwanamme mwingine, pole sana ndugu yangu.
na shukuru mkuu kwa mawazo yako maana ndoa siku hizi ni karaha wala sio raha kwa hiyo tuombeane nikifika nitajua lakufanya
 
Bro, kutukanana tu kwenye ndoa ni sababu ndogo sana ya kuweza kuachana, nakushauri vumilia. matusi ni kitu kidogo sana rafiki yangu. Mimi mke wangu hata akinitukana siwezi umiza kichwa sana labda kama kufumaniana hapo ndio kesi nyingine, kwani kwanza inategemeana amenitukana kwa sababu gani, pengine siku hiyo ameamka vibaya na ukizingatia umetuambia mama yake amefariki pengine inampa stress hivyo ukimgusa kwenye kovu analipuka.

Wewe ulipokuwa ulikuwa hutukani sijui ulikulia mazingira gani ambayo hayana challenges ndogondogo kama hizi, kama ulikulia maisha ya kijeshi kama sisi wengine unatukanwa unachapwa unanyanyaswa hadi inafika kipindi unakuwa sugu na kuweza kuishi maisha yeyote yale na kuishi na mtu yeyote yule ukammudu, hasa kutukanwa na mwanamke ni kitu kidogo sana na lazima kuna sababu iliyofanya akutukane.

Sisapoti kukutukana ila nasema hiyo sababu inavumilika kwa wanandoa na si sababu ya kuachana. kwa kifupi, kwa mwanaume aliyekamilika kiutu uzima na mwenye uwezo wa kukaa na familia, yote hayo uliyoyaongea ni ya kuvumilia na kurekebishana tu tena kwa maneno ya mdomo tu. ungeniambia umemfumania hapo nisingekuwa na la kusema kwani hiyo ingekuwa kesi kubwa, ila matusi tu?

kwani kwenye maisha yako hujawahi tukanwa, uyo wife wako ndio wa kwanza kukutukana? amekutukana unataka kumuacha? unafikiri huyo utakayeenda kumuoa hatakutukana? kama sababu unayotaka kuachana na mkeo ndio hii, aisee utaacha na kuoa kuacha na kuoa hata mara 20.

zaidi ya yote, mtu anayetukana sana hivyo sio yeye, ni shetani tu anamtumia, na pengine shetan ameona ndoa yenu ikiendelea mtafanikiwa sana sasa anataka akuachanishe ili mvurugikiwe wewe na mkeo na mtoto wenu.

bofya hapa kwenye link yangu SHERIA KWA KISWAHILI
 
Tafuta nauli umpeleke kwa TB Joshua huwa nasikia kuna mapepo uhenda ana pepo linamtuma akutukane ili ndo ivunjike liendelee kumfaudu peke yake.
 
Naomba kujua ndoa ya kiislam ili ihesabike imevunjika rasmi huwa ktk stage gani ya talaka? Talaka tatu na maana zake kila moja
 
Back
Top Bottom