Sheria za elimu zina upungufu..........

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Sheria za elimu zina upungufu
ban.mtazamo.jpg

Samwel Mwanga

amka2.gif
NI muda mrefu sasa tangu tupata uhuru; serikali imekuwa ikiendelea kutunga sheria na sera mbalimbali za elimu, kama vile ya Elimu kwa Wote (UPE), Elimu ya Watu Wazima na nyinginezo. Jambo ninalotaka kulizungumzia katika mtazamo huu ni kitendo cha Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na taasisi zake kutunga sheria na kanuni ambazo zimekuwa zinatia mashaka kama kweli zinalenga kuleta tija kwa Watanzania wa sasa na kesho.
Kwa mfano katika miaka ya hivi karibuni wizara hiyo ilipitisha sera kwamba masomo ya Fizikia, Kemia na Bailojia yafundishwe kama somo moja.
Pia somo la kilimo na masomo ya biashara, yaani utunzaji wa mahesabu na biashara, yaanze kufundishwa katika vyuo vikuu.
Jambo jingine ambalo limenishangaza ni kitendo cha Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kuzuia vijana waliomaliza kidato cha nne zaidi ya miaka minne au mitano iliyopita kujiunga na mafunzo ya ualimu wa daraja la tatu A, kwa madai kuwa umri wao ni mkubwa, huku serikali kila siku ikilia kuwa shule zina uhaba wa walimu.
Sheria nyingine ni kitendo cha wanafunzi wote wa mafunzo ya ualimu kuanzia ngazi ya cheti na stashahada kutakiwa kukusanya vyeti vyao halisi vya kidato cha nne na sita na kuvipeleka Baraza la Mitihani hadi hapo watakapomaliza kipindi chao cha masomo yaani miaka miwili.
Suala hili limesababisha usumbufu mkubwa kwa wakuu wa vyuo kutakiwa kujaza vyeti hivyo kwenye mabegi na masanduku na kuvipeleka Baraza la Mitihani kwa ajili ya kuvikabidhi kwa maofisa wa baraza hilo.
Jambo hilo ni hatari, kwani katika kusafirisha vyeti hivyo lolote laweza kutokea kama vile kuibiwa huko vilipopelekwa au kupotea kutokana na ajali, mathalani ya gari, hivyo kwa hili nani atawajibika, wakuu wa vyuo waliokabidhiwa na wanafunzi hao au Baraza la Mitihani?
Kama ni suala la kudhibiti, kwanini maofisa wa baraza hilo wasitembelee vyuo hivyo na kuvikagua vyeti hivyo huko huko, ukizingatia kuwa licha ya baraza kutaka vyeti hivyo, bali ni mali ya mwenye cheti kwa huvilipia kabla ya kuvipata au kwanini baraza hilo lisitumie utaratibu kama ule wa Tume ya Vyuo Vikuu ( TCU) wa kuskani na kutuma vyeti vya watahiniwa wote.
Tatizo lingine ni sheria ya ubaguzi wa wazi kwa shule zisizo kuwa za serikali, mfano serikali imeamua kufuta ada za mitihani kwa ngazi zote lakini imetoa maelekezo kwamba ni kwa shule za serikali tu.
Inavyoelekea serikali haina mwelekeo mzuri kwa wawekezaji katika sekta ya elimu, ukizingatia kuwa wawekezaji wa elimu hapa nchi mitaji yao hupatikana kwa mikopo kutoka katika benki mbalimbali na hivyo kutakiwa kurudisha asilimia 18, ukilinganisha na ile ya kilimo ambayo hutozwa asilimia 2 hadi 5.
Sheria zote hizo zimetungwa bila kuwashirikisha wadau mbalimbali wa elimu, hasa wamiliki wa shule na vyuo binafsi ambao wanatoa mchango mkubwa wa kuendeleza sekta hii, kwani hadi sasa kuna vyuo vya ualimu 68 hapa nchini visivyo vya serikali vilivyosajiliwa.
Sasa wakati umefika wa kutunga sheria na sera za elimu kwa kuwashirikisha wadau, kwani tusipokuwa makini, elimu yetu itakuwa ni ya kukariri tu na si ya ukombozi tena; kama maana halisi ya elimu, na hii inathibitishwa na wasomi wetu kuwa hawawezi kushindana katika soko la ajira kwani kwa sasa kunatakiwa mapinduzi katika uongozi wetu wa elimu.
 
Sera na sheria zetu katika nyanja zote ni zima moto..................na huo ndiyo ukweli wetu....hatuna mchawi ila ni ubabaishaji wetu tu.............
 
Back
Top Bottom