Sheria ya Uchaguzi ni mbovu! Kuendelea kuitumia sio Ujinga? Kuwabebesha masikini gharama za Uchaguzi sio Dhambi?

Kuna wakati walipa kodi inafaa mjionee huruma wenyewe sasa! Chagua CCM hawanunuliwi, vinginevyo mtafanya uchaguzi kila mwaka mkijitia ununda...
Nao ni ushauri eti! Mkiitwa shithole mnanuna! Mwambie mwenyekiti wenu kuwa hao anaonunua mayai tu huku kamuacha mama kuku mtagaji akiendelea kutaga mayai mengine! Muulize kama ataweza kuuyanunua yote?
Ni ujinga kujisifu kuwanunua viongozi ukidhani kuwa anawamiliki waliomchagua kumbe walimtuma tu kuwawakilisha! Ccm mnakufa hivi punde hata ninyi ni mashahidi wa kifo chenu! Buriani mkaisalimie KANU!
 
Nao ni ushauri eti! Mkiitwa shithole mnanuna! Mwambie mwenyekiti wenu kuwa hao anaonunua mayai tu huku kamuacha mama kuku mtagaji akiendelea kutaga mayai mengine! Muulize kama ataweza kuuyanunua yote?
Ni ujinga kujisifu kuwanunua viongozi ukidhani kuwa anawamiliki waliomchagua kumbe walimtuma tu kuwawakilisha! Ccm mnakufa hivi punde hata ninyi ni mashahidi wa kifo chenu! Buriani mkaisalimie KANU!
viongozi wenu wanawachezea.
Sasa kafanyeni utani tena mumchague Mwalim halafu tukutane hapa tena mwakani atakapokuwa "amenunuliwa" na nyie mkilia na kodi zenu...
 
Si ndiyo utaahira huo! Na viongozi wenu wanajua nyie majuha ndo maana wanawachezea.
Sasa kafanyeni ujinga tena mumchague Mwalim halafu tukutane hapa tena mwakani atakapokuwa "amenunuliwa" na nyie mkilia na kodi zenu...
Tuna safari ndefu sana ndani ya ccm uongozi wa ccm dah kulima na kupanda mbengu zikiota tunangoa tuna lima tena tuna otesha ujinga sana
 
Si ndiyo utaahira huo! Na viongozi wenu wanajua nyie majuha ndo maana wanawachezea.
Sasa kafanyeni ujinga tena mumchague Mwalim halafu tukutane hapa tena mwakani atakapokuwa "amenunuliwa" na nyie mkilia na kodi zenu...
Kwa maana yako kinachochaguliwa na cdm au cuf ni ujinga mbele ya ccm sio? Na mnatarajia kuwanunua wote na kurudia uchaguzi kila mwezi ikibidi siyo?
Tukisema kuwa huu ni aina ya ulaji na uvujaji wa kodi zetu mtatuelewa au hadi tuingie barabarani?
Nahisi kuna sababu ya kijinga inayotafutwa ili kuhalalisha ile miaka yenu saba! Jilazimisheni kucheka huku moyoni mkiwa na huzuni kuu! Itisheni basi uchaguzi mkuu upya muone kama hamjaambulia zile za nec na policcm! Mnatutia umaskini wa kijinga badala ya hizo fedha za kununua na kurudia chaguzi zingejenga hosptali za kuwatibu kina nani yule wa shilawadu!
 
Ukisema kuwa kiongozi akihama asinyanganywe cheo chake hapo itakuwa vurugu!! Tunategemea kuwa anapohama anaenda kukosoa upande mwingine!! Sasa Wa afrika hatujakomaa !! Bunge litakuwa genge LA wahuni wasiyo heshimiana!!

Lengo la kuweka kudhaminiwa na chama ni kudhibiti ni dhamu ili kuondoa uwezekano Wa wahuni!! Yani vyama viko zaidi ya kumi then unakosa chama cha kujiunga? Basi wewe ni mbinafsi sana!!!

Lengo LA vyama kuwepo ni kupika viongozi wazalendo ili kushika hatamu za uongozi katika nchi!! Sasa mgombea binafsi sijui kaandaliwa na nani na atasimamiwa na nani?

Kuwalazimisha watu wasihame vyama vyao hii nayo ni aina ya ujinga,udikteta uchwara! Chama kinakosa mwelekeo then unataka watu wasihame? Kwa nini?
 
Ukisema kuwa kiongozi akihama asinyanganywe cheo chake hapo itakuwa vurugu!! Tunategemea kuwa anapohama anaenda kukosoa upande mwingine!! Sasa Wa afrika hatujakomaa !! Bunge litakuwa genge LA wahuni wasiyo heshimiana!!

Lengo la kuweka kudhaminiwa na chama ni kudhibiti ni dhamu ili kuondoa uwezekano Wa wahuni!! Yani vyama viko zaidi ya kumi then unakosa chama cha kujiunga? Basi wewe ni mbinafsi sana!!!

Lengo LA vyama kuwepo ni kupika viongozi wazalendo ili kushika hatamu za uongozi katika nchi!! Sasa mgombea binafsi sijui kaandaliwa na nani na atasimamiwa na nani?

Kuwalazimisha watu wasihame vyama vyao hii nayo ni aina ya ujinga,udikteta uchwara! Chama kinakosa mwelekeo then unataka watu wasihame? Kwa nini?
Kweli, bora mtu aliyekuwa wa pili apewe hicho cheo.
 
Demekrasia ina gharama zake lakini pia ina mipaka yake. Haiwezakani wananchi wale wale wawe wanachagua mbunge huyo huyo kila anapohama chama hayo ni matumizi mabaya ya kodi za wananchi. Wewe ukiachia ubunge au udiwani nenda ukafanye shughuli nyingine kwani ulikuwa na uwezo wa kukitumikia hata chama tawala bungeni ukiwa upinzani. Kwa mfano pale bungeni wapo wabunge wa Chadema wanamuunga mkono Rais Magufuli na tumeona michango yao kwenye kazi za kamati mfano Silinda na Ole Milya, na wamefanya hivyo bila kuhamia CCM. Ifike mahali tusikubali huu ujinga wa kumchagua mtu huyo huyo kila " anapojisikia" kuhama hama vyama huu umalaya wa kisiasa utaligharimu taifa na hawa wanasiasa wa aina hii ni Wahujumu wa Uchumi. Nawasilisha!


Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,

Declaration of Interest.
Mimi ni miongoni mwa Watanzania wazalendo wa nchi yangu, ambaye sio mwanachama wa Chama chochote cha siasa, kwa sababu siasa za vyama za Tanzania, tunaziona kama ni ujinga Fulani hivi, hivyo nawaomba sana univumilie, ninapoita siasa za ujinga ujinga, hii ni opinion yangu, everybody has the right to his/her own opinion, hivyo tukitofautiana kwenye hili, tutofautiene kwa hoja, mimi nimeleta hoja zangu kuwa siasa zetu kwenye maeneo Fulani Fulani zikiwezo siasa za uchaguzi ni ujinga ujinga kwa hoja, naomba tubishane kwa hoja.

Watanzania Tufanye Siasa za Ukweli, Tuachane na Siasa za Ujinga Ujinga.
Tufike mahali sisi Watanzania, wazalendo, wenye nia njema na maendeleo ya taifa hili letu masikini, hatuwezi kukaa kimya kwa kuendelea kukumbatia sheria mbovu, bad laws, za uchaguzi, na kuendelea kuwawabesha masikini wa Tanzania, mzigo wa gharama za uchaguzi wa marudio, kwa sababu za kijinga jinga kabisa, zinazotokana na siasa za ujinga ujinga!. Kitendo hiki cha masikini wa kutupwa wa Tanzania, wanaoishi kwenye lindi la umasikini uliotopea wa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, halafu kuja kubebeshwa mzigo wa kugharimia chaguzi za marudio kutokana na sababu za kisiasa za ujinga ujinga, na sababu zenyewe kuwa ni sababu za kijinga kabisa, its not only ni nonsense, but also ni dhambi kwa Mungu, kuwabebesha masikini hawa gharama hizi za ziada kutokana na ujinga tuu wa watu fulani in the name of politics!..

Kwa Nini Sheria Yetu ya Uchaguzi ni Sheria Mbovu, Bad Law.
Kifungu 21 cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kinatoa haki ya kila Mtanzania mwenye sifa, kuwa huru kushiriki katika siasa kuanzia serikali za mtaa hadi serikali kuu, bila ubaguzi wowote.

Uhuru wa kushiriki shughuli za umma Sheria ya 1984 Na.15 ib.6 Sheria ya 1994 Na.34 ya ib.4
21.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya ibara ya 5, ya 39 na ya 67 ya Katiba hii na ya sheria za nchi kuhusiana na masharti ya kuchagua na kuchaguliwa, au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, ama moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao, kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.

Lakini kukatokea kikundi Fulani cha wajinga Fulani, wakaipindua katiba kwa sababu Fulani za kijinga kabisa, wakainyofoa haki hiyo ya raia kwa kulazimisha, ili mtu ugombee nafasi yoyote ya uongozi wa umma, ni lazima udhaminiwe na chama cha siasa!, kiukweli kabisa na ki haki, this is nonsense!.

Rev. Mtikila alikipinga kifungu hiki na Mahakama Kuu ikatamka bayana kipengele hicho ni batili na kinakiuka katiba ya JMT. Wajinga wale, wakaamua kuihalalisha batili ile, kwa kukipenyeza kipengele hicho batili kwenye katiba, ili kuuhalalisha ujinga wao!.

Japo Lengo la Kudhaminiwa na Chama ni Nini, Huu Sii Ujinga Tuu?!.
Katiba katiba ilisema kila Mtanzania ana haki ya kushiriki uongozi, hili sherti la kudhaminiwa na chama lilitoka wapi, na kwa kwa nini watu walazimishwe kuwa wanachama wa vyama ili wadhaminiwe, ndipo waweze kugombea?. Mfano mimi, sina chama kwa sababu naziona siasa za vyama kwa ni ujinga Fulani hivi, ikitokea nina uwezo wa kuwatumikia wananchi wa eneo langu na kuwaletea maendeleo bila kupitia chama chochote, kwa nini nizuiliwe?!. Kiukweli kabisa, huu ni ujinga, it is nonsense, Watanzania tusikubali ujinga huu uendelee hadi 2020!, tupiganie milango ya wagombea binafsi ifunguliwe, 2020, watu wenye nia ya kugombea, tuwaletee wananchi maendeleo, bila kupitia hizi nonsense za vyama tuingie, tushindane kwa hoja na sio kushindana kuhonga, kama hali inavyoendelea sasa!.


Kiongozi Akiishachaguliwa, Anakuwa ni Kiongozi wa Watu, na Sio Kiongozi wa Chama, Kwa Sababu Anachaguliwa na Watu na Sio Chama!.
Ujinga mwingine mkubwa kabisa ni huu, hata kama mgombea amedhaminiwa na chama cha siasa kugombea, akiishapitishwa na Tume ya Uchaguzi kuwa Mgombea, japo anatambulika kama ni mgombea wa chama Fulani, lakini akiishachaguliwa, mwenyekiti wa mtaa, diwani, mbunge au rais, anakuwa sio kiongozi wa chama kilichomdhamini, bali anakuwa ni kiongozi wa wananchi. Mfano baada ya rais Magufuli kuchaguliwa kuwa rais kwa tiketi ya CCM, lakini hakuchaguliwa na wana CCM, amechaguliwa na Watanzania, na sio kiongozi wa CCM bali kiongozi wa Watanzania wote, vivyo hivyo kwa wabunge, madiwani na viongozi wa serikali ya mtaa, kitendo cha kujitoa chama na kupoteza ubunge, udiwani au uongozi wa umma, ni ujinga ambao haupaswi kuvumiliwa. Nini muhimu kati ya umma na chama?. Kuukosesha umma kiongozi waliemchagua kwa sababu za chama, sio tuu sio haki kwa wananchi waliomchagua, bali ni ujinga uliopitiliza, halafu kuja kulipisha wananchi hawa ngarama za uchaguzi wa marudio ni ujinga mwingine na dhambi juu yake ukizingatia kiwango cha umasikini wa nchi yetu.

Nini Kifanyike, A Way Forward.
Kama nilivyowahi kushauri humu, ukosoaji wenye kujenga, huandamana na ushauri wa nini kifanyike kurekebisha kasoro hizi ili kuundoa ujinga huu unaoendelea nchini mwetu kwa sasa.
  1. Iwekwe faini maalum kwa kila kiongozi wa umma, atakayejiuzulu nafasi yake kwa sababu za kijinga jinga, ikiwemo kukatwa mafao yake na ikibidi kufilisiwa ili kugharimia gharama za uchaguzi wa marudio kwa kulitia hasara taifa.
  2. Viongozi wote wanaojiuzulu, wasiruhusiwe tena kugombea nafasi walizojiuzulu, kama sababu za kujiuzulu mimi nimeziita ni za kijinga, tusiwakubalie wajinga hawa kugombea tena, ili wasije kutuletea tena ujinga ule ule na kutugharimisha masikini sisi kugharimia uchaguzi wa marudio.
  3. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kufuta chaguzi zote ndogo, na tuanzishe proportional representation kwa mwenye kura nyingi ndiye mshindi, lakini likitokea lolote, akasita kuwa rais, mbunge au diwani, yule aliyemfuatia katika uchaguzi uliopita ndio anatangazwa mbunge, kama hayupo anachuliwa mtu wa tatu, hadi wa mwisho, kama wote hawapo, ndipo uchaguzi mdogo unafanyika.
  4. Kile kipengele cha kudhaminiwa na chama kiishie kwenye uteuzi tuu, kiongozi akiishachaguliwa, anakuwa kiongozi wa watu, anaweza kuhama chama bila kupoteza uongozi wake kama ilivyo nchini Kenya.
  5. Tubadili sheria yetu ya uchaguzi, kwa kuondoa kipengele cha kudhaminiwa na vyama ili kila Mtanzania mwenye sifa za kugombea uongozi wa nafasi yoyote, aruhusiwe, ila kwenye urais, tuweke vigezo vya ziada, ili asijetokea tajiri mmoja mwenye ukwasi wa kuwanunua watanzania wote, tukajikuta tuna rais wa kununuliwa. Ila kwenye ubunge, udiwani na serikali za mtaa, kila mtu awe free kugombea, hivyo tuwe na wagombea huru, na hili likifanyika hata sisi tusio na vyama tutashiriki, mfano mimi, naweza kabisa kugombea jimbo fulani na kulitwaa kama kuokota embe dodo lililojiangukia, ambapo mbunge wa hapo, nitamsukuma kama nimesukuma mlevi!.
Hitimisho.
Tanzania is too poor spend billions on by elections for foolish and nonsense reasons, nikimaanisha nchi yetu Tanzania ni masikini wa kutupwa, kuhalalisha matumizi ya mabilioni ya fedha kuendesha chaguzi ndogo kwa sababu za kijinga. Ili Taifa letu lipate maendeleo ya kweli, ni lazima sisi Watanzania tukubali kuwa wakweli toka ndani ya nafsi zetu, tusikubali ujinga huu wa kuhama vyama, uendelee kutugharimisha sisi masikini wa kutupwa, tunaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, halafu kuendelea kugharimishwa na wajinga Fulani kwa sababu za ujinga wao!.

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
Rejea.
Rev. Mtikila ashida kesi ya kuruhusu mgombea binafsi mahakama ya ...
Mtikila: Shujaa wa Demokrasia, Mwanamapinduzi halisi na Shujaa ...
Mgombea binafsi Tanzania: Tatizo ni nini? | Page 9 | JamiiForums ...
Swali kwa Wana UKAWA: Is UKAWA for Real or Just A Marriage of ...
Mkuu ccm wanapindisha sheria kwa manufaa yao lengo kuu likiwa ni kutawala milele.
 
Mkuu Paskali nashukuru umeongea lakini ukiwa umechelewa. Watu kama nyie ambao hata hao viongozi wanafahamu kwa sura mnapokaa kimya kwa mambo ya kipumbavu wanaona sawa. Iko siku mtakuja kutoa ushauri watu wakiwa wameuwawa wa kutosha kwa kukaa kimya mpaka. Umetumia lugha nzuri ya ujinga ujinga hii ni lugha inayobeba ukweli bila kuremba. Mimi sasa hivi nasema kushiriki hizi chaguzi za kinyama na kikatili ni upuuzi na ushenzi wa hali ya juu.

Wakati wengine tukihoji wale wapinzani waliokuwa wanahama kwa sababu inayofanana tena wa sehemu na chama fulani mbona mlikaa kimya? Wakapokelewa mbele ya hafla ya kijeshi wakati jeshi na siasa vimetengwa kabisa kikatiba, akina Paskali mlikalia kimya kosa lile la kimaadili kisa anayefanya yale ni mkuu wa nchi. Hivi ni kweli mlikuwa hamuoni kwamba ule ni mchezo wa kipuuzi, umeona wapi watu wanahama pamoja, kwa sababu moja na wakati mwingine barua zikiwa zinafanana maneno na kukosewa majina. Ikasemekana muandishi wa barua ya kujiuzulu ni mmoja ila saini tu ndio za wahusika akina Paskali bado mkawa kimya.

Leo hii tunashindana na watu huku jukwaani kwamba kinachoendelea kwenye hii hamahama ni kutakatisha siasa chafu. Watetezi wa huu upuuzi wanasema tulete ushahidi, yaani wanatuona sisi ni watoto kwamba tunapaswa kuleta EFD receipt ndio iaminike kwamba kuna biashara. Hivi ni nani asiyejua kuna biashara ya ukahaba? Udhibitisho wa biashara hiyo ni receipt ya EFD? Haya basi huo ushenzi wa kuhama chama kwa muwakilishi unafanyika kisha uchaguzi unarudiwa, kwenye chaguzi hizo kuna chama kinaamini kinapendwa kinafanyia wengine ukatili wa kutisha na sheria za uchaguzi zinakiukwa mchana kweupe. Toka lini sheria zeti za uchaguzi zikamtambua Rc na Dc kuratibu upigaji kura? Akina Paskali bado mchezo huu mlikuwa kimya, nalo hili hamkuliona? Kibaya zaidi viongozi wa dini nao wako kimya wanasubiri kuombea nchi amani. Seriously Paskali? Bora umeongea ila ukiwa umechelewa.
Comment iliyojaa mawazo yanayotakiwa kuwa vichwani mwa waTanzania wote (ikibidi) ili kuitoa hapa ilipofikishwa kwa miaka 50+. Ni comment ambayo sitegemei kama kuna mpumbavu ambaye atakua amesimama kiitikadi na kuipinga. Hongera mkuu kwa mawazo yaliyoshiba uzalendo.

Watanzania tuamke, tumechezewa vya kutosha kwa miaka zaidi ya 50, huu ujinga ututoke sasa.
 
Walivo mshabikia nyalandu awakuona swala gharama ee. Wali beep JPM kapiga.
Wewe nadhani kichwa chako hakiko sawa. Hoja kuu hapa ni kujiuzuli na MTU yule yule kurudi kugombea nafasi ile ile katika eneo lile lile na kupigiwa kura na watu wale wale. Nyarandu kagombea wapi!!?? Kama huna hoja, pita kimya kimya ndugu.
 
Poleni na majukumu wadau

Natafakari tu... hivi karibuni kuna mchakato wa kuhamisha walimu wa stashahada na shahada kwenda shule za msingi uhamisho ambao nafikiri utakuwa na usumbufu mwingi saana

Sasa kwa kuwa Mwalimu aliyezoea kufundisha sekondari hii sasa siyo Demotion? je, watakuwa na Mori ya kazi ?

Mbili, Jamii walio wapa heshima kama walimu wa sekondari si itawadharau?

Tatu, Content walio ipata walimu vyuoni ni sawa na ya shule za msingi?

NINI KIFANYIKE,

Mosi,kama ikama ya walimu shule za msingi ni ndogo kuna baadhi ya shule za Msingi zina walimu wa ziada hao ndo wapunguziwe kwenye shule ambazo ikama ni ndogo wao kwa wao siyo kuvuka mipaka.

Pili,kama serikali haina fungu (maana pesa wanazo) la kuajili ajira mpya sasa si wachaji kifungu kingine kama cha uchaguzi mdogo wa makusudi (maana mtu hajafa kajitoa tena kagombea) hizo pesa si waajili walimu wa kada hiyo
kuliko usumbufu huu

mwisho,naomba basi kama watalazimisha wawape walimu hao semina ya ufundishaji wa shule za msingi ili uamisho huo ulete tija kumbuka walimu wa msingi wapo wa Elimu hiyo tena wengi lakini hao ni wa kada hiyoo na wana uzoefu .....NAOMBA TUAJILI WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI NA WPO VIJANA WA ELIMU MAALUMU WALE WA UDOM NA VYUO VINGINE WANAMALIZA SASA WAAJILINI HAOOO NA SIO KWA USUMBUFU HUO...

AHSANTENI
 
Mkuu labda walimu wote wajiunge na chama dola kwanza hasa hao walio hitimu karibuni. Tofauti na hapo hatunahaja ya kuajiri wapinzani wakafundishe Watoto wa wapinzani.
 
Wengi tunalalamika sana kwamba gharama za uchaguzi ni kubwa na pesa hivyo ingeweza tumika kwa kufanyia jambo jingine la kimaendeleo.
kuna mambo mawili ya kufanya ili kuepuka gharama za uchaguzi huo/hizo.
1-kwanza tuvunje tu katiba kidogo kwa kufanya mambo mawili:
A)mbunge atakae hama chama ahame na ubunge wake yani sifa ya ubunge ibaki pale pale ila ruzuku ya chama ibaki ktk chama cha mwanzo alichotoka.
B)hilo likishindikana,basi jimbo limebaki bila mbunge mpaka 2020 kwani hata akiwepo hatoleta maendeleo ya moja kwa moja.
2-chama atakacho hamia ndio kigharamie uchaguzi.
hii itasaidia ktk mambo mawili:
A)vyama vitaogopa kupokea wabunge watakao watia hasara ya pesa.
B)uhakika wa mbunge muhamaji kupata chochote (pesa) utakuwa mdogo kwani tayari pesa yote itakuwa inagharamia uchaguzi.
SULUHISHO NDO HILI.
 
Back
Top Bottom