Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya ndoa ya mwaka 1971

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by shugri, Apr 16, 2010.

 1. shugri

  shugri Member

  #1
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau hivi ni nini madhara ya hii shera hasa ukiuunganisha na haki za binadamu?
  :rolleyes:
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Apr 16, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  KARIBU JAMVINI : Yaani unataka tusome page zote 58??? naomba u-summarise itakapotokea kutoelewana then tutasoma kwa undani!

  Just spot out where do you think human right is violated, kindly, utakuwa umetufundisha wengi kwa muda mfupi na ndipo tutaanza hapo,
   
 3. shugri

  shugri Member

  #3
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  well thanks for the clarification, the thing is am much mor interested in where excatly does this law violates women human rights?
  So far i know about the age for marriage issue on girls, but what i dont undestand is if ur parrents agree and you dont- does it not allow a forced marriage?

  Hope am clear now
   
 4. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Karibu jamvini shugri, kweli kuku mgeni utamtambua kwa kamba mguuni.
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Unaposema "madhara" una maana gani??? Labda kiswahili kina mapungufu wa maneno, ebu tumia kithungu basi ili ueleweke...Kama ni kazi ya utafiti unataka kufanya, ni vyema ukajaribu kuainisha yale unayotaka kubainisha ( si lazima uweke hewani) ila kwa kuonyesha welekeo wa hoja yako ina nia ya kujua nini. Pengine neno "Madhara" laweza likamaanisha zaidi ya unavyofikiria...na jaribu kutofautishwa na neno kama "athari(effects/impacts/consequences", "hasara (disadvantages/cons/loss/failure)", :target:

  Najua kuna jambo wataka kutafiti kwa kujifunza pia kutoka kwa wengine (ni vizuri). Labda kwa kutokukatisha tamaa, ebu jaribu kueleza tu vizuri kile unachohitaji ili ueleweke.

  Aidha, ni vyema pia kwa hizi sheria za muda mrefu ukawaunazisoma kwenye durusu la marekebishoa ya sheria la Mwaka 2002 (JUTA/ R.E 2002) au sheria yenye marekebisho baada ya hapo (Revised Edition) kwani pengine hizi za kwenye mtandao kama Bunge zinakuwa hazijajumuhuisha marekebisho (kama yapo).
   
 6. shugri

  shugri Member

  #6
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 22, 2010
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Thanks M-bongoz,

  Ngoshwe, nakushukuru sana, ukweli ni kwamba mie sina ufahamu sana juu ya hii sheria lakini ukisoma ripoti ambayo tanzania imeandika kwa Commission of the Status of Women- UN, inaainisha kwamba hii ni moja kati ya sheria zinazochochea ukandamizaji na unyanyasaji wa wanawake wa tanzania. My aim is to highlight what exsactly are those areas, within a law? And in what way they could be changed, so that tanzanian women can enjoy human rights equivalent to men.

  Thanks for the input on durusu za marekebisho ya sheria, but can i get them online?

  Je naweza jua ni kwa njia gani hii sheria inapingana na haki nyingine za binadamu? kama vile haki za mtoto?

  Natanguliza shukurani.
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Oky:

  Labda kwa kukushauri ni vyema ukaangalia kwa kina hasa eneo unalotaka kujikita." Kwa ujumla haki za wanawake ni pana sana kwani unapoongelea wanawake hawatofautiani na binadamu wengine hivyo haki zao hazichangamani/ kutofautiana na na haki zote za msingi za binadamu (zile za kuzaliwa nazo "Natural rights) na zile ambazo zipo kwa mujibu wa Katiba na Makubaliano mengine ya kijamii (Civil & Political Rights) ambazo pengine uitwa "codefied rights".

  Lakini pia kwa unapozungumzia haki za Mwanamke inayegemea katika Jamii ipi huyo mwanamke anatokea. Kwa mfano, kwa nchi za Magharibi, kwa mwanamke wa Kiislamu kuvaa "ninja" (hijabu) kwao wanadai ni kupingana ni ukandamizaji wa mwanamke lakini mtizamo kama huo unaweza kutofautiana kwa mazingira ya nchi za kiarabu ambaopo hiyo ni sheria ya dini, mapokeo na pia ni ustaarabu wa kwao.

  Mfano wa pili ni pale ambapo unapojaribu kuleta dhana ya usawa katika mazingira ambayo kanuni ya jumla ya asili haikubaliani kama mazingira, maumbile (mke vs Mume; Mlemavu vs Mzima nk), majukumu ya asili (kuzaa, kunyonyesha,kutafuta maisha kwa jasho nk) uwezo wa jumla wa jamii husika (elimu, uepo, uchumi nk nk), (usawa na haki vinaendana na kipimio, ni lazima uwe na kigezo cha kufananishia, HAKI ZIPI NA DHIDI YA NANI??? MWANAMKE VS MWANAUME ???)....na haya maneno yanayotumia na wanaharakati wengi wa haki za binadamu kama "Haki Sawa kwa Wote", "ukandamizaji na unyanyasaji wa wanawake !!!!"nk unaweza kujiuliza maswali mengi sana yasiyo na majibu ya kina.

  Kwa Kwa jinsi gani unasema ukandamizaji, nani ana makandamiza nani na kwa nini kuwepo kukandamizana?? kwa mfano katika jamii ya watu ambao kiongozi wa jamii hiyo ni mwanamke, ambae hatoi fursa au usawa kwa wanawake wengine, au katika mazingira ya sasa ambayo kwa nchi nyingine imekuwa rukhisa kwa watu kuoana wanavyojisikia ikiwemo ndoa za jinsia moja. Ikiwa mke kwa mke wameona au Mwanamume kwa Mwanaume wameona na wanaitana "husb and Wife, Je, bado hapo patakuwa na "ukandamizaji wa mwanamke ikiwa hakuna fursa sawa kati yao"??..


  Kwa mtazamo binafsi labda kwa kukushauri, kama ni mara yako ya kwanza kufanya utafiti, jaribu kujiuliza maswali mepesi ambayo unaweza kujijibu katika yale mapana unayojaribu kutaka kutafiti .Hii inasaidia kupunguza kutokuogelea kwenye utafiti wako kwenye lengo na upeo unaotaka kufikia/kuthibitisha(Scope & Objective).


  Kwa kuwa tayari katika sheria hii ya Ndoa kuna mandiko (Literatures) kibao ambazo binafsi nayafahamu, labda ni vyema mzee kwa nia ya kuweka sawa kama nia ni kuthibitisha hayo yaliyoripotiwa tu kwenye taarifa ya TZ ya Commission of the Status of Women- UN, naona kama tayari majibu yatakuwepo hata katika hito taarifa jambo ambalo utafiti wako unaweza kuwa kama tayari ulifanyika.

  Kwa msaada labda ungesoma pia hii taarifa ya Tume ya Kurekebisha Sheria http://www.lrct.or.tz/documents/marriage.pdf kupata mwanga zaidi kwani pia inahusu vifungu vilivyopitwa wa wakati na vyenye "ukandamizaji" katika hiyo sheria ya ndoa.

  Kwa kuwa hata hiyo ripoti kwa Commission ya UN hujaitaja ni ya mwaka gani, ni vyema pia ukafanya utafiti wa awali katika mapitio yako (Literature Review) kupitia mamlaka husika kama Lawa Reform Commssions na Tume ya Haki za Binadamu na NGOs zinazohusu haki za wanawake kama TAWLA, WLAC, NOLA etc waweza kukuta tayari hivyo vifungu unavyotaka kuvibainisha vimekwisha pengekezwa kwa marekebisho au vimerekebisha kupitia sheria nyingine zinazohusiana....( Kwa mfano Sheria ya Ukimwi, Sheria ya Ajira na Mahusinao Kazini, Sheria /Mapendekezo ya Sheria ya Watoto, Sheria nk nk )..

  Angali pia hiaya andiko la nyuma na onanisha na hali ya sasa...soma soma soma tena na tena utapata "scope" nzuri!..

  OLDER WOMENÂ’S RIGHTS IN TANZANIA

  http://www.iwraw-ap.org/resources/pdf/41_shadow_reports/Tanzania_SR_HAI.pdf

  General Women Rights:

  http://www.equalitynow.org/english/campaigns/un/unhrc_reports/unhrc_tanzania_en.pdf

  http://lawfam.oxfordjournals.org/cgi/reprint/2/1/1.pdf


  Kwa msaada pia waweza kupitia nyaraka mbalimbali za kisheria ikiwemo za Tz katika hii site http://www.lexadin.nl/wlg/legis/nofr/legis.php


  Otherwise, Juta hazipaitikani katika mtandao, cha kufanya ni kuomba mtu unayemfahamu kama anayo akupe soft copy.

  kila la kheri
   
Loading...