Habari wanajukwaa,
Ipo haja ya kurekebisha sheria ya ndoa kuhusiana na kugawana mali baada ya kutalikiana. Hii itasaidia kutenda haki pia kwa kiasi fulani kupunguza kiwango cha ndoa zinzovujika.
Imekuwa kawaida kwa wanandoa kutoka nje ya ndoa na baada ya kufumaniwa huachana au huendelea kuishi pamoja kwa kuogopa kugawana mali.
Kwa maana hiyo baadhi ya ndoa zinaendelea hata kama ni ndoa mfu kwa kuogopa kugawana mali za wanandoa.
Sasa ili watu waondolewe kwenye jela hii ya kuishi katika ndoa mfu kwa kuogopa kugawana mali basi ni muhimu kurekebisha sheria ya ndoa.
Sheria intakiwa imtake mgoni kumlipa mwanaume au mwanamke aliyetalikiwa kwa kwa uzinzi, badala ya mwanandoa ambaye ni innocent kuingia katika ghrama ambazo hakuzipanga za kuanza kugawana mali ili kumlipa mzinzi.
Hapa naona mwanandoa mzinzi alipwe anachodai katika ndoa na mtu aliyefanya naye uzinzi. Sheria imtake aliyezini naye ndiyo amlipe badala ya kumsababishia deni mwanandoa ambaye hahusiki katika ufuska wala hakupanga kumwaacha mke au mme bali analazimika kwa kuwa mwanandoa mwenzie kaanzisha ndoa kivuli.
Hii itapunguza wanandoa kutoka nje ya ndoa kwa jeuri ya kugawana mali au wizi kupitia kuolewa. Mtu anaolewa au kuoa hali akiendelea kuhusiana na wapenzi wake wa zamani kwa kujua kuwa kuachika kwake ni mtaji. Iwapo wanandoa wanaachana kwasababu nyinginezo wagawane mali hapo naona ni sawa.
Nawasilisha kwa mjadala