- Thread starter
- #21
Inaonekana wewe ni
mwanasheria nimependa pendekezo lakoMi naona iwe hivi;
Iwapo sababu kubwa ya kutalakiana itakuwa ni uzinzi, aliyefanya kosa hilo (aidha mwanamke au mwanaume) hatakuwa na haki yeyote juu ya mali iliyochumwa au kuandikishwa kwa jina la wana ndoa.
Kama ilivyo kwenye kifungu kidogo kilichopita, mwanandoa aliyetenda kosa hilo ataruhisiwa kuchukua mali iliyoandikwa kwa jina lake tu, tena kwa kuongozwa na busara za mtalaka wake.
Nadhani hii ndio itakuwa dawa ya wanandoa wazinzi ambao wanajua hata mkiachana, ana mgao wake.