Sheria ya Mirathi ya Kiislamu kwa mtoto wa nje ya ndoa ibadilishwe

GOLD BOY

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
388
473
Niende Moja Kwa Moja kwenye mada, enyi waislamu kwanini hamtambui uwepo wa mtoto wa nje ya ndoa wakati wa mirathi?

Eti mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kirithi mali za baba ake mzazi hivi sheria gani hizi ambazo zinamkandamiza mtoto?

Mtoto ni mtoto tu haijalishi ni kambo au wandoa.

Wanasema kwamba mtoto wa kambo ni mali ya mama hii inakuaje aisee?

Sheria hizi zibadilishwe ili kulinda haki ya mtoto katika taifa hili kwasababu inamharibu mtoto kisaikolojia anajiona kama amelaaniwa kuja duniani .
 
Sheria nzuri sana hiyo inachangia kuzuia uzinifu, baadhi ya wanawake wanajilengesha mimba za matajiri kwa mbinu zote ili watoto wao warithi mali, mtu na mkewe wamekula dagaa na sukuma wiki ili wajenge, anakuja mpango wa kando na mwanawe kwenye matanga kudai mirathi.
 
Back
Top Bottom