Sheria ya mfanyakazi kulipwa siku 7 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya mfanyakazi kulipwa siku 7

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mr.Mak, Mar 30, 2012.

 1. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Habari zenu ndugu wana sheria.
  Napenda kujua juu ya hili suala. Nimepata kusikia kuwa mtu akipewa termination kazini eti kwa mujibu wa sheria ya kazi hapa nchini mtu huyo aliyepewa termination anatakiwa kulipwa siku 7 tu katika kila mwaka aliofanya kazi na hiyo kampuni.

  1.swali langu ni je hii sheria inafanya kazi hata katika mashirika ya kigeni?

  2. katika mashirika ya kigeni kama mfanyakazi si mtanzania yeye analipwa mwezi mmoja katika kila mwaka aliofanya kazi na kampuni, je hichi kifungu kinachowafanya wao walipwe hivo kipo katika sheria zetu za wizara ya kazi?

  3. kama hazipo wao wanalipwa kwa kufuata sheria zipi na kwanini?

  NITASHUKURU SANA KUPATA HII ELIMU.
   
 2. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #2
  Mar 30, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Tanguliza 'Consultation fee' kwanza..
   
 3. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #3
  Mar 30, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  nitangulize kwa nani na kiasi gani?
   
 4. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #4
  Mar 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Najihisi kukosa msaada hapa. Mie nilitegemea mtanisaidia lakini sijaona. Kama kuna mwenye kujua anieleweshe.
   
 5. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #5
  Mar 31, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Vumilia tu wanasheria wamelala subiri waamke si unajua jana wikiend ilianza +mwisho wa mwezi bank zao zimecheuaaa haaaaaaa kibelaaaaaaaa!
   
 6. J

  Jamuhuri Huru Member

  #6
  Apr 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mr Mak, pole kwa kuchelewa kupata majibu ya swala lako. Lakini naamini kuchelewa huku hakujaadhiri haki yako ya msingi yakikatiba ya kupata habari, ni kwa vile watu wapo busy hawakupitia kwenye ukurasa huu.

  Ni kwamba ulichosikia ni kitu kinaitwa Severance Pay (Kiinua Mgongo) ambacho kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Mahusiano Kazini kipo kwenye Section 42. Kisheria kama mfanyakazi amefukuzwa kwa utaratibu unaotakiwa (fair termination) Mwajiri halazimishwi kumlipa Severance Pay mfanyakazi. Ukiisoma vizuri sheria na marekebisho yake utagundua kuwa mtu ambaye anapaswa kulipwa pesa hiyo ni yule ambaye ameachishwa kazi for operational requirement na wala sio kwa kuretire sababu ya umri, au sababu zingine zozote.
  Hivyo ndivyo sheria inasema, lakini siku zote sheria inatoa minimum requirement, hapa inatakiwa unielewe vizuri. Sheria inatoa minimum requirement kwa maana mtu au mwajiri anatakiwa asishuke chini ya vitu vilivyotolewa kisheria. Mfano kwa swala hili la kiinua mgongo kama Mwajiri ataamua kuwalipa wafanyakazi wake wanapoacha kazi au anapowafukuza kazi, wanapofariki wakiwa kazini au vyovyote vile sheria inaruhusu. Na wapo waajiri wanafanya hivyo, kisheria wapo sawa kabisa ila hawataki kushuka chini ya sheria inavyotaka.

  Swali kwamba sheria inatumika kwa makampuni ya kigeni? YES, sheria hii ya Kazi na Mahusiano Kazini inatumika kwa waajiri wote Tanzania ukitoa Jeshi la Wananchi, Jeshi La Polisi, Jeshi la Magereza na National Services. Angalia Section 2 (1) imeeleza vizuri. Tena kwa uelewa tu ni kwamba hata Watumishi wa Serikali nao Sheria Hii inawahusu moja kwa moja. Nakumbuka kuna kipindi kulikua na discussion ndefu kuhusu hili na nilieleza vizuri sana na ni kwa jinsi gani watu wanazani Watumishi wa Serikali haiwahusu.

  Swala kwamba ktk kampuni za kigeni wafanyakazi ambao sio watanzania wanalipwa mwezi mzima ktk kila mwaka waliofanyakazi. Hii ni kama nilivyoeleza hapo juu, sheria inatoa minimum requirement na hapo inaonekana mwajiri anatoa juu zaidi kuliko sheria inavyotaka that is fine. Ila mwajiri hatakiwi kutoa chini ya sheria inavyotaka. Ila kwa mwajiri mwenye busara hawezi akawa anafanya hivyo kwa wafanyakazi kutoka nje halafu hafanyi hivyo kwa wafanyakazi watanzania. Kwangu hii naona kama ni unyanyasaji inatakiwa mwajiri aliangalie vizuri hilo. Kwani akipata chama cha wafanyakazi wenye kujua sheria vizuri hilo linaweza kumletea dispute.

  Nazani swali lako la tatu limejibiwa pia hapo juu, kwamba sheria inatoa minimum requirement - ukiweza kulipa zaidi ya sheria inavyotaka sio shida ila hutakiwi kulipa chini. Hiyo si tu katika maswala ya pesa ila hata maswala mengine ya kikazi mfano Likizo, zipo kampuni mfano kwenye migodi kwa mwaka wanapumzika zaidi ya siku 28 zilizotolewa na sheria.

  Nazani kwa maelezo yangu utakuwa umenipata kidogo, km kuna chakuongezea wenzangu wataongeza na mimi nikikumbuka nitaongeza ikibidi.
   
 7. Matope

  Matope JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 539
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Maelezo ni mazuri sana hata me nimewahi kupata ufafanuzi hii lakini kuna haja ya hizi sheria za kazi kubadilika!!
   
 8. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #8
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  Nashukuru sana kwa elimu, hakika umenipa mwangaza mkubwa.
   
 9. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #9
  Apr 2, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  sasa kaka kama mwajiri ananiachisha kazi kwa sababu kama zilizo ktk MEMO ifuatayo nini kinapaswa kuwa haki zangu za kimsingi.

  "
  Dear Colleague,
  The global telecommunications sector has seen substantial advances in technology, resulting in the need for telecommunication operators to focus on their core competencies and allow industry specialists to manage the non-core services. The concept of Managed Services (MS), where an industry specialist assumes ownership of non-core business processes and activities, formalises a new way to improve operational efficiencies and enhance the customer value propositions.
  Managed Services is experiencing rapid adoption globally, with more and more African operators partially or fully using Managed Services. This global trend is envisaged to experience widespread adoption, especially in developing markets like Tanzania. It is clear that this trend will be embraced in Tanzania as well, where there is a clear need to ensure that telecommunication services are made affordable to all.
  In order for X Tanzania to remain competitive in the market, it will be critical for us to benefit from these efficiency advantages provided by the MS concept. This will ensure that we maintain our market leadership position in network quality and service performance as well as to provide a competitive value proposition for our customers.
  Accordingly, X Tanzania has made a strategic decision to outsource certain components of the technology operations. This will result in staff members from the technology department being retrenched and employed by international service providers. All affected roles will be guaranteed, with no staff members exposed to the loss of a job as all affected employees will be offered alternative employment of the same package by Y or any other company to be communicated to you soon.
  X Tanzania has identified Y as its Managed Services partners for the Network and IT components. We have already successfully started the collaboration with Y in several Network areas previous years. We have therefore decided to expand the Managed Services scope and outsource additional components of our technology operations.
  Your role in X's journey so far is recognized and greatly appreciated. You have been, and remain a valuable member of our team. Because of this, we have taken great efforts through our lengthy negotiations to ensure you are offered a rich and rewarding position in our extended organization.
  Human Resources will keep you informed of the important steps that will be followed, such as time for the retrenchment exercise and selection of employees, through the usual channels.
  I wish to thank you for your contribution to X's success to date, and I look forward to welcoming you into our transformed organization soon.

  Yours sincerely,

  "
  mwisho wa kunukuu

  Je kama mwajiri aniniachisha kwa sababu kama alizoeleza sheria inanilindaje mimi ili mwajiri asinidhurumu?
   
 10. M

  Mr.Mak JF-Expert Member

  #10
  Apr 3, 2012
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 2,635
  Likes Received: 496
  Trophy Points: 180
  msaada kwa wanasheia please
   
Loading...