Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Kaka umeshaambiwa kuwa Rais atasaini hiyo miswada yote miwili sasa unauliza nini kuhusu kupita kwake? itapita na itakuwa sheria maana haiko kwa lengho la kumkomoa mtu fulani, hii itasaidia kuheshimiana.

Kuheshimiana unakotaka wewe ni kupi? Manake wengine vichwa vyenu ka vimejaa maji vile. Kuwambia kuwa mmezidi kula rushwa na mumafisadi ni kukosa heshima. Mutatufunga sana lakini mwisho wa yote kabuli letu wote si udongo tu. Wako wapi walio wakali sana unawowajuwa wewe? Raha mnazo zinunuwa kwa gharama ya manyanyaso ya wenzenu ni takribani miaka sabini tu. Ikiondoa 25 ya kusotea umande na 15 ya kujikomba kwa wakubwa ili wakubebe kwenyembeleko ummebaki na mingapi? 30. Weka ya kuuguza ukimwi na visukari kibao. Na kansa. Say 10. Umebaki na 20 ya kuponda raha. Na hapo sijaweka provision ya maajali etc etc. Kweli ka raha ka miaka isiyo zidi kumi inaweza ikakufanya uuze utu wako. Kweli.? Ukaacha maisha bora na raha ya milele. Kweli bin Adam haoni zaidi ya urefu wa pua yake. Siku nikiamuka vizuri nitakupeni tafsri ya milele ya watu wanawo ona zaidi ya urefu Wa pua zao.
 
January Makamba na Membe wanapenda vitu kama hv kwa kuhofia watu kuwaumbua matendo yao nyuma ya pazia.
Mumezidi kufuatilia mambo yake mpaka mitihani yake mnamuambia imefutwa kwasababu amekopi anataka asiguswe hata kama kweli kagushi

.
 
Jamani naomba kueleweshwa kuhusu hii sheria aliyosaini JK! Kwa kifupi tunatakiwa tufanyeje na tuepuke kufanya nini sisi wananchi wa kawaida! Manake hata sielewi kwani nasikia hata ukitumiwa picha ya uchi (ambayo sio ya mtu anayefahamika kwa ajili ya kumkashifu) ni kosa pia?

Naomba kueleweshwa kilichomo kwenye sheria hii kwa kifupi sana.

Nawasilisha
 
mie nashangaa wamekimbilia sheria ya mtandao, ile ya madawa ya kulevya ndio imepotezewa?, naona imekomaliwa ya mitandao tu, kwa kweli hapo hajafanya fair, kwani zote zilijadiliwa mjengoni
 
ccm wameona sasa harakati zimeingia mtandaoni maana tunajadili na kueleweshana mambo ya muhimu sana ambayo kwa ccm wao hawapendi tuyajue xaxa wanaona ni vema kutunyima uhuru wa kutumia mitandao. xaxa swali ni kwa nini tuwe na maendeleo ya techolojia?
 
mie nashangaa wamekimbilia sheria ya mtandao, ile ya madawa ya kulevya ndio imepotezewa?, naona imekomaliwa ya mitandao tu, kwa kweli hapo hajafanya fair, kwani zote zilijadiliwa mjengoni

As ooooqi.mo

ccm wameona sasa harakati zimeingia mtandaoni maana tunajadili na kueleweshana mambo ya muhimu sana ambayo kwa ccm wao hawapendi tuyajue xaxa wanaona ni vema kutunyima uhuru wa kutumia mitandao. xaxa swali ni kwa nini tuwe na maendeleo ya techolojia?
 
Kuna bandiko kama sikosei kaiweka Yericko Nyerere kuwa JK kasha saini Sheria hii. Moderator wekeni hiyo taarifa sawa.(dhibitisheni).Ni wajibu wa Members kuwa makini ilikuepusha usumbufu na mikwao-maana Mafisadi kweli wamejipanga ama zao ama zetu-Wadanganyika
 
Last edited by a moderator:
Watu wanauliza kuhusu hiyo sheria kiufupi ni Sheria nzuri tu kama wote mtaweza kuwa polisi.
 
MTANDAO WA RADIO ZA JAMII WATOA TAMKO

Sheria ya Makosa ya Habari Mitandaoni (CYBER CRIME ACT) na Ile ya TAKWIMU zilizopitishwa hivi karibuni bungeni Dodoma na kusainiwa na Rais Jakaya KikweteNi dhahiri kuwa, sheria hii tayari imeisha sainiwa na Mhe Rais.
Katika hotuba ya Waziri wakati akithibitisha Raais amesaini sheria hii, Sababu alizozitoa kupelekea kuunda sheria ni hizi hapa:
“Ndugu Wananchi,
Makosa hayo hujumuisha uhalifu wa Mitandao ambao simu za mkononi, kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu huo.
Mifano ya makosa hayo ni kama ifuatavyo:
1. Kumekuwepo na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,
2. Kumekuwepo na ugaidi kupitia kwenye mitandao,
4. Kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili,
3. Kumekuwepo na uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa kwa makusudi, Kwa mfano kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. [Hii imepelekea kuisababishia Serikali na Sekta binafsi hasara na kusababisha kukosekana kwa huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii].”

Kwangu naona interventions zilizowekwa ndani ya sheria, hazihusiani na sababu hizi hata kidogo, badala yake, zinalenga kudidimiza uhuru wa wananchi kupata taarifa sahihi.
Hata hivyo, badala ya kuzuia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari,vyombo vya habari ni FURSA MUHIMU ya kupata taarifa muhimu ambayo nayo pia zisingefahamika, kama ambavyo imejihirisha katika matukio yaliyofichuliwa na uandishi wa habari makini.
Wewe unaonaje kuhusu sheria hii?
Wako,

Joseph Sekiku
Mwenyekiti
Mtandao wa Radio za Jamii (COMNETA)
 
RAIS KIKWETE AMESAINI SHERIA YA MITANDAO, SOMA HAPA
TAARIFA YA SERIKALI
TAARIFA YA MHE. PROF. MAKAME MBARAWA (MB), WAZIRI WA
MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA KUHUSU SHERIA YA MAKOSA YA
MTANDAO YA MWAKA 2015 KWA WAANDISHI WA HABARI
TAREHE 8 MEI, 2015
Ndugu Wananchi,
Ndugu Waandishi wa Habari,
Kukua kwa kasi kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
(TEHAMA) kumeleta mafanikio mengi katika nyanja mbalimbali za maisha ya
kila siku. Mafanikio haya yanathibitika kwa kuongezeka kwa huduma za
mawasiliano, huduma za kifedha na matumizi ya mitandao ya kijamii. Aidha,
mafanikio hayo yameleta changamoto nyingi katika jamii. Changamoto hizo ni
pamoja na kuibuka kwa makosa mapya ya jinai na pia mbinu mpya za kutenda
makosa ya zamani.
Ndugu Wananchi,
Makosa hayo hujumuisha uhalifu wa Mitandao ambao simu za mkononi,
kompyuta au mifumo ya kompyuta hutumika kama nyenzo za kutenda uhalifu
huo.
Mifano ya makosa hayo ni kama ifuatavyo:
1. Kumekuwepo na wizi wa fedha kwa njia ya mtandao,
2. Kumekuwepo na ugaidi kupitia kwenye mitandao,
4. Kuwepo na mmomonyoko mkubwa wa maadili,
3. Kumekuwepo na uharibifu wa miundombinu muhimu ya Taifa kwa
makusudi, Kwa mfano kukatwa kwa makusudi Mkongo wa Taifa wa
Mawasiliano. [Hii imepelekea kuisababishia Serikali na Sekta binafsi hasara na
kusababisha kukosekana kwa huduma mbalimbali za kiuchumi na za kijamii].
Ndugu Wananchi,
Kama mnavyofahamu kwenye kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania lililopita, Serikali ilipeleka Mswada wa kutunga sheria ya uhalifu wa
mtandao (Cyber Crimes) na Sheria hiyo ilipitishwa na Bunge. Madhumuni ya
kutunga sheria hii kama sheria nyingine zilizotungwa na Bunge hapa nchini ni
kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii hasa kwenye matumizi ya
TEHAMA.
Ndugu Wananchi,
Ndugu Wandishi wa Habari,
Tanzania siyo nchi ya kwanza kutunga sheria kama hii. Kuna nchi mbalimbali
duniani zimetunga sheria kama hii, kwa mfano nchi ya Uingereza (UK
Computer Misuse Act, 1990), India (IT Act, 2000), Malaysia (Computer Crime
Act 2. ) Uganda (Computer Misuse Act, 2010), Korea ya Kusini (Information and
Communications Network Act na Information and Communication
Infrastructure Protection Act), Singapore (The Computer Misuse and
Cybersecurity Act), Maturities (Computer Misuse and Cybercrime Act, 2003),
Afrika ya Kusini, Marekani (Computer Fraud and Abuse Act, 1984) na nyingi
nyinginezo.
Ndugu Wananchi sasa mmepata pahala pa kukimbilia, kwani mukitendewa
uhalifu kupitia mitando sheria hii itawasaidia kupata haki zenu. Ninawashangaa
sana wale wanaopinga kutungwa kwa sheria hii hapa Tanzania. Haikubaliki
hata kidogo kuona Wantanzania wengine wanakumbana na uhalifu kupitia
Kwenye mtandao na wachache kwa faida zao binafsi wanataka Serikali ikae
kimya. Sheria hii haina tofauti na sheria za nchi nyingine nilizozitaja hapo awali.
Sheria hii imetungwa kwa mazingira ya nchi yetu ya Tanzania.
Ndugu Wananchi,
Sheria hii sasa imeshasainiwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kupitia hatua zote za
kuiboresha. Hatua ya MWISHO ilikuwa ni ile ya marekebisho yaliyofanywa na
Bunge ambapo baadhi ya vifungu vilivyolalamikiwa viliboreshwa. Kwa hivyo
wananchi sasa tuipokee sheria hii na kuitumia. Sheria hii ni nzuri na itasaidia
sana kuwalinda wananchi, mitandao na miundombinu yetu muhimu ya kitaifa.
Katika kuitumia sheria hii na kama ilivyo kwa sheria nyingine yoyote,
patakapoonekana kuna mapungufu, marekebisho yatafanyika. Kwa hivyo kama
kuna mtu yeyote mwenye maoni ya kuiboresha sheria hii anaweza kuleta
maoni Serikalini hapa Wizarani. Ninarejea tena: Waheshimiwa Wabunge,
Waheshimiwa Mabalozi, wadau mbalimbali wa Sekta ya Mawasiliano,
waandishi wa habari, wana-bloggers, na wananchi kwa ujumla kama kuna
yeyote mwenye maoni ya kuboresha kifungu chochote cha sheria hii alate
maoni hayo hapa Wizarani.
Serikali kupitia Wizara yangu itapokea maoni au ushauri huo, tutayatafakari na
kuyafanyia kazi kwa kina. Haitosaidia sana kusema huko pembeni, jukwaa zuri
la kuleta maoni ni kupitia Wizara yangu.
Ndugu Wananchi, na
Ndugu Waandishi wa Habari,
Hii haitokuwa sheria ya kwanza kufanyiwa marekebisho kama itaonekana kuna
umuhimu wa kufanya hivyo.
Ahsanteni na Ninawashukuru sana kwa kunisikiliza.
 
Mimi nadhani ingekuwa vyema kwa wabunge tuliowachagua sisi wangejikita kutetea wananchi waweze kupata habari na pia kuelimika kwa maana ukuizingatia mambo mengi sana siku hizi tunayapata kupitia mitandao mbailimbail ya kijamii na kama wameamua kubana huko nashindwa kupata jibu tutalimbilia wapi na habari nyingi tutazipata wapi kwa maana ishakuwa shida.
 
Hii sheria ianze kwa kuwabana watengeneza sinema feki mashuhuri kama vile Kova na Chagonja kabla ya kuanza kutumika kwa raia wa kawaida.

Tiba
unajua hata wewe hapo umeshafanya kosa kulingana na sheria hii? ni movie gani feki chagonja na kova walishatengeneza ambayo wewe unao ushahidi kuwa ni feki. kama ukibanwa ulete ushahidi utaleta ushahidi gani?

au utajitetea kuwa ulikuwa haumaanishi chagonja na kova hawa mapolisi kwasababu majina hayo yanaitwa na watu wengi sio hao mapolisi tu..hahaha.haki ya nani kwa hii sheria, Democracy imeminywa sana.

kwa upande wangu, kuna mazuri na mabaya kwenye hii sheria, mabaya ninayoyaona ni pale nitakaposhindwa kupost picha ya mbunge aliyefuniwa, kupost document ya serikali inayofichua ufisadi nikiwa na maana kama sheria hii ingepita kabla ya escrow na richmond na ufisadi wote ambao baadhi ya watu wameshawajibishwa basi ingekuwa ni kosa kuwafichua kwasababu at the begining of the saga huwa hakuna ushahidi bali baada ya kuwamung'unya humu jf na kurusha ushahidi humuhumu utakuta watu wanakamatwa. hivyo wahalifu hasa wa serikalini watakuwa wanakunywa shampeni kwa hii sheria kwasababu si rahisi kufichuliwa kwa njia ya mtandao. watu wataiba sana serikalini sasa, na kwasababu wizi huwa unakuwa wa akili, ukiwatuhumu tu wakikukamata watakuambia ulete ushahidi, ushahidi wameshauharibu na upo peke yako hakuna wana jf wengine wanaokuletea ushahidi, hapo ndipo utafungwa kabisa.
 
Wanipeleke tu mahakamani ninao ushahidi kwamba Kova na Chagonja ni watengeneza sinema feki. Period.

Tiba
 
Back
Top Bottom