Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015: Kwa mkakati huu wa Serikali, Watumiaji wa Mitandao tutapona?

Ndiko tulikofika? All Assad na Gadaf walifanya hivyo, lakini hali ya kibinadamu ni ngumu na ya hatari sana,

Uchina na Urusi walijaribu havyo lakini utandaridhi vimewashinda,

Sasa kwetu si watafunga kila wanayemhisi tu bila ushahidi?

Hii inadhihirisha tukimpa Makamba uraisi tumetengeneza Gaddafi na Saddam mwingine. Mungu atupishe naye mbali. Kama ujana ukamsaidie babake.
 
nimeisoma cyber crime act bila shaka mitandao ya kijamii maarufu kwa uhuru wa kupashana habari kama vile JF, FB, whatsap, twiter na baadhi ya magazeti hazitasalimika na zitasababisha watu wengi kwenda segerea.
Ninaomba nilogoff mitandao yote, nitakuwa nangalia TBC tu.
Waliosoma cyber crime act vizuri tiririkeni kuelimisha jamii....
 
1. section 7(2)(b) haifai kabisa kwani iweje mpokeaji data bila kujua anapewa adhabu (imekuwa rushwa hii!), 2. section 20 - unsolicited message - kwenye context ipi? marketing, promotion, online invitation to take part in research?, 3. nini faida zaidi za ku-install TTMS https://www.tcra.go.tz/index.php/2-tcra/232-dg-s-desk, 4. sio CCM na serikali wanaweka mazingira ya kufanya surveillance/ spying citizens, 5. hivi 'false information' [section 16] inatofautishwa vipi na 'opinion/ views' ambavyo vinaruhusiwa kikatiba?
 
MZIMU,Moja ya Vipengele vinampa uwezo Police yoyote kuchukua Simu ya Mkeo au yako au ya Mtoto

Shida sio matusi,uongo katika sheria hii,ni mamlaka makubwa waliyopewa 1.POLISI 2.WAZIRI katika followup yake na mahakama kutupwa kando

ila katiba itatulinda amin, kwani hila umalizwa kwa hila!
 
Last edited by a moderator:
The Laws whatever are they they remain null and void until the president sign!
 
Hapa vipi?

10.(1) A person shall not unlawfully deal with or possess: (a) (b) a device, including a computer program, that is designed or adapted for the purpose of committing an offence;

Ina maana kuwa na uTorrent, Tor, Decryption software, Wireless sniffing tools, hata kama ni for educational purposes ni kosa?

Kwasababu hizi zote zinaweza kutumika kufanya illegal access e.t.c
snipa Richard Njunwa Wamavoko Good Guy Dreson4 Kiranga Nyani Ngabu

Hii sehemu inajonyesha ipo ambiguous.

Mtu anaweza kununua "used computer" na ikiwa na programmes kibao ndani yake na asifahamu chochote kwa sababu anakuwa amenunua kwa bei rahisi.

Hii nazungumzia mtu kanunua computer kutoka kwa rafiki au ilikuwa ikitumika ofisini, au chuoni au kwenye biashara.

Pia unaweza kuwa unahodhi computer ambayo imeibiwa na labda iliibiwa kutoka kwa mtengenezaji filamu za ngono, au anae-download mambo ya ngono kutoka kwenye tovuti mbalimbali kwa kutumia torrents, na pia unaweza kuwa najikuta unahodhi computer ambayo imekuwa inatumiwa na gaidi au magaidi na wana programs kibao wanazotumia.

Kwa mtu anaelenga wahalifu ambao hizo keywords zimetumika inakuwa ni vugumu kukwepa charge itakayotoka hapo.

Nafikiri ni ngumu sana kueleweka na msisitizo upo hapo kwenye RED, yaani ukiwa na nia mbaya basi hio sehemu inasaidia kuunda kosa na baadae mashitaka.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kilichonishangaza hapa ni kimoja,mtoto mdogo(sheria ya mawasiliano) hata mwezi hajafikisha tayari ana meno ya kutafuna mifupa.
wakati mtu mzima wa miaka kadhaa(sheria za takukuru & co) mpaka leo hana meno,na hakuna anayejishughulisha kuhakikisha meno yanaota.
Kweli kuelekea uchaguzi tutaona mengi.Tusubilie sheria ya kuzuia mikusanyiko kama huna kadi ya mwaliko kimaandishi.
 
Wale vijana wa chadema wanaopewa viroba kisha wanapewa komputa wamepatiwa dawa sasa
 
Kazi ipo.

Ilza wasisahau kuwa sheria ni "Msemeno" Hivyo aita kula kwetu tu bali ata kwao pia. Wapi Kova na mtekaji wa Dr. Ulimboka? Mwigulu na kauli zake za Ugaidi?

Zaidi naona itakula sana kwa Nape Nnauye maana yule bila kuongea uongo na kusingizia watu hawezi fanya uenezi.

Time will tell

Hshahahahah wapi IGP Mahita na container lililojaa visu vyenye rangi ya cuf?
 
Wametulazimisha tukanunue kompyuta mpya je kwa watanzania tulio wengi tutaweza kumiliki hizo laptop.....ukiangalia kwenye ibara ya 10 (1)Illegal device

Je tutafikia malengo ya E-government? Huku wengi wetu tukishindwa kuafford hzo new brand
 
kwa hali hii ingebidi watanzania tuelimishwe ustaarabu then sheria hii ipite, kuna vipengele vinaashiria wazi ya kuwa ustarabu tulionao watanzania hauna ustahamilivu na kuhimili vishindo vya sheria hii.... ni hayo tu ila uchambuzi unaendelea
 
mi cdhani kma kna tatizo kwani sheria hio imetungwa ila mchakato haujamalizka kwn unatarajiwa kujadiliwa ili kufanya editing panapohitajka........c unajua ya mwanadamu hayakos kasoro najua kubananga hakutakosekana wadau hvo vumilieni,ndo hali hlisi ya nchi kama hzi!
 
hivi haijasainiwa hadi sasa?
ukiona hivi ujue watawala wa ccm wamechoka kufikr, hii ni yetu sasa kufanya maamuz sahihi oct 2015
 
hivi haijasainiwa hadi sasa?
ukiona hivi ujue watawala wa ccm wamechoka kufikr, hii ni fursa yetu sasa kufanya maamuz sahihi oct 2015
 
Back
Top Bottom