Sheria ya kuwalipa viongozi wastaafu 80% ya mshahara wa kiongozi alie madarakani ipitiwe upya

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,705
149,939
Hivi Raisi au Waziri Mkuu aliapishwa leo na baada ya mwezi mmoja,miwili au mitatu akasita kuwa kiongozi kwasababu yoyote ile kama kujiuzulu, n.k, nae alipwe asilimia 80 ya mshahsra wa Raisi au Waziri Mkuu aliepo madarakani?

Mimi ningependekeza kiongozi atumikie nafasi hiyo kwa walau muda usiopungua miaka miwili ndio astahili asilimia 80 ya mshahara wa kiongozi alieko madarakani na atakaetumikia chini ya kipindi hicho alipwe asilimia 50 tu ya mshara wa kiongozi aliepo madarakani.

Nasema hivi kwasababu ipo siku anaweza kutokea Raisi akambadili Waziri Mkuu wake aliekaa madarakani kwa miezi miwili au hata siku mbili tu na bado kila mwezi serikali ikawa inalazimika kumlipa asilimia hiyo ya mshahara kama kiongozi mstaafu.
 
hata kama amekaa miaka 10 alipwe 50% tu mbona watumishi wengine kama walimu pamoja n kuwa n mishahara midogo bado hawalipwi kabisa
 
mkuu umeona hizo nafasi za juu tu ambao kimsingi wanapeta fedha nyingi hata kama 25% inatosha maana wana previledge nyingi. hii pia itazamwe kwa watumishi wa kada nyingine.
 
My suggestion, kama kajiuzulu kwa ubadhilifu hasilipwe kabisa, na Kama akistaafu kawaida apewe pensheni kama wafanyakazi wengine basi, haina haja ya kumlipa mtu hasiefanya kazi
 
My suggestion, kama kajiuzulu kwa ubadhilifu hasilipwe kabisa, na Kama akistaafu kawaida apewe pensheni kama wafanyakazi wengine basi, haina haja ya kumlipa mtu hasiefanya kazi
Wanasiasa wanatunyonya sana!
 
Kwahiyo sumaye anakula 80% ya anachokula majaliwa???..kweli namba wataisoma makapuku!!!
 
Back
Top Bottom