MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
Tanzania ni moja kati ya mataifa yaliyo na sheria ya kunyonga hadi kufa. sheria hii haifai na ni kinyume na haki za binadamu na mapenzi ya Mungu. Ktk historia ya nchi yetu marais wamekuwa hawatii saini watu kufa kama ambavyo mahakama imeridhia. ni Mwl. Nyerere tu alinyonga watu wawili. Aliyemuua mkuu wa mkoa wa Iringa Mh. Kleruu na Mtz mwenye asili ya Asia aliyebuni ajali ikamuua mkewe ili alipwe bima. ikumbukwe ukimnyonga mtu humpi nafac ya kumfundisha na wakati ukimfunga jela maisha anajifunza. pia mkifuatilia nchi zinazotekeleza adhabu hiyo kama Marekani, China, Irani, Saudi Arabia na nyinginezo, uhalifu unaoelekeza adhabu hizo ndo unaongezeka siku hata siku. na tukumbuke Mungu amekataza kuutoa uhai wa mtu kwani ni chukizo kwake. nadhani katiba ya nchi ibadilishwe ili asije kutokea kiongozi akanyonga wahalifu ambao utu wao hautoweki kwa sababu ya makosa yao hata kama ni makubwa namna gani!