Sheria ya kulinda uchumba.

Sheria ya kulinda uchumba.

JUKWE

Member
Joined
Oct 4, 2011
Posts
20
Reaction score
6
Wadau jana nilikuwa kijiweni na jamaa zangu,wakati tunastorika as usual walipo vijana story kama sio siasa basi ni masuala ya mahusiano.

Jamaa mmoja akaja na wazo ambalo ilibidi ni think na kurethink more about it maana nimeona ni relevant sana kipindi hiki

Eti iwepo sheria ya kulinda uchumba ambapo ukimchumbia mtu kwa kipindi cha miezi sita au zaidi iwe official au unofficial then usipomuoa/kuolewa na huyo mchumba,unaweza kumfikisha kortini huyo aliyevunja uchumba kwa kukupotezea muda na resources.

Mimi naona ni valid kwa sababu itapunguza au kuondoa kabisa hiki kilio cha kuachana mitini wakati umri ushasogea na ushapoteza rasilimali nyingi ambazo ungeweza kuinvest kwenye mambo mengine pia ingesaidia kuondoa uchumba feki.

Wadau hii mnaionaje hebu tiririkeni hapo uwanja ni wenu
 
eti nimesikia eti kenya waipitisha eti hii sheria eti
 
Wa TZ kwa kuiga wakenya hatujambo, bora tukae chini na kufanya kulingana na tamaduni zetu, luku vere vere TZ tusije iga kunya kwa tembo tukaja pasuka mnduku. ohoooo...
 
Wadau jana nilikuwa kijiweni na jamaa zangu,wakati tunastorika as usual walipo vijana story kama sio siasa basi ni masuala ya mahusiano.

Jamaa mmoja akaja na wazo ambalo ilibidi ni think na kurethink more about it maana nimeona ni relevant sana kipindi hiki

Eti iwepo sheria ya kulinda uchumba ambapo ukimchumbia mtu kwa kipindi cha miezi sita au zaidi iwe official au unofficial then usipomuoa/kuolewa na huyo mchumba,unaweza kumfikisha kortini huyo aliyevunja uchumba kwa kukupotezea muda na resources.

Mimi naona ni valid kwa sababu itapunguza au kuondoa kabisa hiki kilio cha kuachana mitini wakati umri ushasogea na ushapoteza rasilimali nyingi ambazo ungeweza kuinvest kwenye mambo mengine pia ingesaidia kuondoa uchumba feki.

Wadau hii mnaionaje hebu tiririkeni hapo uwanja ni wenu

Ni kweli, kama valid point vile, lakini najiuliza kipuuzi, Kwa hiyo, hata kama nimebaini tabia zake ni mbovu bado niendelee kuwa naye kwa sababu tu nimechumbia kwa miezi sita au zaidi?
 
Ni kweli, kama valid point vile, lakini najiuliza kipuuzi, Kwa hiyo, hata kama nimebaini tabia zake ni mbovu bado niendelee kuwa naye kwa sababu tu nimechumbia kwa miezi sita au zaidi?

hapo sasa mahakama ndo itaamua nani mwenye kosa ikionekana yeye ndo mwenye kosa lililopelekea wewe ukavunja uchumba then anatakiwa akulipe fidia wewe.
 
kibongo bongo the prison will surely be full......

ya ngoswe tumwachie ngoswe tu
 
Yaani tunalia na taifa hili lenye totally corrupt gvmnt wewe unataka kuongeza mianya ya rushwa? Binafsi nasema no!
 
hiyo safi itaongeza mapato ya nchi. mchumba akulipwa fidia akatwe na VAT
 
Wadau jana nilikuwa kijiweni na jamaa zangu,wakati tunastorika as usual walipo vijana story kama sio siasa basi ni masuala ya mahusiano.

Jamaa mmoja akaja na wazo ambalo ilibidi ni think na kurethink more about it maana nimeona ni relevant sana kipindi hiki

Eti iwepo sheria ya kulinda uchumba ambapo ukimchumbia mtu kwa kipindi cha miezi sita au zaidi iwe official au unofficial then usipomuoa/kuolewa na huyo mchumba,unaweza kumfikisha kortini huyo aliyevunja uchumba kwa kukupotezea muda na resources.

Mimi naona ni valid kwa sababu itapunguza au kuondoa kabisa hiki kilio cha kuachana mitini wakati umri ushasogea na ushapoteza rasilimali nyingi ambazo ungeweza kuinvest kwenye mambo mengine pia ingesaidia kuondoa uchumba feki.

Wadau hii mnaionaje hebu tiririkeni hapo uwanja ni wenu

Hii hoja yako ni nzuri ila kumbuka imekaa kinadharia sana. Sidhani kama inaweza ikawa na uhalisia katika mazingira yetu haya. Ki uhalisia na jinsi ambavyo imekua ikizoeleka na ikifanyika, ni rahisi kuvunja uchumba kuliko kuvunja ndoa.
Uchumba hauna any legal binding compared to marriage.
Mtazamo wangu kwa sasa ni huo. I welcome different contributions
 
Embu someni uzi wa MziziMkavu huu hapa wa leo hadi mwisho halafu mpate picha halisi ya maisha ya Bongo kuhusiana na hili la uchumba

NDUGU WAMKANA NA WAMTIMUA MJANE WA ASKARI WA JWTZ ALIYEUAWA HUKO DARFUL...!!

Hata kabla ya maziko askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), waliouawa Darfur, Sudan hayajafanyika, mchumba wa mmoja wa wapiganaji hao, Amina Juma ameonja chungu nyingine baada ya kutimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi na marehemu mwenza wake.
Amina ambaye inadaiwa kuwa alikuwa akiishi na Fortunatus Msofe aliyekuwa askari katika Kambi ya Msangani, 36KJ Pwani alisema jana: "Kumekuwa na mzozo wa hali ya juu na ndiyo maana tumeshindwa hata kufika Uwanja wa Ndege kuupokea mwili na hata kesho (leo) sidhani kama nitakwenda... kuna mtafaruku mkubwa wa kifamilia."

Baada ya kutimuliwa, Amina ambaye hawakuwahi kupata mtoto na marehemu Msofe, alilazimika kuondoka kwenye nyumba hiyo na kwenda Mlandizi kwa wazazi wake.

"Nimeishi na Msofe kwa miaka mitatu, akiwa kambini mimi niko hapa na wakati mwingine alikuwa analala huku... lakini leo wamenitimua," alisema huku akilia.

Habari zilizothibitishwa na baadhi ya waombolezaji waliokuwa nyumbani kwa marehemu Visiga, Kibaha zinasema baadhi ya wanandugu walimkana Amina siku chache baada ya kutangazwa vifo hivyo.

Ilidaiwa kwamba Amina alitimuliwa katika nyumba hiyo Ijumaa iliyopita, saa saba mchana baada ya ndugu watatu wa marehemu kufika hapo wakitokea Tanga.

Walipofika inadaiwa kuwa walitangaza kusitishwa msiba huo katika nyumba hiyo na kutangaza kutomtambua mke huyo.

Watu hao waliwaeleza waombolezaji kuwa walitumwa na baba mzazi wa marehemu, Willbad Msofe kutoka Kange, Tanga kufika Kibaha kusitisha msiba uliokuwa ukiendelea nyumbani kwa mtoto wake huyo.

Inadaiwa pia kuwa katika msafara huo, alikuwapo mdogo wa marehemu ambaye aliwahi kuishi kwa miaka miwili na Amina hapo Visiga.

Ilidaiwa kuwa walipofika nyumbani hapo walionana na mfiwa, Amina na wazazi wake ambao pamoja na majirani na watu wengine wengi, walikuwa wakimfariji binti yao huyo.

Mmoja wa waombolezaji alisema baada ya salamu wanandugu hao walianza kuulizia mali za marehemu na walikuwa wakimuuliza Amina ambaye aliwaleza kila kitu kilipo na baada ya hapo ndipo walipomweleza kuwa wametumwa na baba wa marehemu kuwa watu hawatakiwi kuomboleza kwenye eneo hilo kwani msiba upo Tanga tu ambako ndiko iliko familia yake.

Alipoulizwa baba wa marehemu, Mzee Msofe alisema: "Mimi ndiye niliyeagiza nyumba ifungwe na ukweli ninamfahamu Amina, lakini simtambui kama mkewe kwa kuwa hawajafunga ndoa... Hata wewe si unayafahamu haya? Uchumba si ndoa na ukifunga ndoa ndipo unatambulika rasmi," alisema.
 
Back
Top Bottom