supersembe
Member
- Aug 23, 2022
- 33
- 51
Majuzi imetokea ajali ya gari kugongana na kichwa cha treni hilo Singida. Lawama zote zikaelekezwa kwa dreva wa treni. Wenzetu Ulaya wametumia teknolojia tena ya bei rahisi kubadili mambo. Makutano yote ya barabara kuu na reli yamepewa vizuizi vya automatic, kufunga beria ya barabara, kupiga kengele na kuwasha taa nyekundu mara treni ikifika mita 100 kabla ya makutano.
Gharama husika kwa kila kizuizi ni usd 2000 sawa na sh. 5m. Tujiulize kwa nini TRC isinunue hiyo mitambo na kuokoa maisha ya watanzania. TRC imebaki na uzembe chini ya sheria iliyopitwa na wakati eti treni haigongi bali inagongwa.
Vipi SGR ikianza kazi, mfumo wa vivuko utatumia beria ya namna gani? Wabunge wetu paza sauti ili sheria zetu zibadilike na teknolojia.
Kila mkitembea Ulaya fanya utafiti, tutaokoa maisha ya watanzania.