Sheria ya faragha kwa ndege zisizokuwa na rubani "DRONES"

isajorsergio

Platinum Member
Apr 22, 2018
4,125
6,250
Tuangazie sheria za mataifa mbalimbali kuhusiana na 'Ndege zisizokuwa na rubani' maarufu DRONES.

Teknolojia na matumzi ya ndege hizi inatazamiwa kupiga hatua mara mbili zaidi kwa miaka mitano ijayo, kutoka Trillioni 51.2 TZS (2020) Hadi Trillioni 102.3 TZS (2021). Matumzi makubwa yakiwa kibiashara, binafsi na kijeshi.


Drone-Pivacy-Laws-2400px.jpg


Kwa haraka tunaweza kuona Mmarekani mmoja kati ya saba amekwisha rusha ndege isiyokuwa na rubani. iFood inatumia drones kusambaza chakula jijini Campiñas, Brasil.

Nchini Ghana drones zinatumika kunyunyizia maeneo ya umma katika kipindi hiki cha COVID-19. Huku Israel ikiwa mzalishaji mkubwa na msabazaji wa drones kuelekea Amerika ya Kusini.

Ukraine drones zinatengenezwa kwa majaribio ya usafirishaji. Na New Zealand likiwa taifa la kwanza kusambaza chakula (Pizza delivery) mjini Whangaparaoa.

Mamlaka mbalimbali nchini Japan zinatoa mafunzo ya drones kukabiliana na matatizo mbalimbali ya kijamii.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-Africa-1.jpg


Afrika ni taifa la Chad ambalo halina vizuizi katika matumizi ya ndege hizi. Huku Ghana urushaji wa drone bila kibali unaweza hukumiwa miaka 30 jela.

Rwanda inatumia drones kusambaza dawa na vifaa tiba, usambazaji uliokuwa unatumia masaa manne sasa ni dakika 20. Malawi likiwa taifa la kwanza Afrika kuwa na kituko cha mafunzo na uwezeshaji chenye lengo la matumizi ya drones kwa masuala ya kibinadamu.

Tanzania matumizi ya ndege hizi yakihitaji vibali na sheria zaidi zikiruhusu ndege hizi kuonekana wakati wa urushaji.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-NorthAmerica-1.jpg


Ensenada, Mexico matumizi ya drone 1 yanawezesha kukumata waharifu 500 na kupunguza kiwango cha uharifu kwa asilimia 10%.

Takribani drones millioni 1.8 zilizosajiliwa Marekani, asilimia 71% ni matumizi binafsi na 29% matumizi ya kibiashara.

Hugo El Salvador inatumia drones kusambaza mahitaji mbalimbali nchini El Salvador. Cuba, Honduras na Belize matumizi ya ndege hizi yamepigwa marufuku.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-EastAsiaOceania-1.jpg


China ni nyumbani kwa kampuni ya DJI mzalishaji na mmiliki wa mgawanyo wa nusu ya drones zote duniani.

Unatakiwa kuwa na miaka 20+ kuweza kuendesha drone yenye uzito wa kilo mbili nchini Indonesia.

Takribani rubani 5,870 ndio waliosajiliwa na mamlaka nchini Australia kuendesha drones.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-Europe-1.jpg

Majaribio ya kwanza ya drone yalifanyika mwaka 1917 nchini Uingereza.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-MiddleEastCentralAsia-1.jpg


Iran ni marufuku kutumia drones, lakini ndio taifa la kwanza kutumia ndege hizi kijeshi. Kyrgyzstan, Uzbekistan, Syria, Iraq na Yemen drones ni marufuku.

Umoja wa Falme za Kiarabu umekuwa ukifanya majaribio ya ndege taxi.


Drone-Privacy-Laws-Full-width-SouthAmerica-1.jpg


Chile drones zinatumika kukagua maeneo ya maji na utoaji huduma ya dharura (Ugawaji life jackets) kwa watu walio maeneo hatarishi.

WaAmazonia wanatumia drones kufutilia uharifu dhidi ya mazingira na ukataji miti.

bit.ly/DronePrivacyLaws (Surfshark)
 
Nimeweka maelezo na picha kabisa! Tanzania ni Visual Line of Sight Required.
kwaiyo mfano mimi ni hobbiest natengeneza au kununua rc plane na drone natakiwa kufata vigezo gani ili kurusha?
au ndio nitengeneze uko shinyanga kwa gharama ya 50k alafu nikatafute leseni na kibali kwa 200k?
na je nikienda open field nikarusha device yangu ndani ya iyo visual line of sight siwezi fatwa kuambiwa navunja sheria?
naomba msaada wa majibu juu ya haya maana ilo shirika hata email zangu hawajibu
 
kwaiyo mfano mimi ni hobbiest natengeneza au kununua rc plane na drone natakiwa kufata vigezo gani ili kurusha?
au ndio nitengeneze uko shinyanga kwa gharama ya 50k alafu nikatafute leseni na kibali kwa 200k?
na je nikienda open field nikarusha device yangu ndani ya iyo visual line of sight siwezi fatwa kuambiwa navunja sheria?
naomba msaada wa majibu juu ya haya maana ilo shirika hata email zangu hawajibu

Hello 👋 Srebrina

Kwa sheria za Tanzania zinahitajika kila mmiliki wa drone/s afanyie usajili ndege yake. Katika usajili kuna gharama kadhaa hulipwa na hapo unakuwa huru huku ukitambulika kama mmiliki na mrushaji halali.

Ikiwa wewe ni mtengenezaji au muendelezaji wa drones nadhani utakuwa unahitaji vibali zaidi kutoka mamlaka za serikali, wizara ya mambo ya ndani na jeshi pia.

Urushaji wa Visual Line of Sight ulikuwapo before kabla ya marekebisho ya sheria mwaka 2020. Ukiwa unahitaji uhalali na pasi ya usumbufu fika makao makuu ya Mkoa/wilaya utapewa vibali na masharti yake.
-
Out of topic! Your name sounds more Serb - Slavic - Russian - Albanian 😊
 
Back
Top Bottom