Sheria ya Ardhi ina makosa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria ya Ardhi ina makosa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Shark, Sep 5, 2011.

 1. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #1
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Ndugu wapendwa,
  Kuna suala moja naona kama lina walakini, na ningepata wasaa ningemshauri Waziri wa Ardhi aliangalie kwa makini.
  Mtu umejipinda ukapata pesa kidogo ukaingia maeneo ya Mbezi, Bonyokwa, Goba n.k kutafuta kipande cha Ardhi ili ujenge maana kodi haziaminiki mjini.
  Unamalizana mwenye ardhi na kupitia michakato yote pale kijijini ili isiwe tabu baadae.
  Kwakua hutaki shida unakwenda ardhi ili kukipima upewe hati kabisa,
  Cha ajabu watu wa arhi wanakuja kukuambia kua kwa mujibu wa "Master Plan" ya mji, hapo ulipopata ni eneo la wazi/soko/barabara,
  Swali langu ni kua, kwanini basi hizo master plan zisiwekwe huko kijijini ili kila anaenunua ajue hukohuko kua kaliwa?
  Serikali ya kijiji inakupitisha kununua kwamba ni mahali halali,
  Serikali kuu inakuja kukuambia kua sio, hapa imekaaje?
  Kuna masuala ya kuchukua location ya eneo (GPS) ili ukapate uweli kuhusu hilo eneo wizarani, but ni wangapi wanajua kuhusu hii kitu?
  Ni kweli unaweza kuomba amendment ya hiyo plan ikafanikiwa?
   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  A very big concern. Sheria ya ardhi ina matatizo makubwa. Haikufanyiwa utafiti wa kutosha kabla ya kuipitisha. Waziri Tibaijuka ayaangalie haya mapungufu ni ya msingi sana tena sana. Lakini wana muda huo?
   
 3. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #3
  Sep 5, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,971
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kweli kabisa mkuu, sheria ya ardhi ina matatizo makubwa sana. Mipango miji hwawezi kuweka master plan wazi kwa sababu wanataka usubiri viwanja wapime wao na wakuuzie kwa rushwa na tena kwa gharama kubwa. Ukinunua kiwanja kwa wanakijiji maanake wao watakosa pesa.
  Pia sheria ya aridhi inachangia umaskini. Watu wenye mashamba huko nje ya mji wananyang'anywa ardhi yao wanayoitegemea kwa kilimo bila kulipwa fidia, badala yake vinapimwa viwanja ambavyo vinauzwa na halmashauri badala ya wenye mashamba. Mtu anaponyang'anywa eneo ambalo amekuwa akilitegemea kujipatia mapato yake bila fidia maana yake ni kwamba huyo mtu tumemsukuma aende kuwa ombaomba wa milele. Ni unyama wa hali ya juu.
  Ni afadhali mipango miji wachore ramani, viwanja auze mwenye ardhi maana Hilo ndo tegemeo lake, upimaji ufanywe na makampuni binafsi.
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  Umeleta wazo la haki. Kama kuna mipango miji, basi hatukatai, lakini viwanja viwe mali ya mwenye ardhi, auze yeye mwenye ardhi. Ni uonevu na unyama kumtoa mtu kwenye ardhi ambayo ameimiliki vizazi na vizazi, leo unamtoa kwa fidia kiduchu/kidogo. Halmashauri wanauza viwanja kwa rushwa kubwa sana. History will tell, ni wizi na unyama wa serikali yetu kwa wananchi wake.
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ni ujinga na uzembe wa serikali kusema ukweli. Kwa kiasi kikubwa serikali ndio inahamasisha makazi holela na migogoro ya ardhi. Ilitakiwa kila mwaka wa fedha serikali iwe inapima viwanja visivyopungua 20,000 na kujenga vilevile majumba mengi ya kupangisha kutokana na sekta yenyewe ya makazi na upangaji kuwa legelege na unregulated. Sasa kunapokosekana mipango ndio kunapokuja mambo kama haya. Sasa utashangaa siku hizi hata huko vijijini na kwene miji midogo kuna makazi holela wakati Tz haina matatizo ya ardhi.
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Sep 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Kwani kuna ugumu gani kwa mfano ku-print master plan ya Goba ukawapelekea hukohuko Goba wakae nayo wao ili akija mtu kununua ardhi kwa mwanakijiji wa-verify hukohuko kijijini kuliko kusubiri mpaka Wizarani?
  Hawaoni kama itawarahisishia kazi,
  pili kupunguza utapeli,
  Tatu kuondoa kero kwa wananchi,
  Nne kupunguza ujenzi holela?
  Hivi kama kijiji kimeshanipitisha kununua hiyo ardhi wakati master plan inasema ni barabara, naweza kuwashitaki serikali ya kijiji na mamihuri yao waliyoyagonga?
   
 7. T

  Taso JF-Expert Member

  #7
  Sep 5, 2011
  Joined: Jun 12, 2010
  Messages: 1,653
  Likes Received: 458
  Trophy Points: 180
  Shark, sheria ina tatizo gani hapo specifically? Umesema "unamalizana na mwenye ardhi" halafu unaenda Ardhi kutafuta hati unakuta "umeliwa." Sasa hapo ndugu yangu, tatizo ni sheria au ni wewe uliyefanya mambo kinyumenyume? Hata ukinunua pikipiki huwezi "kumalizana" na mwenye pikipiki halafu useme "kwa kuwa hutaki shinda" unaenda TRA kuangalia usajili wa pikipiki kama aliyekuuzia ndie alikuwa mmiliki halali. Too late! Huwezi kufanya hivyo. Sembuse kiwanja?

  Kaangalie allocation ya matumizi ya kiwanja kwenye master plan kabla hujanunua, na kabla ya kulaumu sheria.

   
 8. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #8
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duu bwana Taso nashukuru mungu amekuleta hapa. Pale Morogoro vijijini kuna shamba nataka kulinunua ni la ukubwa wa ekari mia tatu hivi sasa kulingana na jinsi ulivyo kritisaiz kuhusu jinsi watu wanavyo ishambulia sheria kabla ya kufanya analysis ya hali halisi kuhusu sheria na pia kufanya tafiti ya ardhi kabla ya manunuzi, embu ngoja nikimbie kwanza lakini sjui niende wapi.

  Je naweza nikaingia ofisi ya ardhi ya mkoa?? maana serikali ya kijiji tayari wameshatoa baraka kuwa ardhi ni ya anayeuza na haina shida yoyote kabisa.

  Please kama humo umo pls endelea kunijuza.
   
 9. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #9
  Sep 5, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tatizo si sheria, ni mnunuzi wa ardhi anapoenda kwenye watu wasiohusika ambao anawaita "wenye ardhi!" Kwa nini asingewaomba hao "wenye ardhi" wampimie hiyo ardhi na kukimbilia ofisi za Mipango Miji?
   
 10. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #10
  Sep 5, 2011
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  masaburi yao yooote yanafikiria gamba la 2015
   
 11. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #11
  Sep 6, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Kuna tofauti kati ya kuthibitisha uhalali na ku-registre ardhi iwe officialy yako ambayo ndio nayoizungumzia,
  Pili sizungumzii sheria kwa vigezo vya vifungu vyake, bali utaratibu unaotumika ambapo sheria ndio inayosimamia.
  Kama ni kuthibitisha Kijiji kishanithibitishia kua ni mali ya muuzaji.
  Na kupima ili upate hati inaweza kua ni option tu, kwani asilimia kubwa tunaishi kwenye skwata na bado maisha yanaenda,
  Elewa point yangu, kuna mgongano hapa kati ya serikali ya kijiji na serikali kuu!!
   
 12. e

  emrema JF-Expert Member

  #12
  Sep 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 270
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tumia wataalamu wa ardhi ilikuepuka matatizo baada ya kununua kiwanja.Wengi wanaliwa sababu ya kutoelewa, na ubahili. matokeo yake ni doube allocation na kujenga kwenye matumizi ya public. Pale Mbezi Makonde kuna watu wameuziwa viwanja kwenye eneo la kiwanda linalomilikiwa kwa term ya 99 years. Wamejenga magorofa mazuri tu. Wiki 2 zilizopita mmiliki halali anakuja kujenga ukuta, wao oooh ulikuwa wapi muda wote!? Tutenganishe siassa na utaalamu wa ardhi. Sheria zipo sawa tu ila tunazidharau.
   
 13. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #13
  Sep 7, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,106
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  Hapo ndipo panapotokea tatizo, ushanunua halafu ndio baadae unakwenda kwa hao wataalamu wa ardhi ambao wanakuambia kua umeuziwa barabara,
  Nafikiri ungesema "kabla" ya kununua
   
 14. l

  laila Member

  #14
  Sep 8, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  namimi naongeza kwamba ni sahihi kuwasiliana na wataalam kabla ya kufanya biashara yoyote maana cku hizi usanii ni mwingi kila mtu anatafuta pesa kwa njia anayoifahamu
   
Loading...