Masaki
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,463
- 753
Hapa panaweza pasiwe mahala muafaka kwa kujadilia suala hili, lakini katika sehemu zote nilizoangalia, angalau hapa panaelekea kidogo...Nashauri wamiliki wa bodi hii waongeze kipengele cha "Jamii/Ustawi wa Jamii".
Katika nchi yetu siku hizi tunaona wananchi wanajichukulia sheria mkononi pindi wanapowakamata wahalifu badala ya kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Hii inatokana na kwamba, vyombo vya sheria vimekuwa havifanyi kazi yake sawa sawa na hivyo wahalifu kuachiliwa kirahisi, ama kwa kujuana, au kwa kutoa rushwa.
Matokeo yake wananchi wameamua kuwapiga na pengine kuwaua kabisa, tena kwa kuwachoma moto wahalifu wote wanaowatia mikononi!
Kama tatizo ni utendaji mbovu kwenye vyombo vya sheria, nini kifanyike kuboresha utendaji huo? Na je baada ya kuwepo kwa mmomonyoko wa uaminifu wa wananchi kwa vyombo vya sheria, pindi vyombo hivyo vitakaporekebishwa na kuanza kufanya kazi sawa sawa, tunadhani wananchi wataacha tabia ya kujichukulia sheria mikononi ambayo imeshajengeka miongoni mwao?