Sheria inasemaje kuhusu mtu aliyejeruhi au kuua akijitetea dhidi ya adui

LA7

JF-Expert Member
Aug 26, 2019
457
1,728
Naombeni kujua wakuu maana kuna mtu anituhumu nimemtaka mke wake sasa amenitishia kuwa atanifanyia kitu kibaya.

Sasa hapa nilipo natembia na kaslaha kadogo kwa ajili ya kujitetea kwa lolote lile.

Mpaka tumefikia hapo ilikuwa hivi?

Mke wake alinipigia simu kuwa yupo ofisini kwangu nikamwambia anisubirie kidogo, sasa wakati nafika ofisini nikamwambia mbona (umenikimbia) hiyo sms ndo mume wake aliyoiona na kunihisi vibaya kwa mke wake, ni jirani tu wanaishi na ilipo ofisi yangu.
 
Kama mwanaume huna hajabya kutembea na silaha waite wote kwanza uwaweke sawa pili mwamvie kabisa vitisho sio vizuri ukiona hakuelewi karipoti kwenye mamlaka. Sheria ya hapa tz ni pesa tu unaweza ukawa umeonewa na bado hiyo sheria ikakukandamiza. Maongezi nadhani ni njia nzuri zaidi kama kweli hukuleta michezo ya kumtaka huyo mke wake.
 
Karipoti kwa viongozi wa eneo lenu kuwa umetishiwa, unaweza ukasaidika tofauti na kuzunguka na silaha. Mkidhuriana huko itakuwa ngumu kwako kusikilizwa kwa utetezi wa kutishiwa maisha
 
sasa hapa nilipo natembia na kaslaha kadogo kwa ajili ya kujitetea kwa lolote lile,
Malice aforethought, ukienda kujieleza hivi Mahakamani wewe tayari ushajitia hatiani

Kwa hio hatua pekee uliyoiona ni hio ya kutembea na silaha tayari kwa kufanya mashambulizi?

Wewe ulitakiwa ukatoe taarifa kwenye vyombo vya dola huyo anaekutishia aitwe apewe maelekezo kikikutokea chochote ukajihami hapo utakua na pa kuanzia Ila unapofanya hivyo kwamba unabeba silaha tu na hujareport kwenye ngazi husika unajiweka mashakani ikitokea umefanya mauaji hapo kifungo cha Maisha kinakuhusu hata km yeye ndio aliekuanza

Nb: Mimi sio mtu wa masuala ya sheria napenda tu vipindi vya redio na TV kuhusu masuala hayo hususani kipindi cha Ijue Sheria
 
Back
Top Bottom