Sheria inasemaje kuhusu mtoto wa nje ya ndoa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheria inasemaje kuhusu mtoto wa nje ya ndoa?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Leornado, Jul 5, 2011.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Nina mshikaji wangu huu mwaka wa tano anateseka kudai mtoto wake bila mafanikio. Stori ilikuwa hivi:

  Yeye kaoana na mmarekani walikutana alipoenda huko kimasomo, bahati mbaya mkewe aligundulika ana matatizo ya uzazi hivyo hataweza kupata nae mtoto. Jamaa anapenda sana kuwa na watoto au walau mmoja. Wakaelewana na mkewe akaja bongo akamzalisha mwanamke mmoja ili baadae amchukue mwanae wakaishi nae marekani. Hii ishu mama mzazi wa mtoto aliijua kwamba anamsaidia jamaa kuzaa then mkataba unaishia hapo, lakini cha kushangaza baada ya kuzaa kambadilikia jamaa na hataki kumpa mwanae. Huu ni mwaka wa tano wanahangaika mama anawapiga tarehe. Amewageuza kitega uchumi kwa kupitia mgongo wa mtoto kwani matumizi anayodai ni makubwa sana kiasi kwamba jamaa anaelemewa kutuma pesa za matumizi kila mwezi wakati angeweza kuishi na mwanae marekani freely. Yeye na mkewe wamechanganyikiwa hawajui wafanyeje.

  Kuna sheria yoyote itakayomsaidia mshkaji wangu na mkewe wa ndoa kumpata mtoto huyu. Ni kavulana kazuri na kamefanana sana na baba yake.

  Thanx wakuu.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Suala hili lina utata mwingi sana. Kwani unavyobainisha ni kuwa walikubaliana wapate mtoto kisha mwanamme amchukue huyo mtoto. Labda ili niweze kukusaidia ningependa kuku uliza masuala yafuatayo.
  1. Je waliandikiana hayo makubaliano?
  2. Tunajua Mama aliposhika ujauzito alihudhurua clinic. Kule clinic kuna Card ya Clinic. Je kwenye ile kadi aliandika jina la baba la nani?
  3. Je kama amepata cheti cha kuzaliwa, Je kimeandikwa jina la baba ni nani?
  4. Je mtoto ana umri gani hivi sasa?

  kama mtoto atakuwa na umri chini ya miaka sabaa basi Taratibu za Kisheria zinaainisha wazi kuwa atakuwa chini ya malezi ya mama na baba itampasa atoe matunzo. baada ya hapo ndio mnaweza kujadili zaidi.

  Naomba ufafanuzi wako tukusaidie.

  Nasriyah Saleh Al Nahdi. (Mke wa Barubaru)
  Mapumzikoni Unguja
   
 4. L

  Leornado JF-Expert Member

  #4
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0


  Kabla ya mimba walielewana bila maandishi, ila alipokuwa mjamzito kuna documents alizisaini. Alipojifungua mtu na mkewe wakaja kumuona mtoto na kumpa majina waliyoyataka wao. Baada ya miezi sita baba wa mtoto na mkewe wa ndoa wakarudi tayari kumchukua mtoto 4ever hapo ndipo ugomvi ulipoanzia kwani yule mama alidai bado hayuko tayari kumtoa mwanae. Document alizosaini amezikana kwa madai kuwa hakuzielewa. Huu ni mwaka wa tano anapiga dana dana na mtoto umri wa shule unakaribia.

  Cheti cha kuzaliwa kimeandikwa jina moja la huyu baba, wakati kule marekani mtoto ana majina mengine tofauti kabisa na huyu mama aliyombatiza.
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hapa ningeomba ufafanuzi kidigo tena.

  Je Docs hizo ziliandikwa nini?
  Je zilisainiwa na nani ? je kulikuwa na mashahidi? Je zilipitia kwa mwana sheria kuthibitisha hilo? au ziliandikwa kisheria?
  Unaposema Cheti cha kuzaliwa kimeandikwa jina moja una maana gani? Kimeandikwa eg Joseph na sio kama ilivyoada Joseph Abdi Mkude?
  Na vipi card la clinic limeandikwa majina gani?

  Naomba ufafanuzi hapo.

  Nasriyah. Saleh Al Nahdi
   
 6. L

  Leornado JF-Expert Member

  #6
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Document alizisaini mbele ya baba wa mtoto hawakuona haja ya kufanya mambo kisheria kwani mama wa mtoto mwanzoni alikuwa na ushirikiano sana. Alikuja kuwabadilikia ghafla.

  Docments zote zilikuwa from states, kwamba she is allowing parental guidance to the couple na yeye atabaki kama mama mzazi lakini hana maamuzi yoyote kuhusu makuzi ya mtoto. Kwa nchi waliopo unahitaji hii "full parental guidanceship document" la sivyo kuna maamuzi huyu mama wa kambo asingeruhusiwa kuyafanya juu ya mtoto. Pia huyu mama mzazi kwa kusaini doc ile ina maanisha hana mamlaka tena juu ya mtoto bali hawa wanandoa.

  Cheti cha kuzaliwa kimeandakiwa jina la kwanza tu la baba.


  Ishu ni je watampata vipi huyu mtoto? na wanaanzaje?
   
 7. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #7
  Jul 8, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna makosa mengi sana kisheria ambayo wameyafanya kiasi cha kuleta utata mkubwa sana kisheria.
  1. Siku zote kwenye card la clinic linaandikwa jina kamili la baba na kazi yake ----Hawakufanya hivyo
  2. Cheti cha kuzaliwa kinaandikwa jina kamili la baba na kazi yake ----- hawakufanya hivyo
  3. Walitakiwa waelewe sheria za Marekani ni tofauti na sheria za tanzania. So hizo form ni batili tanzania kwa mujibu wa sheria za tanzania


  Kinachoweza kufanyika ni kumuomba huyo mama nje ya sheria ili mkubaline na kumpa fungu lake ikiwa na kumuahidi mtoto atakuja kumtembelea na hata mama kwenda na kumuona mwanae. Zitumike busara katika kumuomba mama ampe mtoto kwa baba na wala wasikimbilie kisheria kwani mtoto hajafikisha miaka sabaa. na hata akifikisha kuna kosa Baba kalifanya cha kuandika jina moja.

  Nasisitiza Busara itumike katika kumuomba huyo mtoto kwa baba yake
   
 8. L

  Leornado JF-Expert Member

  #8
  Jul 8, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ina maana kwa sheria za bongo hawataweza kumpata mtoto? Mama katoa sharti ambalo kulitimiza ni vigumu sana. Thanx sana kwa ushauri wako mzuri.
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Jul 10, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana.

  Kama watatumia busara zaidi na hikma kubwa kwa mama yake kumuomba basi wanaweza kufaha
   
 10. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #10
  Jul 10, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Hapana. Documents za Marekani whether legal or not sidhani kama zitahalalisha hiyo process. Tanzania ina procedure zake kwa issue kama hiyo. Kinachotakiwa ni kufuata sheria na kanuni za Tanzania katika ku handle hiyo issue. Hata akifanikiwa kumpeleka huyo mtoto Marekani, vyombo vya huko vitarely kwenye legal documents za Tanzania kama mtoto ni wake, nk. Kama Barubaru alivyosema atumie busara zaidi b'se kwa sasa sheria inaonekana inaenda against him. Achana na sheria nyingine zinazoweza ku-aaply kwenye hili suala, mwanamke anaweza kukubali kuwa alisaini hizo document lakini under under influence.

  Issue nyingine inaonekana interests za mtoto hapa hazijachukuliwa kwa uzito mkubwa. mara nyingi yanapokuja masuala kama haya tunasahau kabisa interests za watoto ambao ndio kiini cha suala husika. The fact kuwa yeye ni baba mzazi haina maana kuwa he can do whatever he wants including moving the child to America. The child's interest are paramount kwenye hili suala. Inawezekana anataka kumpeleka Marekani kwa nia nzuri tuu, lakini vipi mtoto anasemaje juu ya hili? Amekuwa consulted? Yupo tayari kuishi na mama wa kambo? Implications za mahusiano kati ya mama wa kambo na mtoto amezifikiria kwa undani? Akihamia Marekani, mahusiano yake na mama mzazi yakuwaje?

  Awe makini sana b'se hayo makubaliano yanaweza kutafsiriwa as if they intended to traffic the child to America. Ushauri: jaribu kuwasiliana na watu wa ustawi wa Jamii wa Tanzania (wilayani kwako) watakupa mwanga zaidi juu ya hili suala. Kama utamtafuta mwanasheria, then tafuta yule ambaye amespecialise kwenye haya mambo. Otherwise, ataliwa pesa tuu.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jul 11, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sawia kabisa. Lakin mimi nazidi kumsisitiza afanye mambo yake nje ya sheria na afuate mila. Unajuwa zamani kulikua na kile kitu cha Mtu kumkomboa mtoto wake kama alizaa nje ya ndoa. sasa hiyo ni njia ya kwanza.

  Njia nyingine Kwa mujibu wa Sheria mtoto atakaa kwa mama na baba atalazimika kumtunza kwa kupeleka pesa za matumizi mpaka miaka sabaa. Na ikifikia hapa Mzazi wa kiume anaweza kumwomba huyo mtoto kwa nia ya kumlea na kumwendeleza kimasomo. Hili sasa linaweza kuzungumzwa na watu wa ustawi wa jamii na lina nafasi kubwa sana kufanikiwa.

  Lakini all in all Busara zaidi inahitajika katika kufikia maamuzi ya kumpata mtoto .
   
 12. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,070
  Likes Received: 6,533
  Trophy Points: 280
  asanteni wana sheria
   
 13. L

  Leornado JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii ishu imekuwa ngumu, kila anayeombwa ushauri anakula kona, sio wachungaji wala wazee wa ukoo.

  Pia kama wataalamu wa sheria walivyoeleza hapo juu, chance ya hawa jamaa kushinda kesi mahakamani ni ndogo sana. Sasa sijui busara ipi itumike kumchukua mtoto.
   
 14. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukiona hata wachungaji na wazee wa ukoo wanakula kona, then ujue hapo hata wao wanaona suala ni gumu hasa kwa upande wa mwanaume. kitu cha msingi hapa ni jamaa kujaribu kuachana na dhana ya kushinda au kushindwa juu ya kupata mtoto. Watu wengi hatupendi kukubali makosa yetu, tukiamini kuwa kufanya hivyo ni sawa na kukubali kushindwa. Nikisoma maandishi yako, unachotaka kujua ni njia ipi itumike kumchukua mtoto. Moyoni mwako umeshafanya maamuzi kuwa lazima mtoto achukuliwe kwa njia yoyote ile bila hata kuangalia interests za mtoto. Narudia, interest za mtoto ni paramount. Atumie busara na hekima kwa kuangalia kwanza interests za mtoto. Kila mtu ameumbwa na busara lakini kiwango cha hekima kinatofautiana.
   
 15. L

  Leornado JF-Expert Member

  #15
  Jul 14, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0

  Wazee wa ukoo wanadai jamaa aliharibu tangu mwanzo na pia hapo hakumshirikisha mtu hadi mambo yalivyoharibika ndio sasa wanatafuta ushauri.

  Mkuu naona umekomalia sana interest za mtoto, hebu dadavua hapo kidogo. Hivi mtoto mchanga nae ana interest? kwa sasa ana miaka mitano, anaweza kutoa maamuzi kama abaki TZ au aende kwa baba yake?, tukiachana na sheria kuwa abaki kwa mama hadi miaka saba. Hii sheria nayo imepitwa na wakati.

  Mama yake anadai hali ya hewa ya huko mwanae ataathirika,sasa kwa nini alikubali mwanzoni na baada ya mtoto kuzaliwa ndio anakataa?
   
 16. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Inawezekana wazee wa ukoo wako right. Kwa sababu kama angewashirikisha mwanzoni kabisa, wasingemshauri azae na huyo mwanamke kwa madhumuni ya huyo mtoto kwenda kuishi na mwanamke mwingine Marekani. Na inawezekana ndio maana jamaa hakuwashirikisha, kwa sababu atakuwa alijua wasingeafikiana. kwa maana nyingine, jamaa ilibidi atumie busara na hekima kutafuta ushauri kwanza kabla ya kuamua kwenda kuzaa na huyo mwanamke.

  Mkuu mtoto regardless ya umri wake ana interests kama binadamu wengine. Children are human being like older people. Wana haki ya kutoa maamuzi juu ya maisha yao. Hata pale panapokuwa na conflicting interests kati ya mtoto na mtu mkubwa, interests za mtoto zina prevail. Mtoto mchanga anayo haki ya kutoa maamuzi yake. Hilo halina mjadala na linalindwa na na sheria za watoto. Zipo njia zinazokubaliwa kutumika ili mtoto nae atoe maamuzi yake. Mkuu napingana na wewe kwa asilimia 100. Na kama hii ni fikra yenyewe then sidhani kama atafanikiwa kumpeleka huyo mtoto Marekani hata akifikisha umri wa miaka 7. Mtoto akiamua kuwa anataka kushi Tanzania, atamlazimisha kwenda kuishi marekani?
  [/QUOTE]

  Well, you may be right but as it stands, that is the law. Kusema tuu sheria imepitwa na wakati bila kuchukua hatua sidhani kama itasaidia kutatua tatizo lililo mikononi mwako.
   
Loading...