Sheria Inasemaje kuhusu Mirathi, Mjane akizaa mtoto nje ya wale wa Ndoa?

Pantomath

JF-Expert Member
Jan 4, 2019
789
3,230
Mume halali wa Ndoa alifariki miaka Sita iliyopita, watoto walichukuliwa na ndugu wa Mme, namaanisha kaka ambao kwake ni Shemeji, na Babu/Bibi ambao kwake ni wakwe...,
Katika mirathi alikabiziwa nyumba.

Baada ya miaka 5 kupita mke akaza na mwanaume mwingine(haishi naye wala hafiki nyumbani kwa mwanamke)
Na sasa anaishi na huyo mwanae hapo kwenye nyumba yao,

Sasa, Ukweni wamemwendea wakimtaka aachie nyumba kwa kosa la kuzaa na Mwanaume mwingine kwenye mji wao..

Jee sheria inamtoa au inambakiaza?.

Wahusika wote ni Watu wangu wa Karibu, ila mmoja wa wahanga, (Sitaja ni Ni huyo Mwanamke au Wakwe ili isilete biases katika mawazo humu) jana alikuja kuniomba ushari..

NOTE : Mali nyingine zote zilizokua chini ya watoto zilishauzwa na ndugu, hii ndugu wanasema watawashikia watoto kwa kuipangisha mpaka wakue..

Lakini pia Mjane aliongeza nyumba nyingine ndogo hapo hapo nje ambayo ameipangisha.

Mimi sina uzoefu kabisa na hayo mambo kabisa.

Huruma, Mihemko tuiache kwanza...
 
Mme wake wa mwanzo alipokufa ile ndoa yao ilikasimisha urithi kwa mke na watoto!
Mke ni pamoja na mayai yake ya uzazi ikiwa na maana ..maisha ya mwanamke yaendelee akiendeleza Mali zake na watoto wake (SIYO MALI ZA UKOO)
Huenda kaona meno pause inakaribia na hakuna dalili ya kuolewa akaamua kuzaa na yoyote!
Sasa ndugu wanataka kumtimua yanawahusu nini wakati mwanaume haishi naye pale?

Wewe kama ni miongoni mwa hao ndugu mpeni ushirikiano aishi aleee mimba yake!
Cha msingi mkumbusheni tu asiishi na mwanaume pale kwenye nyumba! Lakini kama hana Mme ...mpeni ushirikiano huyo bado mke wenu wa kufikia!
Hakuna namna yoyote ya kutenganisha mwanamke ni binadamu lazima ananyege sasa afanyeje kama hana wa kumuuoa?

Au mnataka mimba akaipangishe halafu yeye abaki?
Hakuna namna huyo ni wenu njia nzuri ongeeni naye vizuri na mvae viatu vyake nyege hazina baunsa!

Kuna wakati nawaza baadhi ya mila zinazorithi wake ziliona mbali zaidi kuliko ujuaji tulionao sasa!

Mara mia bora kurithi wajane au waume!
Yaaani ni bora kuoa mdogo wake mke baada Dada kufariki ili watoto wabaki salama!

Wahindi wamewezaje
 
Hio nyumba alikuta ishajengwa? Kama ndio hapo Sijui, labda wataalamu waje.

Hio nyumba wamejenga ndani ya ndoa?
Kama ndio, naamini na yeye ana haki yake humo unamtoaje kirahisi?
 
Hao ndugu za marehemu (wa mume) wajue tu mali zozote alizoacha ndugu yao baada ya kufa ni za mke na watoto haziwahusu.

Hiyo nyumba ni ya mjane na watoto wake

Hata akiolewa na mwanamume mwingine wanaweza kuishi naye pamoja ndani ya hiyo nyumba

Akiamua alete bwana sogeza tuishi ni juu yake.

Hivi kwa mfano mke ndiye angekuwa amekufa kabaki mwanamume mngeanza kumpangia mwanamume asizalie kwenye nyumba aliokuwa anaishi na mkewe?
 
Maana ya kurithi mali hiyo mali inakuwa ni ya kwako, unaweza kumrithisha mwingine na hakuna atakayeuliza. Hao wa toto ni mali ya mama yao sidhani kama atawafanyia jambo baya, na aliyezaliwa pia ni mtoto wa huyo mama hivo atakavyoona inapeendeza kuishi nao ukoo unahusika nini hapo. Kimsingi watoto waoewe tu haki yao ila sio kuanza kupelekana mahakamani kisa kazaa ni ujinga

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Mume halali wa Ndoa alifariki miaka Sita iliyopita, watoto walichukuliwa na ndugu wa Mme, namaanisha kaka ambao kwake ni Shemeji, na Babu/Bibi ambao kwake ni wakwe...

Baada ya miaka 5 kupita mke akaza na mwanaume mwingine(haishi naye wala hafiki nyumbani kwa mwanamke)
Na sasa anaishi na huyo mwanae hapo kwenye nyumba yao,

Sasa, Ukweni wamemwendea wakimtaka aachie nyumba kwa kosa la kuzaa na Mwanaume mwingine kwenye mji wao..

Jee sheria inamtoa au inambakiaza?.

Mmoja wa wahanga, (Sitaja ni Ni huyo Mwanamke au Wakwe ili isilete biases katika mawazo humu) jana alikuja kuniomba ushari..

NOTE : Mali nyingine zote zilizokua chini ya watoto zilishauzwa na ndugu, hii ndugu wanasema watawashikia watoto mpaka wakue.

Mimi sina uzoefu kabisa na hayo mambo kabisa.

Huruma, Mihemko tuiache kwanza...

Katika kuandika hio Milathi nilikua nasita jee ni mirathi au urithi,
Naomba tofauti kati ya Mirathi na Urithi.
Ni dini Gani? Tuanzie hpa
 
Mme wake wa mwanzo alipokufa ile ndoa yao ilikasimisha urithi kwa mke na watoto!
Mke ni pamoja na mayai yake ya uzazi ikiwa na maana ..maisha ya mwanamke yaendelee akiendeleza Mali zake na watoto wake (SIYO MALI ZA UKOO)
Huenda kaona meno pause inakaribia na hakuna dalili ya kuolewa akaamua kuzaa na yoyote!
Sasa ndugu wanataka kumtimua yanawahusu nini wakati mwanaume haishi naye pale?

Wewe kama ni miongoni mwa hao ndugu mpeni ushirikiano aishi aleee mimba yake!
Cha msingi mkumbusheni tu asiishi na mwanaume pale kwenye nyumba! Lakini kama hana Mme ...mpeni ushirikiano huyo bado mke wenu wa kufikia!
Hakuna namna yoyote ya kutenganisha mwanamke ni binadamu lazima ananyege sasa afanyeje kama hana wa kumuuoa?

Au mnataka mimba akaipangishe halafu yeye abaki?
Hakuna namna huyo ni wenu njia nzuri ongeeni naye vizuri na mvae viatu vyake nyege hazina baunsa!

Kuna wakati nawaza baadhi ya mila zinazorithi wake ziliona mbali zaidi kuliko ujuaji tulionao sasa!

Mara mia bora kurithi wajane au waume!
Yaaani ni bora kuoa mdogo wake mke baada Dada kufariki ili watoto wabaki salama!

Wahindi wamewezaje
Mimi Naona Cha Muhimu ni kutofuatila Maisha ya mtu, Cha muhimu mtu apewe faraja stahiki, kufiwa Sio mtu anapenda ila kinachotakiwa Maisha yaendelee!! Hakuna mwenye kuishi milele, sasa huyo mama kaamua kuzaa, kwani kulea mtoto pale kwenye hiyo nyumba itaanguka!? Cha Muhimu afanye jitihada wale watoto watambue yule ni mdogo wao WA damu, hata kama ni ya upande mmoja, by the way hizo Mali ambazo mtu anaacha ni nyingi kiasi Gani hadi familia iishiwe amani!? Huu ni umaskini uliopitiliza
 
Hicho kisa kinaelekea kua kama hiki kabisaa..

Mme alivyokufa wakamuomba wamsaidie kulea watoto, wakadai wamewapekeka English medium gharama ni kubwa wakaanza kuuza mali zilizochini ya watoto, walivyomaliza wakamuambia mjane njoo huku tuna nyumba yetu haina mkaaji uishi karibu na wanao hio upangishe,

Alivyokua mpole dada wa watu akakubali, yupo kule majirani wakamtonya, Baba mkwe wako yupo huku na mteja anataka auze nyumba..

Aliondoka usiku kwa lori bila mtu kujua Asubuhi akiwa na polisi aliwakuta Kwa mwenyekiti wanakamilisha mambo, ndio pona yake, ila watoto walimtupia.
Kuanzi pale yule dada sio yule niliyekua namjua, hana roho ya kinyonge tene..

Kwa hio, huyo Mjane awe makini, hio nyumba inaweza ikauzwa, na watoto atarudishiwa, mpaka hapo itakua kwisha habari yake watamtoa kwenye familia yao na yeye atarudi kwa wazazi tena..

Kama sheria inambana ila akomae isiuzwe iwe ya watoto.
 
Mume halali wa Ndoa alifariki miaka Sita iliyopita, watoto walichukuliwa na ndugu wa Mme, namaanisha kaka ambao kwake ni Shemeji, na Babu/Bibi ambao kwake ni wakwe...

Baada ya miaka 5 kupita mke akaza na mwanaume mwingine(haishi naye wala hafiki nyumbani kwa mwanamke)
Na sasa anaishi na huyo mwanae hapo kwenye nyumba yao,

Sasa, Ukweni wamemwendea wakimtaka aachie nyumba kwa kosa la kuzaa na Mwanaume mwingine kwenye mji wao..

Jee sheria inamtoa au inambakiaza?.

Mmoja wa wahanga, (Sitaja ni Ni huyo Mwanamke au Wakwe ili isilete biases katika mawazo humu) jana alikuja kuniomba ushari..

NOTE : Mali nyingine zote zilizokua chini ya watoto zilishauzwa na ndugu, hii ndugu wanasema watawashikia watoto kwa kuipangisha mpaka wakue..

Lakini pia Mjane aliongeza nyumba nyingine ndogo hapo hapo nje ambayo ameipangisha.

Mimi sina uzoefu kabisa na hayo mambo kabisa.

Huruma, Mihemko tuiache kwanza...

Katika kuandika hio Milathi nilikua nasita jee ni mirathi au urithi,
Naomba tofauti kati ya Mirathi na Urithi.
Mchakato wa mirathi uliisha? Na kama uliisha nyumba hiyo alipewa nani?
 
Hao ndugu tamaa na umaskini zinawasumbua tu. Tuanze na mume alipofariki, mali zilibaki kwa mama na watoto hata kama watoto walipelekwa kuishi mbali. Mgawanyo wa mali haukubadirika baada ya mke wa marehemu kuzaa tena hata baada ya mume kufariki. Hao ndugu wasijifanye wao ni mume wa huyo mke. Wasiguse mali za mke wa marehemu ndugu yao. Wana wivu utadhani marehemu aliwaolea wao.
 
Mchakato wa mirathi uliisha? Na kama uliisha nyumba hiyo alipewa nani?
Kila kitu kiliisha, Alipewa Mjane kwa maamuzi ya Mahakama,

Mjane aliulizwa unataka nani awe msimamizi wa mirathi, akamtaja Baba mkwe na akataka kila kitu kiwe chini ya baba mkwe,
Mahaka ikamuambi hapana angalau hii nyumba iwe chini yako...

Yule Dada alikua mdogo sana alikua hajui chochote vitu vingi aliwapa wao, aliwaamini sana kutokana na upendo aliokua akipata......

Alikua kila kitu akiulizwa anasema mpeni baba,
Wakati huo akili yake pia haikua sawa kuwaza mengine maana ndio kampoteza mume.
 
Ifikie wakati wagombania mirathi muanze kuoana ndugu,Dada na kaka ili mulinde cycle ya Mali zenu ikitokea mauti kusiwepo na usumbufu. Mnawahangaisha sana wajane. Watu kaskazini bhana!!!
Umeathirika na ili swala uku kaskazini?
Mbona unakomalia sana watu wa kaskazini na ili swala
Wewe unatoka wapi na jamii yenu mnatatuaje ilo swala tuwaige
 
Naona wengi wa wachangiaji ni wahusika was upande mmoja na wanajibu ki mihemko bila kuhoji
- huyo mama alibaki kwenye hiyo nyumba Kwa makubaliano yapi?
-je baada ya mume kufariki ugawaji wa kisheria either za kidini au kidunia ulifanyika? Na hiyo nyumba alikabidhiwa nani?
-je huyo mwanamke hiyo nyumba ilikuwa inamuhusu Kwa kiwango Gani kipindi yupo na mumewe? Je walijenga wote, aliikuta, na kama aliikuta huyo mumewe aliipataje? Aliijenga au alilithi?
-je kama nyumba ilikuwa Mali ya marehemu Kwa asilimia mia je marehemu aliweza andika mirathi kabla hajafa kuhusu hiyo nyumba?
-je hiyo nyumba yote alikabidhiwa huyo mwanamke au still ilikuwa ya jumuhiya ilioachwa na marehemu(mama+watoto)hivyo kila mtu anasauti na mamlaka juu ya hiyo nyumba? Hivyo hao ndugu wanasimama mbadala wa watoto
 
Mjane ambaye bado ni kijana aolewe.

Mjane ameshindwa kukaa au tuseme watoto aliporwa na ndugu wa mume, sawa.

Ameamua kubeba ujauzito ndani ya nyumba ya watoto.

Hapo anatakiwa apishe kwenye nyumba ya watoto aende huko kwa mume mpya.

Sijui kama hiyo nyumba ya watoto ndugu hawataiuza 😭😭 kifo hakina huruma.
 
Back
Top Bottom