sulphadoxine
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 2,257
- 645
KATIKA jamii ya makabila mengi ya Kiafrika kumekuwepo mtazamo kwamba mwanaume akishalipa mahari kwa ajili ya kumuoa mwanamke fulani hata kama yeye mwenyewe hana habari au hapendi, atapaswa akubali na kwamba hiyo itakuwa ni ndoa halali.
Kutokana na mtazamo huo, wamekuwa wakijitokeza wajanja wachache katika jamii au makabila hayo, hasa wazazi, kuamua kupeana mahari bila vijana wao kujua au mtu mzima kuamua kutoa mahari ili kumuoa binti yeyote bila hata binti mwenyewe kujua.
Pengine suala hilo ndilo limefanya kuwepo kwa tabia ya watoto wadogo wa kike kuolewa bila hata wenyewe kujua. Inashangaza kuna kabila hapa nchini ambapo mwanamme mtu mzima eti anaweza akafanya booking ya ujauzito ikiwa mama mhusika atajifungua mtoto wa kike. Mwanaume huyo anaweza kulipa kabisa mahari.
Yawezekana mtazamo huo bado upo, ingawa kwa uchunguzi wangu hivi sasa umepungua kutokana na ndoa za kimila kuwa chache na badala yake ndoa nyingi kufungwa kidini na kiserikali ambapo, ahadi za ndoa lazima zitolewe mbele ya watu ambao walishatangaziwa kuwepo kwa tukio hilo ikiwemo kualikwa katika sherehe ili wawe mashahidi.
Ni kutokana na hali hiyo, Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971, inasisitiza kwamba ndoa halali lazima ishuhudiwe na watu walao wawili ambao sio pamoja na yule anayefungisha ndoa hiyo. Ushuhuda huo ndio unaotambulika kuwepo kwa sherehe ya ndoa ambayo kwa kawaida yaweza kuendelea miongoni mwa ndugu na jamaa katika kumbi mbali mbali.
Kwa hiyo ikitokea utata katika kuwepo kwa ndoa kinachoangaliwa sio cheti tu cha ndoa kama ambavyo hivi sasa imezoeleka, bali pia upande usiotambua kuwepo kwa ndoa unaweza ukasema kwamba hakukuwa na watu walioshuhudia ndoa husika kufungwa au kisheria ni kwamba hakukuwa na sherehe ya ndoa.