Sherehe za Nane Nane mkoani Mbeya ni zaidi ya Krismasi, Pasaka na Eid zote

Nyanda za juu kusini Mbeya ambapo ndio stoo/kapu la taifa la chakula. Mikoa hii ndiyo "food reserve"ya nchi.
Ila mbeya swala la chakula limerahisishwa sana

Luna siku nienda kwa mama ntilie nikaagiza wali maharage wakaniletea na parachichi wakati nashangaa nikastukizwa na mtindi umewekwa mezani

Nikaanza kuogopa maana mfukoni nilikuwa na buku hiyo hiyo . Kabla sijala nikajisemesha nikasema "daah mama bora tumalizane nikupe chako mapema"

Nikamchapa na buku nikiwa maskizia kama atadai pesa nyingine kumbe ndio huduma yake hiyo kwa buku unapata parachichi na maziwa mgando saafi
 
Na huku ndio wafanye yawe yanafanyika Kimataifa sio kupeleka Dar,Dom,Moro au Arusha..

Maonyesho ya Kimataifa ya Kilimo yawe yanafanyika Mbeya..

Kiujumla kwa Mbeya ,nane nane huwa ni siku kuu kubwa Sana,hakuna mkoa wanasherekea nane nane hapa Tanzania ukiacha Mbeya na Songwe.

Kabisa huu ndio ukweli hata zilipofutwa Mbeya waliendelea kusherehekea kwa nguvu kubwa sana
 
Haaa kwani ulijua anafanya mzaha kama huko kwenu?

Mbeya kuna nane nane,mwaka mpya na krismas kidogo..

Krismas huwa wanasherekea ndani zaidi,Rukwa wao krismas ndio sherehe zingine huwa hamna kitu..

Dar huwa naona Mwaka mpya na siku kuu za kiislamu.

Kabisa basi nikazoea nilikua addicted kila nane nane kama nipo Bongo hua nasafiri nafika kuisherehekea Mbeya ndio najisikia furaha
 
Mbeya kuna nini ndugu, jiji limejaa bajaji na zinaonekana kama kinguni kwenye godoro

Umeona bajaji tu hujaona ni gateway kwanza ya kuingiza mazao kama kahawa, ufuta, soya na karanga kutoka zambia na malawi kwenda Uganda, Rwanda na sudan kusini, hujaona kua mpunga wa kyela watu wanatajirika, hujaona ndizi za tukuyu zinazopatikana mwaka mzima, hujaona maharage kule umalila, hujaona viazi mviringo, hujaona hata kahawa kule mbozi, endelea kuona bajaji ukizeeka utaona maguta
 
Ila mbeya swala la chakula limerahisishwa sana

Luna siku nienda kwa mama ntilie nikaagiza wali maharage wakaniletea na parachichi wakati nashangaa nikastukizwa na mtindi umewekwa mezani

Nikaanza kuogopa maana mfukoni nilikuwa na buku hiyo hiyo . Kabla sijala nikajisemesha nikasema "daah mama bora tumalizane nikupe chako mapema"

Nikamchapa na buku nikiwa maskizia kama atadai pesa nyingine kumbe ndio huduma yake hiyo kwa buku unapata parachichi na maziwa mgando saafi

Hahaaa Mbeya unapewa chakula na mama ntilie baadae anakuuliza kama haujashiba akuongeze kwa pesa ile ile ya mwanzo wanaita kukubalansia
 
Mbeya Mbeya Mbeya!
Moja ya mambo yakustajaabisha ambayo nimekua nikiyaona Mbeya kwa miaka yote 20 niliyoifahamu Mbeya kwa kupita nikiwa naenda mahali pengine au kukaa kidogo ni sherehe za Nane Nane ambazo hakuna mkoa wowote Tanzania ambao wanasherekea sikukuu hizo kama Mbeya.

Mbeya sikukuu za Nane Nane kuanzia wanaume, wanawake, watoto wote huvaa nguo mpya kabisa mimi ni shuhuda wa hilo.

Mbeya Sikukuu za Nane Nane kila nyumba lazima wapike pilau na nyama na vinywaji watakunywa vya kutosha hii ni kwa kila nyumba hata vijijini.

Mbeya sikukuu za Nane Nane mzunguko wa pesa hua mkubwa kuliko kawaida na biashara hua kubwa kuliko wakati wowote ule kwani watu hununua mahitaji kwa wingi kuanzia nguo na vyakula na mambo mengine.
Mbeya nane nane ndio utaona watu wengi wakipishana huku na kule kuanzia Mbalizi, Uyole, Igawilo, Chunya, Tukuyu, Kyela, Chimala yaani watu hupishana kwa wingi sana.

Hakuna mkoa Nane Nane inachukuliwa kwa ukubwa nchi nzima isipokua mkoa wa Mbeya hata sikukuu hizo zilipofutwa mbeya waliendelea na utamaduni wao huo miaka yote.
I see wewe mkubwa umenishangaza utadhani tulikuwa wote. Nikiwa hapa Iringa Jana nimeombwa hela ya nguo ya sikukuu na Demu wangu Mnyakyusa. Nikabaki nashangaa, mbona sikukuu ziko mbali au Maulid ya Mtume lakini mbona jina la Kikristo? Akanijibu sikukuu ya NANENANE!!!
 
Mbeya Mbeya Mbeya!
Moja ya mambo yakustajaabisha ambayo nimekua nikiyaona Mbeya kwa miaka yote 20 niliyoifahamu Mbeya kwa kupita nikiwa naenda mahali pengine au kukaa kidogo ni sherehe za Nane Nane ambazo hakuna mkoa wowote Tanzania ambao wanasherekea sikukuu hizo kama Mbeya.

Mbeya sikukuu za Nane Nane kuanzia wanaume, wanawake, watoto wote huvaa nguo mpya kabisa mimi ni shuhuda wa hilo.

Mbeya Sikukuu za Nane Nane kila nyumba lazima wapike pilau na nyama na vinywaji watakunywa vya kutosha hii ni kwa kila nyumba hata vijijini.

Mbeya sikukuu za Nane Nane mzunguko wa pesa hua mkubwa kuliko kawaida na biashara hua kubwa kuliko wakati wowote ule kwani watu hununua mahitaji kwa wingi kuanzia nguo na vyakula na mambo mengine.
Mbeya nane nane ndio utaona watu wengi wakipishana huku na kule kuanzia Mbalizi, Uyole, Igawilo, Chunya, Tukuyu, Kyela, Chimala yaani watu hupishana kwa wingi sana.

Hakuna mkoa Nane Nane inachukuliwa kwa ukubwa nchi nzima isipokua mkoa wa Mbeya hata sikukuu hizo zilipofutwa mbeya waliendelea na utamaduni wao huo miaka yote.
Ni Sabasaba Mkuu na sio nanenane!
 
Back
Top Bottom