Sherehe ya miaka 50 ya Uhuru, umejifunza nini?

Nadhani yapo mengi ya kujifunza, na hivyo kuchukua hatua katika uongozi wetu.
  1. Maraisi wa Africa Mashariki hawakufika walituma wawakilishi, kwa nini? Tumekosa nini? Lile ambalo tumekosa tulifanyie kazi, au wao ndio wamekosea?
  2. Onyesho la polisi wa mbwa na farasi kupambana na waandamaji katika Uwaja wa Uhuru, lilikuwa na mantinki ipi? Message ipi ambayo waonyeshaji walikuwa wamelenga? Nadhani halikuwa pahala pake!! Tuepukane na viashiria vya kuvuluga amani.
  3. Maendeleo tuliyoyapata ni kidogo ukilinganisha na matarajio kama nchi zingine zilivyofanya, katika kipindi hicho cha miaka 50; k.m Malaysia, China na Singapore ambazo uchumi wao ulikuwa karibu sawa na Tanganyika.
 
Mosi,nimejifunza kupasua yale matofali membamba ya kuchoma kwa kutumia ngumi kama wale askari walivyoonyesha pale uwanjani,
Pili, nimejifunza na kugundua kuwa jeshi letu linatumia vibaya nguvu waliyonayo dhidi ya raia hususani baada ya kuona lile igizo la waandamanaji kukamatishwa mbwa waliloigiza askari wale mbele ya umma.
Tatu, nimejifunza kuwa rais anaweza kukagua gwaride la jeshi lake akiwa na bodyguards wake wawili ambao sio wanajeshi tena waliovalia style ya 'men in black'.
 
Mi bado nipo nipo kwanza ngoja 2cheki 50 mingine labda 2tapata cha kujivunia na kujifunza. Kwasababu mim ckupata nafasi/kitengo cha kutafuna pesa za tanganyika kama walivyopata wachache kwan kuna wa2 wamenunua nyumba,magari na vi2 vingine vya thaman kwa pesa hiz 2 za sherehe.
 
Ndugu wana JF,sherehe ya jana mmejifunza kitu gani?

matumizi makubwa ya rasilimali za walipa kodi yasiyo na tija.wakati tunatumia mabilioni ya shilingi kwa kufurahisha na kuwafaidisha baadhi ya watu watanzania wanakufa kwa njaa kwa kutokuwa na chakula.ingependeza kama wangetupatia gharama ambazo zimetumika katika sherehe hizi na kama kuna chenji imebaki na ni lini tunavunja kamati ya maandalizi
 
...Tanganyika ipo hai
...Tanganyika siyo maskini ila watu wake ndiyo maskini
...Matumizi ya fedha si kitu cha hovyo ktk sherehe hata kama tunazihitaji kwa shughuri za maana eg mishahara na malimbikizo ya wafanyakazi
...Tunapaswa kutmia pesa nyingi saa ktk sherehe zetu eg HARUSI, UBATIZO, KITCHEN PART, KIPAIMARA potelea mbali watoto wasisome
 
Nimejifunza sana, Never Trust Magamba Company hasa Fisadi Kikwete na genge lake. And also never VOTE for Magamba ni Wabakaji wa Demockasia na ni Majambazi wa Rasilimali zetu. 2015 Never late Magamba wachukue nchi, kuwa wabunge katika jimbo lako au hata kuwapa nyumba yako wakusafishie, watatua 2015 kama tusipo watimua. Magamba its time to pack your and leave our country Tanganyika alone
 
nimejifunza kumbe taifa linapesa nyingi kwa mambo ya jikinga na cyokwa kuwpa mikopo wanafunzi wa elimu ya juu, kuongeza mishahara kwa watumishi wa uma kama vle walimu........na kjipendekeza na kauli za kijinga.........kwani kama ni uhuru wa tanzania bara kwa nini walipeperusha bendera ya tanzania? kwa nn hakukua na raisi wa tanzania bara badala yake wakaleta raisi wa muungano? kwa nini usalama ulikuwa chini ya waziti ambaye ni mzanzibari?
 
Mosi,nimejifunza kupasua yale matofali membamba ya kuchoma kwa kutumia ngumi kama wale askari walivyoonyesha pale uwanjani,
Pili, nimejifunza na kugundua kuwa jeshi letu linatumia vibaya nguvu waliyonayo dhidi ya raia hususani baada ya kuona lile igizo la waandamanaji kukamatishwa mbwa waliloigiza askari wale mbele ya umma.
Tatu, nimejifunza kuwa rais anaweza kukagua gwaride la jeshi lake akiwa na bodyguards wake wawili ambao sio wanajeshi tena waliovalia style ya 'men in black'.

Haleluyaaaaaaa! nimejifunza jambo moja ktokana na mchango wako hapa, kuwa unapofanya jambo mbele ya jamii usifikiri kwa kuwa uko mbele utakuwa umewazidi watu wote ufahamu na kile unachokionyesha kuwa kitakuwa kipya na cha kufurahisha sana, la hasha! Unawezaona watu wanakutazama kwa umakini ukafikiri wanakusikiliza kumbe wanakushangaa, au wanacheka ukafikiri wamefurahi kumbe wanakuzomea, Jua kuna wenye uelewa mpana kuliko wewe hivyo wawezafanya jambo kama fumbo likawekwa wazi muda huo huo, au ukawa unatenda jambo ambalo litaonekana la zama za mawe za kale.. Kumbe imekuwa aibu na mabilioni yote yaliyotumika kwa siku moja tu! Kwanini wasingeadhimisha japo kwa kumuunga mkono Sabodo kwa kuwajengea wananchi visima vya maji maana hatuna tena mbinu mpya, akili ya viongozi wetu haziwezi tena kubuni kitu kipya, zimefikia mwisho wa kufikiria, yaani zimeathiriwa na virus fulani hivi.
 
nimegundua kumbe jeshi linatumia hela nyingi za umma kununua vifaa vya kivita wakati kila siku tunahubiri amani amani, hizo hela almost 25% ya bajeti ya nchi kila mwaka ingeelekezwa kwenye kilimo sasa hivi tungekuwa tunabadilsihana vyakula kwa mafuta na nchi za kiarabu.
 
Bado hatuna viongozi bali watawala,pana haja gani ya kufuja jasho la maskin kwa ajili ya ule upuuz wakat nchi ipo jehanamu ya umaskini!je pana ya kufanya sherehe ili hali mwanao anavaa nguo zenye viraka?yale yalikuwa maonyesho ya urembo kwan hayana tija kwa wananchi tz.Ipo siku wenye hekima wataongoza tz so wale mbweha wa jana tulonao.
 
Back
Top Bottom