Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,163
Kumbe inaweza kuwa kweli.Ngoja tusubirie taarifa kamili.Mtaani tetesi zimeanza tayari.
Daisy, hili ni fumbo? Changamsha genge? Chai ? Au jambo lililotokea kweli?Kaka mmoja alikuja mkoani kwetu kwa barua kutoka Wizarani, aliletwa pale kama Ofisa wa Serikali. Ule mkoa una neema sana, ndani ya miaka miwili yule kaka aliweza kujenga ghorofa pale mjini.
Siku ya ufunguzi wa ghorofa lile, alitualika watumishi wenzake, viongozi wa dini na mama yake mzazi tuliambiwa atafika na basi la saa saba mchana hivyo dua zimsubiri mgeni huyu muhimu.
Tulifika saa 12 asubuhi kusaidia shughuli, tulikata vitunguu na kupika pilau, tulikata kachumbari na tulitengeneza salad ya matunda. Wali maharage na wali kuku havikukosekana.
Basi la saa saba likawasili, mwenye sherehe akaenda kumpokea mgeni wa muhimu. Kufika kule wanamkuta mama amekauka kwenye kiti cha basi. Alifariki saa ngapi ni siri ya Mungu. Basi chakula cha sherehe kiligeuka kuwa cha msiba.
Hahaha nimeona funzo, ni kwamba;Hadithi hii inatufundisha nini? [emoji2369][emoji2369] [emoji3][emoji3][emoji3]
Dhuluma ni kitu ambacho huwa ninajitahidi sana kukikwepa hapa duniani. Hakuna raha kama kula pesa halali kwa maana hauna stress wala wasiwasi mkuumichongo ya dhuluma
Umewaza mbali. Ubwabwa huwa hauachwi kwa kisingizio cha sababu yoyote ile!Ubwabwa ni ubwabwa tu waalikwa wataula regardless ya sababu.
Kabisa mkuu, na ukitaka kuamini kufa halafu ubwabwa upikwe uone kama hautaisha.Umewaza mbali. Ubwabwa huwa hauachwi kwa kisingizio cha sababu yoyote ile!
Wee fikiria, ubwabwa wa kisiasa wa mh.Rungwe ulilambwa hata na watu wasiomuunga mkono.
Kweli ubwabwa ni ubwabwa tu.
[emoji846][emoji4][emoji4][emoji2][emoji1787][emoji1787][emoji1787]!Kabisa mkuu, na ukitaka kuamini kufa halafu ubwabwa upikwe uone kama hautaisha.