Shem alioteshwa je kuna ukweli?

Shem alioteshwa je kuna ukweli?

EPORA

Member
Joined
Apr 8, 2012
Posts
83
Reaction score
16
Habari wana mmu,

Nina rafiki yangu mpendwa katika Bwana,alikuwa na mpenzi wake aliempenda sana kuliko maelezo na kwa bahati mbaya hivi sasa wameachana,na kisa cha kuachana ni shem kudai kwamba Mungu ameongea nae kwenye ndoto kwamba huyo sio mkewe, Hivi ninapoandika sasa kwakuwa wote wameokoka,huyu rafiki yangu aliamua kumwomba Mungu ili ampe moyo wa kumsamehe na kusahau ila tatizo liko hapa,ameongea hadi na wachungaji na marafiki zake wapendwa waliokuwa nae ktk maombi,dada wa watu amelia sana akimwomba Mungu kwamba autoe huu upendo kwa huyo mwanaume lakini hadi sasa moyo umekataa.

Amefanya juhudi hadi kuamka usiku na kulia kwenye maombi sana hadi tunamwonea huruma,kibaya huyo kaka anamtumia msg ikiwa inaenda kwa mpenzi mpya ili kumuumiza na hawana mawasiliano yeyote ingawa huyo dada huwa anatamani kumpigia ila anajikaza tu,wote ni walimu wanamaliza mwakani,wapendwa ni kweli Mungu anaweza kumwotesha mtu ndoto kama hiyo na hapohapo akakupa mwingine?maana huyo kaka anajua jinsi anavyopendwa plz mchango wenu, Samahani sana kwa mpangilio mbovu nawasilisha
 
kiukweli ndo maana lazima kila binadamu lazima afanye dhambi Kwanini walikua wanagegedana kabla ya ndoa?Mungu anahusikaje hapo sasa kwenye zinaa hapo hamna cha kuoteshwa wala nini hizo zote ni ndoto nyevu zake tu
 
hao walitamaniana tu. By the way si huwa tunaamini Mungu aweza yote? Basi hata hayo yatokeayo ni mipango ya Mungu na aendelee kumuomba amuongoze.
 
Acheni kumshirikisha Mungu kwenye uzinzi. eti '...alikuwa na mpenzi wake... Mungu ameongea naye...'

Mkuu hata huyo dada amemwambia shem aache kumsingizia Mungu mambo yake,na shem katafuta gia ya kumwacha huyo dada akaona ni kumsingizia Mungu,wakati anajitafutia laana
 
Habari wana mmu, Nina rafiki yangu mpendwa ktk Bwana,alikuwa na mpenzi wake aliempenda sana kuliko maelezo na kwa bahati mbaya hivi sasa wameachana,na kisa cha kuachana ni shem kudai kwamba Mungu ameongea nae kwenye ndoto kwamba huyo sio mkewe.

EPORA ni kweli Mungu husema na watu kwa maono au ndoto kumjua mmewe au mkewe mtarajiwa,lakini hii inahitaji watu waliokiroho sana wenye uwezo wa kupambanua mambo kulingana na neno la Mungu.

Maana ndoto wakati mwingine huja kwa sababu ya mawazo unakuta kijana amempenda binti anamfikiri sana matokeo yake ni kumuota na kujifanya ameoteshwa na Mungu kumbe ni akili yake.Lakini wengine hutumia njia hii kuwapata wasichana wenye imani sana kwa Mungu kuwa watamuogopa Mungu na kukubali kirahisi kwa vile ni Mungu amesema.

Hutokeaje mtu anamchumbia mtu baadaye anamuacha kuwa Mungu kasema siyo mkeo/mmeo?

...Mara nyingi watu huanza mahusiano au mazoea kabla ya kumuomba Mungu labda mtu anaona dada fulani anavyomheshimu alivyomkarimu anaaona kuwa huyu anaweza kuwa mkewe,na anamweleza nia yake hiyo ya kutaka awe mkewe.Sasa kwa vile mtu huyu anamtegemea Mungu wengi hihitaji kuthibisha kama kweli huyo ni mkewe kama siyo mwenyewe, Mungu anamwambia siyo huyo,na yeye inabidi amuache huyo na kuanza kuuliza kwa Mungu mkewe ni yupi hapo huweza kuonyeshwa mkewe/mmewe halisi.

Ila kwa watu walio makini zaidi hawawezi kumtamkia msichana kuwa ni mke mtarajiwa bila kuthibisha kwa Mungu,wakishathibitisha kwa Mungu ndiyo humjulisha na binti nia yake ya kuwa naye hata mimi nilitumia hii nimeona inalipa.

Kwa mwanaume mwenye hekima siyo vyema sana kumfuata binti na kumwambia unataka kumuoa vile Mungu kasema badala yake ni kumweleza jinsi amempenda na Kama Mungu ikimpendeza atamuoa.

"Mkwe mwenye busara mtu hupewa na Bwana"

Ameongea na Mungu........! mbona Enzi za Musa zishapita
 
hao walitamaniana tu. By the way si huwa tunaamini Mungu aweza yote? Basi hata hayo yatokeayo ni mipango ya Mungu na aendelee kumuomba amuongoze.

Mkuu Mungu amwongoze kwenye nini hapo?
 
Mkuu hata huyo dada amemwambia shem aache kumsingizia Mungu mambo yake,na shem katafuta gia ya kumwacha huyo dada akaona ni kumsingizia Mungu,wakati anajitafutia laana

laana ataipata kama amemuacha kwa hila lakini kama ni Mungu kweli kasema hakuna laana hapo nilishakutana na case nyingi kama hizo.
 
Mpendwa katika Mungu...
Kuoteshwa na Mungu kuwa aache kumgegeda aanze kugegeda mwingine!!
Mungu anaotesha mambo ya ajabu eeeh!!
 
Mzinzi tu huyo han lolote. Wanaopata mafunio ya Mungu live kama anavodai sio watu lelemama wa wokovu hapana lazma mtu awe amesimama kwaMungu sawasawa. Amemsingizia Mungu kuhalalisha tamaa zake za uzinzi tu.
 
Ni kweli mkuu swala la kuomba mke/mme linahitaji kusimama kwa Mungu sawasawa na maombi ya kuatamia siyo ya kubeep beep.
 
Mi sijakataa kwamba Mung anasema kwa njia ya ndoto ninachoamini upendo hufa ila wa huyu dada mhhhh!mchungaji amemshauri amwachie Mungu yeye aendelee na yake ila mwenzetu anaamka saa tisa anaomba kwa machozi na kulia sana kwamba Mungu amsaidie upendo uishe maana she is suffering na huyo kaka amemwambia asimtafute looooh!na anajizuia hata kumsms
 
Yaani hapa wakuu ninachoomba ni nini cha kufanya maana kama kumwomba Mungu kamuomba,amesamehe na ameshamwambia huyo kaka yeye aoe tu hata kama anajua moyo wa huyo dada unavuja damu,ni kweli huyo dada ni mzuri na anajiheshimu sana huenda alitumia kila mbinu kumpata
 
EPORA nani alikwambia moyo huwa unavuja damu ukitendwa ni maneno ya mitaani hayo cha kufanya aombe neema ya Mungu juu yake atapata amani tu kadri muda unavyokwenda,na kama yule jamaa alitenda kwa hila Mungu atamhukumu kwa haki asipotubu, na huyo dada kama alizini na jamaa na yeye ana hatia naye atubu na Mungu atamrehemu kama hakuzini naye basi Mungu atamtafutia mwingine wa kufanana naye.
 
Mi sijakataa kwamba Mung anasema kwa njia ya ndoto ninachoamini upendo hufa ila wa huyu dada mhhhh!mchungaji amemshauri amwachie Mungu yeye aendelee na yake ila mwenzetu anaamka saa tisa anaomba kwa machozi na kulia sana kwamba Mungu amsaidie upendo uishe maana she is suffering na huyo kaka amemwambia asimtafute looooh!na anajizuia hata kumsms

Anaomba upendo uishe hiyo ni ngumu maana hilo ni tunda la Roho ila anachotakiwa kuomba ni amani.
 
Tabia ya walokole feki kutumia jina la Mungu kufanya maovu inakera saana...!

Hata aibu hana eti ameoteshwa na Mungu... !!
 
Back
Top Bottom