Shelukindo: Namuunga mkono Lowassa kumrithi Kikwete

Shelukindo: Namuunga mkono Lowassa kumrithi Kikwete

yegella

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2010
Posts
3,113
Reaction score
1,104
Mh Beatrice Shelukindo ameamua kuvunja ukimya baada ya kutangaza kumuunga mkono Edward Lowassa kumrithi Mh. Rais Kikwete.

Shelukindo alitoa kauli hiyo Jumapili wakati akiwasalimia wakazi wa Monduli baada ya kukaribishwa kuchangia ujenzi wa Hosteli ya KKKT katika sherehe za kukaribisha Mwaka Mpya zilizofanyika nyumbani kwa Lowassa ambazo pia zilihudhuriwa na makada kadhaa wa CCM.


Kazi kwako Nape na Mangula, je bado siku 90 hazijafika?


=================
Beatrice Shelukindo mnuso huu ulikulevya...



P1000772.JPG

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa wakiwapungua mikono wageni waalikwa wakati wa hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kusherehekea Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake Monduli.
P1000790.JPG

Mbunge wa Jimbo la Kilindi,Mh. Beatrice Shelukindo (wa pili kulia) akiambatana na Mbunge wa Jimbo la Bariadi,Mh. Andrew Chenge wakati wakiwasili kwenye hafla ya Chakula cha Mchana iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013.
P1000746.JPG

Wafanyabiashara maarufu jijini Arusha,Papa King na Mdau Mathias (MNEC) wakiwasili kwenye hafla hiyo.
P1000796.JPG

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akihutubia wageni mbali mbali waliohudhulia hafla ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya kuukaribisha Mwaka Mpya wa 2013,iliyofanyika nyumbani kwake,Monduli.
P1000798.JPG

waalikwa wakipata Chakula nyumbani kwa Mh. Lowassa.
 
acha kutukana wengine maana huenda hapo ulipo ni fisadi hata kuliko lowasa.Tena unaweza kuwa hata jambazi
 
Waziri mkuu aliyejiuzulu kutokana na kashifa inayoendelea kumwandama hadi leo ya richmod,akiwa ngomeni kwake Monduli ameapa kumrithi mwenzake ------ kama walivyopanga walipokuwa marafiki walioshibana.

Kabla ya sera yake ya -maamuzi magumu inayomfanya awe tofauti na swahib wake huyo,huku akiungwa mkono na mke wa aliyekuwa mwana kamati (mzee Shelukindo ) iliyosababisha Laigwanani kung'oka katika kiti cha uwaziri mkuu, bibi Bitrice Shelukindo (mbg.viti maalumu kilindi) amemuumga mkono ya kuwa atampigania kwenda white house magogoni, akaendeleze sera ya maamuzi magumu.
Yamenukuu magazeti karibu yote ya leo.

My take; mama huyu lazima kuna kitu kafanyiwa na Laigwanani. Kwani awali enzi za richmond saga, alimpinga Laigwanani kwa sauti yote, leo hii yupo kapuni mwake.
 
Tunaitaji rais mwenye maamuzi magumu kama Lowasa, rais ambae anamsimamo kwa sasa CCM ni Lowasa tu.

Tunahitaji rais fisadi kuliko Kikwete? je Lowasa ni maamzi magumu yapi aliwahi kuyafanya ambayo mtanzania asinge yaweza? Richmond au mvua ya kichina usiwe mjinga kushadadia upuuzi..
 
Tunaitaji rais mwenye maamuzi magumu kama Lowasa, rais ambae anamsimamo kwa sasa CCM ni Lowasa tu.

Mkuu, huo wadhifa huyo jamaa kaupata lini tena? Nasubiri kusikia kama huu nao utaitwa mpasuko kama ule tuliokuwa tunaelezwa upo CDM na kwamba utakisambaratisha chama hicho. Au watawala wao huwa hawana mipasuko ya mapande mapande?
 
mkuu njaa ni mbaya sana,nakumbuka huyu mama alivyotokwa na mapovu mdomoni wakati wa sakata la Richmond mpaka kufikia hatua ya kusema Maisha yao yapo hatarini lakini wanamwachia Mungu,siamini kama leo hii angechomoa maisha yake kwa Mungu na kuyarudisha tena kwa israel wake,FREEMASON AT WORK.
 
Watu wenye akili vizuri kama bado wapo CCM hawawezi kubali huo upuzi. Huyu bwana hana jipya tena alikuwa kwenye mfumo muda mrefu lakini hana alichofanya.
Bungeni ndio usiseme kule kawa bubu sasa tumpe urais mtu kama huyu ili tulie tena miaka 10? Apewe cheo cha MZEE WA MICHANGO HIYO ATAWEZA.
 
Hata mimi nitamuunga mkono Lowasa, anayo kura yangu tayari. Tunahitaji mtu mwenye maamuzi magumu, hata akiwa dictator kama Kagame lakini analeta maendeleo hamna shida, hata akila kidogo lakini analeta maendeleo hamna shida, kuliko kutokula kabisa halafu hata maendeleo haleti.

Hakuna mtakatifu duniani, kila mmoja alishawahi kutenda kosa mara moja au zaidi, sema tu wengine hata wale wanaowanyoshea wenzao vidole hawajawekwa peupe tu, cha muhimu ni kwamba, mtu akifanya kosa huwa kuna mazingira ya kujirekebisha. Kosa si kosa bali kurudia kosa.

Hata hivyo, suala la Lowasa na kashfa yake, inasemekana anazo njia za kujieleza ambazo ameweka fumbo, kuna siku wakati wa kampeni atakuja kujieleza na watu watashangaa kwamba walikuwa wanapiga mayowe ya bure kwa mtu asiyehusika.

Yapo mengi yamejificha mle kwenye ile kashfa, na inawezekana Lowasa akawa kafara tu. Na wapo wengi waliokuwa juu ya Lowasa wamefichwa, lowasa kachukua msalama wa wengi pale.
 
Bado anaota urais? Huyo mama si ndio alikuja na utabiri wa Mch. Joshua......
 
Hata mimi nitamuunga mkono Lowasa, anayo kura yangu tayari. Tunahitaji mtu mwenye maamuzi magumu, hata akiwa dictator kama Kagame lakini analeta maendeleo hamna shida, hata akila kidogo lakini analeta maendeleo hamna shida, kuliko kutokula kabisa halafu hata maendeleo haleti.

Hakuna mtakatifu duniani, kila mmoja alishawahi kutenda kosa mara moja au zaidi, sema tu wengine hata wale wanaowanyoshea wenzao vidole hawajawekwa peupe tu, cha muhimu ni kwamba, mtu akifanya kosa huwa kuna mazingira ya kujirekebisha. Kosa si kosa bali kurudia kosa.

Hata hivyo, suala la Lowasa na kashfa yake, inasemekana anazo njia za kujieleza ambazo ameweka fumbo, kuna siku wakati wa kampeni atakuja kujieleza na watu watashangaa kwamba walikuwa wanapiga mayowe ya bure kwa mtu asiyehusika.

Yapo mengi yamejificha mle kwenye ile kashfa, na inawezekana lowasa akawa kafara tu. Na wapo wengi waliokuwa juu ya Lowasa wamefichwa, Lowasa kachukua msalama wa wengi pale.

Tatizo la huyu bwana ni mwizi wa mali ya umma...
 
Bado anaota urais? Huyo mama si ndio alikuja na utabiri wa Mch. Joshua......

huyu Mama ni mtu mzuri sana kwa siasa za propaganda...Nakumbuka alikuja hadi na kimemo kutoka kwa TB Joshua kumbe ilikuwa usanii tu.
 
Msimamo wa uvccm ni kuwa raisi hatoki kaskazini.....
 
Kwa wale wanaojua connection kati ya hizi familia (Shelukindo & Lowassa) hawatapata mshangao wowote kwa kauli kama hii kutoka kinywani mwa mmoja wa hizo familia

Huu vile vile ulikuwa ni mtego wa Mh. Lowassa kwa viongozi wa CCM na wale wanaojiita comrade ndani ya serikali katika kujipambanua na kujua yupi ni rafiki wa kweli ndani ya chama na serikali na yupi ni 'masalia' kwenye kikundi cha 'Lowassa for President' ndiyo maana mwaliko ulitolewa kwa viongozi wote wakuu wa chama na serikali ngazi za mikoa na taifa na baadhi ya wabunge ambao ni influential


 
Back
Top Bottom