Ngongo
JF-Expert Member
- Sep 20, 2008
- 18,921
- 31,161
MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, William Shellukindo ameitafsiri hatua ya mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umeme(Tanesco), Dk. Idrissa Rashid kutangaza kuachana na mpango wa kununua mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans kuwa ni kukosa nidhamu kwa kuwa ameingilia mamlaka ya waziri husika.
Akizungumza na Mwananchi jana jijini Dar es Salaam, Shellukindo alisema: "Kitendo cha Dk. Rashid kutangaza kwamba nchi itaingia gizani na Tanesco isilaumiwe, ni utovu wa nidhamu kwa sababu haikuwa kazi yake kutangaza hilo, bali kazi ya Waziri wa Nishati na Madini.
"Tena hakupaswa kabisa kutoa kauli hiyo. Yeye ni mtendaji tu wa shirika la Umma... hana mamlaka ya kutangaza kwamba nchi itaingia gizani kwa kuwa hiyo ni kazi ya Waziri mwenye dhamana na Nishati na Madini."
Alisema Dk. Rashid anawajibika kwa waziri na kwamba chochote anachohitaji kufanya kuhusu masuala ya umeme kama tatizo hilo, ni lazima awasiliane na waziri husika, na si kwa matakwa yake.
Alisema kuwa Dk. Rashid alipaswa kupeleka taarifa kwa waziri juu ya uamuzi huo na waziri ndiye aliyestahili kutangaza hatua hiyo badala ya mkurugenzi huyo wa Tanesco na kuongeza kuwa katika kikao kijacho cha Bunge, kamati yake itamuita Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja ili atoe maelezo kwa kamati kama walikubaliana na Dk.Rashid kabla ya kutoa tamko hilo.
"Yawezekana alikubaliana na Dk. Rashid na kama ni hivyo basi aseme hivyo," Shellukindo alifafanua.
"Hata Waziri mwenyewe hana mamlaka ya kutoa kauli kama hiyo bila ya kuwasiliana na kupata ushauri wa Baraza la Mawaziri. Sasa je yeye Dk. Rashid alipata wapi mamlaka hayo," alihoji Shellukindo.
Alisema baada ya Dk. Rashid kutangaza Tanesco imejitoa katika suala la ununuzi wa mitambo hiyo, alipaswa kupeleka taarifa wizarani ili wizara iangalie hatua za kufanya, lakini kutokana na utovu wa nidhamu alionao, aliamua kutoa kauli mbaya na yenye kuwapa wananchi mfadhaiko.
Shellukindo pia alisema kauli hiyo ya Dk. Rashid inaweza kuwachonganisha wananchi na wabunge endapo nchi itaingia gizani na kwamba ukweli wa mambo hayo utajulikana baada ya kamati yake kukutana na waziri katika vikao vya mwezi ujao.
"Kamati yangu ndiyo yenye mamlaka ya kukutana na waziri, hata tunapomwita kwenye kamati, anaweza kuongozana na watu wa Tanesco lakini waziri ndiye mzungumzaji mkuu," alisema Shellukindo ambaye amekuwa na msimamo mkali katika sakata la ununuzi wa mitambo ya Dowans.
"Kutokana na hali hiyo hata Kamati ya Hesabu ya Kudumu ya Mashirika ya Umma bado haina mamlaka ya kukutana na waziri moja kwa moja kwa sababu, wao wanahusika na hesabu za mashirika ya ndani na wana mamlaka ya kukutana na Tanesco tu na kuhoji chochote kuhusiana na hesabu za shirika hilo na si waziri," aliongeza Shellukindo.
Kauli ya mwenyekiti huyo imekuja siku nne baada ya Dk. Rashid kutangaza kujitoa rasmi katika sakata la ununuzi wa mitambo ya kufua umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited iliyorithi mkataba kutoka kampuni hewa ya Richmond Development LLC.
Mbali na Dk Rashidi kutangaza kujitoa, alisema yeye na Tanesco wasije kulaumiwa pale inchi itakapokuwa giza na hospitali, viwanda pamoja na vyuo vikishindwa kutoa huduma nchini.
Kauli hiyo ya Shellukindo ilitanguliwa na kauli za wananchi wa kada mbalimbali wakiwemo wasomi na wanasiasa waliomtaka Mkurugenzi huyo Mtendaji wa Tanesco ajiuzuru wadhifa alionao kutokana na kauli yake hiyo.
Katika maoni yao wananchi hao walisema Dk Rashid alikuwa na kazi ya kuandaa mpango wa muda mfupi na mrefu, ili kuweka uhai na ufanisi ndani ya shirika hilo kwa sababu ni shirika pekee linalotegemewa na wananchi wote, lakini ameshindwa kazi yake.
Source:Mwananchi