Shekhe Ponda aachiwa huru

Shekhe Ponda aachiwa huru

Status
Not open for further replies.

zefounda

Member
Joined
Nov 26, 2012
Posts
97
Reaction score
19
Nimepata taarifa sasa hivi kuwa shehe Ponda kaachwa huru na mahakama. Naomba taarifa halisi wana jf.
===============================================
DSC_0085.JPG
Waumini wa dini ya Kiisilamu ambao walijitokeza kusikiliza hukumu ya kesi ya Sheikh Ponda Issa Ponda na wenzake 49, wakimbeba juu juu mmoja wa wafuasi wake ambao walishtakiwa pamoja mara baada ya kushinda kesi hiyo kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

HATIMAYE katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiisilamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda na wafuasiwake 49 leo wameachiliwa huru na mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kufuatia kushinda mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakibili.

Hata hivyo Sheikh Ponda amehukumiwa kifungo cha nnje mwaka mmoja kutokana na utetezi wake kuonyesha kulikuwa na nia yakutenda kosa hilo.


Mara baada ya kutolewa hukumu hiyomahakamani hapo pali ibuka shangwe za furaha kutoka kwa mamia ya wafuasi wake waliokuwa wamejazana karibu na eneo la Mahakama hiyo.

Pamoja na maelezo yote aliyoeleza Jaji aliyesoma hukumu hiyo alifafanua mambo mbalimbali kuhusu kiwanja kinachodaiwa na waisilamu hao.

1.Mahakama hiyo haina uwezo wakuzungumzia mmiliki halali wa kiwanja kutokana na masuala ya migogoro ya aridhi kuwa na mahakama yake ingawa imegundua kuna tatizo umiliki.

2.Upande wa Serikali hakuwa na hoja ya kisheria wala ushahidi wa kutosha wakuwatia hatiani watuhumiwa.

3. Hati ya Mashataka ilikuwa na mapungufu mengi ya kisheria.

4.Hakimu awaonyesha njia yakudai mali hiyo waisilamu kutokana na kile alichodai mali ya wakfu huwa haiuzwi wala haibadilishwi matumizi yaliyokusudiwa.

5.Upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha kwamba watuhumiwa waliopo mbele ya mahakama ni wafuasi wa sheikh Ponda. Awasihi Waisilamu kufuata taratibu za kisheria ili kuipata mali hiyo halali itumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa.
DSC_0072.JPG
Baada ya hukumu wafuasi wa sheikh Ponda wakitoka kwenye mahakama ya Kisutu.
DSC_0113.JPG
Polisi wakiwa wamejipanga kwa tahadhari kwa lolote litakalotokea.
DSC_0238.JPG

Askari wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu., ambapo leo yeye na wenzie 49 wameachiwa huru ila watatumikia kifungo cha nje cha mwaka mmoja. PICHA ZOTE NA KHAMIS MUSSA
DSC_0444.JPG
Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.
DSC_0489.JPG

Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
DSC_0502.JPG

Wafuasi wa Sheik Ponda wakimshangilia alipokuwa akihutubia ndani ya Msikiti wa Mtambani.
DSC_0548.JPG
Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam.
DSC_4990.JPG

Katibu wa Jumuia za Taasisi za Kiisalamu Tanznania, Sheikh Ponda Issa Ponda akifanya mahubiri katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam, alipokwenda leo baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, kumwachia huru jana, yeye na wenzake 49 waliokuwa wanakabiliwa na shitaka la uchochezi

Chanzo:Michuzi
 
Watakuwa wanapunguza wafungwa huko jela kwa ajili ya kina Prof. Muhongo na wenzie wanaodidimiza taifa kwa kuiba hela za masikini.
 
Nimeona maandamano ya watu kama 100 hivi Bara2 ya BIBI TITI ,Yaeleka kama wanashangilia kitu ila sijaelewa kwani wanaongea Kiarabu

Mkuu hata Mimi nimeyaona hayo maandamano hapa karibu na Ofisi za Zanzibar Insurance, mtaa wa Lumumba na Morogoro rd. Sijaelewa kwa nini wanaandamana
 
Kumbukeni aliyetuhumiwa kumuuwa Padri kule Zanzibar, wapi na wapi fundi seremala ambaye kazi yake ni kukereza mbao tu aweze kupata silaha na kumdungua Padri?!

Ilifunguliwa kesi na mwisho Serikali waliifuta wenyewe, hii nchi kama huijui na (hasa kwa nyinyi Wakristo) siku zote mutakua munalishwa maneno na kuamini kila muambiwacho!

Wakati tulipolewa kile kibonzo ambacho tuliambiwa walikichora FBI kwa kushirikiana na CIA Wakristo mulikua Munafurahia sana, lakini mwisho wa siku yakatokea yaliyotokea
 
kaachiwa huru na hakuna makosa aliyoyafanya na katangazwa kwamba ni ulamaa mkubwa wa kiislamu makosa aliyodaiwa kuyatenda yalikua ni ya uzushi tu! Serikali ya ccm ni mbaya sana
unalazimisha awe na makosa wakati hana
 
Takbiiiiiiiiiiiir mpiganaji, mwanaharakati SHEIKH PONDA ISSA PONDA rudi tuendeleze mapambano%
 
Anayefaa kupelekwa huko ni Askofu Kilaine kwa wizi wa fedha za watanzania masikini sio Sheikh Ponda ambaye hata kuiba penseli hajawahi

Kuna kokoto na vifaa vingine vya ujenzi viliibiwa, wakati Sheikh Ponda na maninja wenzake walipovamia na kuteka viwanja vya markazi pale chang'ombe.Tafadhali tuweke rekodi sawa.
 
Mungu mkubwa sana.
Walitaka kumuonea Shehe Ponda Lkn Haki Imeonekana.
Mara ooo Gaidi mara ohhh analeta machafuko Nchini.

Wanajaribu kuyalinda majambazi na Kuwakamata Waungwana.

Haki na Batil huwa haziendi pamoja.

Cc picchu
 
Last edited by a moderator:
Shekhe Ponda aliiba nondo nakokoto. Kama ameachiwa kila ijuma kazi ni moja kukimbizana na maandamano.
 
Mungu mkubwa sana.
Walitaka kumuonea Shehe Ponda Lkn Haki Imeonekana.
Mara ooo Gaidi mara ohhh analeta machafuko Nchini.

Wanajaribu kuyalinda majambazi na Kuwakamata Waungwana.

Haki na Batil huwa haziendi pamoja.

Cc picchu

Walimuonea sana, Mungu ampe afya njema
 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom