Shein: Zanzibar itakuwa kama Dubai

Shein: Zanzibar itakuwa kama Dubai

MpigaFilimbi

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2008
Posts
1,169
Reaction score
188
Shein+PHOTO.jpg

Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein



Zanzibar. Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk Ali Mohamed Shein amesema akichaguliwa atavifanya visiwa hivyo kuwa mji wa kisasa wenye hoteli za nyota tano, viwanda na uwanja wa kimataifa wa mpira.

Akihutubia mamia ya wafuasi wa chama hicho kwenye mkutano wake wa 25 wa kampeni za uchaguzi uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Mkoa wa Mjini Magharibi, Dk Shein alisema Zanzibar itafanana na miji mikubwa duniani kama Dubai.

Alisema tayari kuna eneo maalumu kwa ajili ya ujenzi huo ambalo limeshatengwa katika eneo la Fumba na kwamba kiwanda cha kisasa za kuzalisha maziwa cha Azam kimeshaanza kazi.

Alisema katika eneo hilo, pia utajengwa uwanja wa mpira wa kimataifa utakaokuwa na uwezo wa kuchukua watu 45,000.

"Mji wa Fumba utakuwa eneo huru la uwekezaji, yatajengwa majengo yenye zaidi ya ghorofa 20 kwa ajili ya makazi na wanaofanya kazi hii ni wawekezaji kwa kushirikiana na Serikali.

"Mradi huo utasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Wazanzibari, wasikudanganyeni wapinzani kwa ahadi hewa, ninachokisema ni mipango ya Serikali inatolewa na rais wengine waongo," alisema.

Alisema Serikali inaingia makubaliano kampuni mbalimbali nchi kuhusiana na miradi hiyo akawataka wananchi wamchague ili aiendeleze.
Akiuzungumzia Mji Mkongwe, alisema Serikali itaendelea kuwatumia wawekezaji kwa ajili ya kuyafanyia ukarabati majengo ya Mji Mkongwe ili yaweze kuendeleza historia na kuingizia mapato kupitia utalii.

"Tutalinda historia ya Zanzibar kwa kuboresha majengo ya Mji Mkongwe bila kuathiri mwonekano wake ili kuboresha sekta ya utalii," alisema.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Balozi Seif Ali Iddi alisema maendeleo yaliyopatikana Zanzibar yameletwa na CCM hivyo akawataka wananchi kukichagua chama hicho ili kuendeleza mambo yaliyobaki. Kwa upande wake, Katibu wa Oganaizesheni ya CCM Taifa, Dk Mohamed Seif Khatib aliwataka wananchi waipe kura CCM ili iweze kudumisha Muungano.

Alisema kamwe Wazanzibar wasifanye uchaguzi huu kwa majaribio, bali wakichague chama chenye rekodi ya kudumisha amani na mshikamano.

Chanzo: Mwananchi


Sasa anayeahidi ni Shein, huyu ambaye ni Rais wa sasa wa Zanzibar, kama wapiga kura wa Zanzibar wana akili timamu inabidi apate kura za familia yake na watu wa Kisiwandui pekee.
 
Mkuu, hizo ni ahadi za Magufuli

Kaamua kupiga mgombea binafsi, basi anapiga sound kuliko JK

Kila kona anaahidi
 
kauli hii iisemwa tangu enzi za salmini, mpaka leo iko vile vile
 
Mkuu, hizo ni ahadi za Magufuli

Kaamua kupiga mgombea binafsi, basi anapiga sound kuliko JK

Kila kona anaahidi

yaani, hizo ahadi ndio nafikiria pesa itapatikana wapi, manake zishavuka mia na zote ni pesa nene
 
yaani, hizo ahadi ndio nafikiria pesa itapatikana wapi, manake zishavuka mia na zote ni pesa nene

Magufuli atatandika lami DAR hadi Zanzibar na ashapata mkandarasi wa hili daraja MPENI TU KURA ZENU
ImageUploadedByJamiiForums1445402398.688879.jpg
NA OLE WAKE WAZIRI ATAKAYEKUWA WA UJENZI ASHINDWE HII KAZI!
 
kwanini mtu unasema vitu kama uko usingizini? kwani huyo Dubai ilijengwa kwa miaka mi5? asiahidi kitu asichoweza kukifanya............
 
Ahadi za ccm nikama vile uchawi uchawi tu, sasa mtu ulikuwa madarakani na bado upo madarakani, muda wote umeshindwa kufanya hayo mpaka uje useme mkinichagua nitafanya hivi na hivi ? kwanini usingeyafanya kabla alafu ukasema mliponichagua nilifanya haya na haya, sasa nichagueni nifanye makubwa zaidi ya haya. tosha kabisa bila kutoa ahadi mpya yoyote na unaendeleza utawala kiulaiiini tu.
Ukiona chama tawala kinatoa ahadi nyingi ujue kinaogopa kutoswa, kinatumia ahadi kama hongo, mnichague kwanza ndo niwafanyie hiki na hiki.
 
Back
Top Bottom