Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,498
IMAMU wa Msikiti wa Masjid Noor uliopo chini ya BAKWATA Bariadi, Mkoani Simiyu, Sheikh Yakubu Saburia, ameeleza kuwa amani ya nchi haipaswi kuhubiriwa kwa misingi ya itikadi za kisiasa au vyama, bali kama tunu ya kitaifa inayopaswa kulindwa na kila mmoja.
Akizungumza wakati wa swala ya Eidi-al-Adh-ha, Sheikh Saburia amesema Tanzania ina amani, lakini baadhi ya matamshi na mienendo ya kisiasa vinaashiria kutokuwa na dhamira ya kuitunza.
"Sisi tunayo amani, lakini tunaona kwamba haitoshi. Tunaona tunaanza kuichezea hii amani tuliyonayo, kama vile tunataka tufike mahali pa kukimbizana kama ambavyo wanakimbizana mataifa mengine," amesema Sheikh Saburia.