Sheikh Yahya: Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya: Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by OgwaluMapesa, Sep 16, 2010.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  LICHA ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake kumkana, Mnajimu maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, ameibuka na kusema kwamba hahitaji kibali katika kumwekea "ulinzi wa majini" mtu anayempenda - Rais Jakaya Kikwete.

  Akizungumzia kauli za viongozi wa CCM na Serikali kwamba hawatambui "ulinzi wa majini" aliosema atautoa kwa Kikwete, Sheikh Yahya, amesema: "Sihitaji kibali cha yeyote kumuwekea rais wangu ulinzi wa majini."

  Sheikh Yahya, ambaye amekuwa akitoa kauli tata kuhusiana na Kikwete hata kabla ya kampeni kuanza, alisema, jana, jijini, kuwa anachozungumzia yeye si uchawi wala ushirikina; bali ni mambo ambayo yapo na hayakwepeki.

  "Kila mtu anazaliwa na jini. Hata Slaa (Dk.Willibrod Slaa, Mgombea urais wa CHADEMA) ana jini anaitwa Subiani. Nakwambia sihitaji kumshirikisha mtu katika hili," alisema Sheikh Yahya Hussein na kumkabidhi simu mwanae aliyejitambulisha kwa jina la Hassan, ambaye naye alisema;

  "Sheikh alisema binafsi hahitaji kumshirikisha mtu katika hili. Serikali iendelee na ulinzi wake na yeye atatoa ulinzi wake. Mbona hao walinzi walikuwapo lakini akaanguka? Matatizo yale si ya kiafya. Sheikh anafanya kwa kuwa anampenda na hutasikia tena anaanguka."

  Awali Sheikh Yahya alinukuliwa katika taarifa yake akisema kwamba atatoa ulinzi usioonekana kwa macho kumkinga Rais Kikwete ili mtu yeyote asijaribu kumfanyia ‘mchezo' wowote kama ilivyotokea Jangwani.

  Sheikh Yahya alisema katika taarifa hiyo ya kuwa amefikia hatua hiyo kutokana na uchungu alionao kwa nchi na kwa Rais Kikwete anayempenda.


  Kufuatia kauli hiyo, Dk. Slaa alikemea kauli hiyo na kusema: "Nchi haiwezi kuongozwa na uchawi. Haiongozwi na imani za watu, kila mtu ana imani yake, lakini tusifike mahali tukaongoza nchi kwa uchawi."


  Alimtaka Rais Jakaya Kikwete kumkemea Sheikh Yahya kwa kauli hiyo iliyotolewa juzi Dar es Salaam, la sivyo wananchi wataamini mnajimu huyo anatumiwa na CCM kuleta hofu katika jamii.


  Dk. Slaa aliwakumbusha wananchi kuwa mwanzoni mwa mwaka huu, Sheikh Yahya alisema mtu yeyote atakayegombea urais na Kikwete atakufa na kuongeza: "Sisi wengine ni majabali, hatuogopi kufa kwa ushirikina."


  Tayari serikali imesema haihusiki na hoja ya ‘ulinzi' usioonekana kwa Rais Kikwete, kama ilivyotangazwa na Sheikh Yahaya.

  Hata hivyo, Sheikh Yahya alisema hakuwa anazungumzia uchawi wala nguvu za giza, "bali majini ambao ni viumbe kama sisi, isipokuwa wao wameumbwa kwa moto na sisi tumeumbwa kwa udongo na wametajwa katika vitabu vyote vitakatifu vya Waisalamu na Wakristo na Mwenyezi Mungu amesema tushirikiane nao".

  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kampeni za CCM, Abdulrahman Kinana, alisema Rais Kikwete ni muumini wa Dini ya Kiislamu, ambaye anaamini Mungu na hivyo hahusiki kwa vyovyote na kauli ya Sheikh Yahya.


  Kauli hiyo ya Sheikh Yahya imeibua mjadala mkali; huku baadhi ya wananchi wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike kuangalia kama kuna fedha za umma zinazotumika kugharamia masuala ya ushirikina.

  Baadhi ya wananachi hao, wakiwamo viongozi wa dini, wamekemea tabia ya baadhi ya viongozi kukimbilia katika imani za ushirikina baadhi wakitumia raslimali za umma katika kugharamia imani hizo.

  Rais Kikwete amepata kuanguka hadharani mara tatu; mara ya mwisho ikiwa ni wakati akizindua kampeni yake ya urais, hivi karibuni, katika viwanja vya Jangwani, Dar es Salaam.

  Alipata pia kukiri hadharani kwamba alimsaidia Sheikh Yahya fedha za kwenda matibabuni nje ya nchi.

  [​IMG]
   
 2. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,676
  Trophy Points: 280
  Sheikh Yahya ni mshirikina, na Kikwete pia ni mshirikina, ndiyo maana yeye mwenyewe JK anajua huduma anayoipata toka kwa huyo gagula, na malipo ameshatoa kwa kumpeleka GAGULA huyo India kwa matibabu. La msingi ni kwa wote wenye kumuabudu Mungu wa kweli kumpinga JK kwa nguvu zooote asirudi tena pale ikulu. KWA KUWEPO ULINZI WA MAJINI IKULU NCHI YOOOTE INAPOKEA LAAANA.
   
 3. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 21,997
  Trophy Points: 280
  CCM NA UCHAWI NI NDUGU MMOJA:cheer2:
   
 4. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,470
  Likes Received: 1,211
  Trophy Points: 280
  wazandiki
   
 5. s

  small Member

  #5
  Sep 16, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  huu ni uchimvi Mungu pekee ndio anayelinda mwanadamu
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Yahaya anataka tuamini kuwa Mungu alisema tushirkiane na SHEITWANI ktk kumtumikia na kumcha Yeye Mungu.
  Siamini kama Watanzania bado ni misukule wa kudanganywa hivi
   
 7. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #7
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na ufisadi!
   
 8. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sheikh Yahya:Naendelea kutoa 'ulinzi' kwa Kikwete

  Mwandishi Wetu​
  Septemba 15, 2010

  [​IMG]Asema hahitaji ruksa ya CCM, serikali
   
 9. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kazi kweli kweli
   
 10. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Hii imenimaliza mbavu kabisaaaa

   
 11. KING COBRA

  KING COBRA JF-Expert Member

  #11
  Mar 22, 2014
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 2,783
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145


  [FONT=&amp]IKULU: MAONI YA SHEIKH YAHYA YAHESHIMIWE[/FONT]
  [FONT=&amp]25/12/2009 [/FONT]
  SIKU moja baada ya mnajimu maarufu, Sheikh Yahya Hussein kujitokeza na kuwatangazia vifo vya ghafla wanasiasa watakaojitokeza kukabiliana na Rais Jakaya Kikwete kwenye uchaguzi mkuu ujao, Ofisi ya Rais Ikulu imetaka maoni ya mnajimu huyo kuheshimiwa.
  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu, alisema maoni ya Sheikh Yahya ni sawa na ya watu wengine, hivyo yanastahili kuheshimiwa.
  Rweyemamu alisema kwa kuwa maoni hayo ni ya mtu binafsi, hivyo Rais Kikwete hapaswi kuingizwa kwa namna yoyote ile.
  "Sheikh Yahya ametoa maoni yake kama ninyi mnavyotoa maoni yenu ambayo si watu wote wanakubaliana nayo. Naomba maoni yake yaheshimiwe na tusimwingize rais katika maoni ya mtu binafsi.
  "Mwacheni rais apumzike kwa Sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. Haya ni mawazo ya mtu binafsi," alisema mkurugenzi huyo.
  Wakati Ikulu ikitoa majibu hayo, Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM) ambaye ameonyesha nia ya kuwania urais mwakani, ameonyesha kutotetereka katika dhamira yake hiyo na kubeza kauli hiyo ya Sheikh Yahya.
  Katika kudhihirisha hilo, amesema yeye anamwamini Mwenyezi Mungu na kwamba jambo lolote linalomtokea mwanadamu limepangwa na Mungu.
  "Wahenga wanasema paka na panya hawapangi chumba kimoja, muumini wa Mwenyezi Mungu si wa shetani. Mimi siamini katika nguvu za giza," alisema.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana, alisema kama Sheikh Yahya ni bingwa wa utabiri ajitabirie kifo chake, ili aweze kuandaliwa mazishi ya heshima.
  "Uongozi unaotoka kwa shetani huwa wa nguvu za giza na shangwe za nyimbo za mizimu ya maruhani na wachawi. Je, sasa kuna maruhani mpaka tuamini hilo?" alihoji Shibuda.
  Pia alimtaka sheikh huyo kueleza kuwa yupo katika kambi ya malaika ya Mwenyezi Mungu ama kambi ya dhuluma ya wachawi kwa kutoa roho za watu.
  Katika hilo, Shibuda alisema Sheikh Yahya anatangaza zabuni ya kutafuta hela ya kuwakinga watu kwa nguvu za giza.
  "Atakalo Mola ndilo linalomfika mwanadamu. Mimi siamini nguvu za giza, namuamini Mwenyemizi Mungu kwani nitaongoza maslahi ya Watanzania wa Mwenyezi Mungu," alisema.
  Hata hivyo, alisema sheikh huyo hana upatu na utashi wa Mwenyezi Mungu na kusema kwamba aliugua na kwenda kutibiwa nchini India huku akisaidiwa na Rais Kikwete. "Kama mtabiri mahiri, angejitabiria ugonjwa uliofanya apelekwe India, asiogope, nikiwa rais nitamsaidia matibabu.
  "Sasa nakupa msemo wa Kipemba, ‘machozi ya vivyo hupatikana vivyo'. Aache kuwaza urais Tanzania unapatikana kwa nguvu za giza. Hatuhitaji rais anayepatikana kwa nguvu za giza kwani haji kuongoza maruhani na mashetani," alisema Shibuda.
  Aidha, alisema CCM si hekalu la maruhani na nguvu za giza na kumuomba Mwenyezi Mungu awaepusha na majaribu hayo.
  Pamoja na mambo mengine, Shibuda alisema kuwa anaichukulia kauli ya Sheikh Yahya kama majaribu yaliyowahi kuwapata manabii na mitume wa Mwenyezi Mungu.
  Kwa upande wake, Askofu Mkuu wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, Zachary Kakobe, amelaani utabiri huo na kuwataka wananchi kuupuuza kwa kuwa nchi inaongozwa kwa katiba na sheria.
  Alisema wananchi hawatakiwi kuongozwa kwa unajimu, kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu za Mungu.
  "Nchi hii haiongozwi kwa nyota wala unajimu, kitendo cha kukubali unajimu huo uliotolewa ni sawa na kukaribisha ushirikina ndani ya nchi yetu," alisema Kakobe.
  Alisisitiza kuwa yapo mataifa mengi yamekuwa yakipinga kazi za Mungu waziwazi, lakini hakuna hata moja ambalo limeangamizwa.

  "Ukiangalia leo vitendo vinavyotendeka ni kinyume kabisa na taratibu za ki-Mungu, lakini hakuna hata mmoja anayekufa, iweje ajitokeze mtu na kuupotosha umma kwa sababu ya kumpinga binadamu mwenzako?" alihoji Kakobe.
  Aidha, alisema wanaohitaji kugombea nafasi hiyo wajitokeze kwa wingi, kwani hakuna hata mmoja atakayekufa kutokana na kumpinga Kikwete.
  Aliongeza kuwa kutokana na kauli hiyo inaonyesha mnajimu huyo anataka kuwarudisha watu katika kipindi cha zama za ujima ambapo walikuwa wakiishi kwa hofu.
  Kakobe alisema hata katika kitabu cha maandiko matakatifu (Biblia) inaelezwa kuwa yupo mpinga Kristo ambaye anapingana na kazi za Mungu, lakini haijaelezwa kuwa atakufa, hivyo alilaami kauli ya mnajimu huyo.
  Nao baadhi ya wananchi waliotoa maoni yao wameonyesha masikitiko na kueleza kuwa hizo ni njama
  za CCM za kutaka kuwanyima watu fursa katika kugombea nafasi hiyo.
  "Haiingii akilini hata kidogo eti mnajimu wa nyota akasimama na kumtabiria kifo mtu atakayejitokeza kumpinga Kikwete, hapa inaonyesha CCM walivyoamua kumtumia mnajimu huyo ili kuwapa hofu wanaohitaji fursa hiyo," alisema mwananchi mmoja.
  Hata hivyo, mwananchi huyo ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alisema hakuna mwanadamu ambaye anaishi milele chini ya jua, hivyo kauli hiyo ni propaganda iliyopitwa na wakati ya kutaka kuwanyamazisha watu wasiwanie nafasi ya urais ndani ya CCM.
  Mwananchi mwingine, Maryrose Nungu, alisema utabiri si kitu cha kuaminika na kwamba kuwatishia kifo baadhi ya watu ni kosa la jinai.
  Alisema kuchaguliwa ni haki ya kila raia, lakini kifo ni fumbo la Mungu, hivyo si sawa kwa mnajimu huyo kutangaza kifo kwa mtu anayetaka kutimiza haki yake ya kikatiba.
  "Unajua huyu sheikh anaweza kushitakiwa kwa sababu kutangaza kifo hadharani ni kosa la jinai…haiwezekani kila mmoja kati ya watu milioni 40 wote wasitimize haki yao ya kikatiba.
  "Anatakiwa kuwaacha watu wagombee, kifo ni fumbo na yeyote atakayekufa kama alivyosema, Sheikh Yahya anastahili kufunguliwa mashtaka," alisisitiza mkazi huyo wa Dar es Salaam aliyejitambulisha kama mwanaharakati.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Tanzania Labour (TLP), Augustine Mrema, amewashauri wanasiasa kutoupuuza utabiri wa Sheikh Yahya kwa maelezo kuwa mara kadhaa anayoyatabiri hutokea.
  Mrema ambaye hivi karibuni amekaririwa na vyombo vya habari akimpongeza Kikwete kwa utawala wake unaojitahidi kupambana na ufisadi, alisema ni heri wanasiasa wenye nia ya kupambana na Kikwete kutafuta kazi mbadala kwa kipindi hiki.

  "Mimi nawashauri waache kiherehere. Hebu angalia nimeona pagumu ndio maana nimeacha urais sasa natarajia ubunge wa Vunjo…yasije yakawatokea, ni heri wapumzike kwanza Kikwete amalize muda wake ndio warudi ulingoni.
  "Yahya amewahi kutabiri mambo kadhaa na yametokea, ni bora watafute kazi nyingine mbadala wasije juta baadaye," alisema Mrema aliyewahi kugombea urais kwa awamu tatu bila mafanikio.
  Naye Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni John Chiligati alisema hawawezi kuiingilia utabiri huo na kusisitiza kuwa suala hilo wanamuachia mnajimu na wananchi.
  Alisema CCM haiwezi kwenda kumchomekea mtabiri, ili kuwatisha wanaotaka nafasi ya urais, bali kazi ya chama hicho ni kushughulika na masuala muhimu hasa kutekeleza ilani yake.
  "CCM haiwezi kumtumia mtabiri fulani achomekee mambo mazuri, karata yetu kubwa ni kutekeleza ilani ya chama ambayo ni kujenga barabara, vyuo vikuu, shule kuhakikisha maji yanapatikana na huduma zote za kijamii," alisema Chiligati.
  Jana, Sheikh Yahya alikaririwa akisema kuna kila dalili za ushindi mwingine wa kishindo kwa Kikwete utakaomfanya aendelee kutawala kwa miaka mitano ijayo.
  Pia mtabiri huyo, alisema baada ya Kikwete kuingia madarakani atamteua mpinzani kushika wadhifa wa uwaziri mkuu.
  Mbali na hilo, mtabiri huyo alisema kwa upande wa Zanzibar Chama cha Wananchi (CUF) kitashinda katika uchaguzi huo wa mwaka 2010.
   
 12. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2015
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Majini pado yapo ikulu???
   
 13. M

  Masunga Maziku JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2015
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 4,040
  Likes Received: 1,999
  Trophy Points: 280
  ndio maana hatuendelei kama viongozi wetu wanalindwa na majini..
   
 14. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2015
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,872
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  bakwata njoeni huku. "mwisho wa utawala wa majini ni 2015" mtume mwingira
   
 15. m

  markj JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2015
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  90% ya walio comment humu kama si 100% ni washirikina kwenye shuguli zao au majumbani mwao.. mdomo tu ndo unatusumbua wabongo
   
 16. CHAMVIGA

  CHAMVIGA JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2015
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 7,694
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Yahaya alikua mshirikina kama alivyo kakobe.
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2015
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,872
  Likes Received: 1,560
  Trophy Points: 280
  bingwa wa koroan unamwita mshirikina?
   
 18. BAOBAO

  BAOBAO JF-Expert Member

  #18
  Jan 8, 2015
  Joined: Oct 12, 2012
  Messages: 1,766
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  ask. Kakobe alivunja uchawi wako mkuu ??
   
Loading...