Sheikh Yahya: Mengi kuingia kwenye siasa, Kikwete Kushinda kwa Kishindo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh Yahya: Mengi kuingia kwenye siasa, Kikwete Kushinda kwa Kishindo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Invisible, Jan 8, 2009.

 1. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #1
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mnajimu maarufu wa Tanzania leo ametabiri kuwa mwaka 2009 utakuwa mwaka mgumu kiuchumi (mwaka wa matatizo); pia akadai kuwa mwaka 2010 uchaguzi hautakuwa na kuibiwa kwa kura kama chaguzi zilizopita.

  The most interesting thing ni kuwa alibashiri kuwa mfanyabiashara mkubwa nchini kwa jina la Reginald Mengi ataingia kwenye siasa kabla ya 2011!

  Je ubashiri wake utakuwa sahihi?
   
 2. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #2
  Jan 8, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ubashiri wa credit crunch angeufanya miaka miwili iliyopita sasa hivi hata mimi ningemfata nijue mshindi wa ubunge kwa jimbo la Kawe na Kinondoni mwaka 2010!!
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Sheikh Yahya acha virungu vyako! na kutafuta biashara iliyokukimbia

  Kikwete kushinda kwa kishindo 2010'
  Gloria Tesha
  Daily News; Thursday,January 08, 2009 @21:15​

  Mtabiri maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein, amemtabiria ushindi wa kishindo Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi mkuu mwakani na kwamba Serikali yake itakuwa ya Muungano wa Vyama vya Siasa.

  Sheikh Yahya amesema pia ushindi wa Kikwete utatokana na mwendelezo wake wa kufichua mafisadi na kuwafikisha katika vyombo vya sheria bila woga na kwamba katika uchaguzi huo, hakutakuwa na wizi wa kura, bali watu watashughulikia kutafuta fedha na mtandao wa mafuta.

  Mtabiri huyo alisema hayo jana, Dar es Salaam wakati akitoa taarifa ya utabiri wake kwa mwaka huu kwa waandishi wa habari. Kuhusu ushindi wa Kikwete na hali ya kisiasa kuelekea mwaka wa uchaguzi, alisema utabiri wa mwaka huu uliopewa baraka zote na Umoja wa Mataifa, kuwa mwaka wa kuongozwa na nyota duniani, unaonyesha kuwa kiongozi mwenye jina lenye herufi J na K nchini, ndiye anayeongoza nchi.

  "Pamoja na kuwa na herufi hizo, pia mwenye bahati kuwa katika uongozi wa awamu ya pili, ya tatu na sasa ya nne, awe mwenye kichwa cha bapa, uso wa meza na rangi ya maji ya kunde … mwenye nyota hiyo ni Kikwete na hivyo namtabiria kuendelea kuongoza nchi 2010," alisema Sheikh Yahya.

  Alisema pamoja na kuwa na nyota hiyo inayoonyesha ushindi, endapo ataacha kuwatetea wanyonge kwa kupingana na baadhi ya matakwa ya watu wa chama chake, atashindwa vibaya katika uchaguzi na akakionya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuacha kiburi na kutambua kuwa hakitaongoza nchi peke yake mwaka huo.

  Akifafanua kuhusu Serikali ya Muungano wa Vyama, alisema dalili zilizopo zinaonyesha Serikali ya Mseto na kuzitaja dalili hizo kuwa ni kampeni za kinyang'anyiro cha ubunge Mbeya Vijijini, ambako vyama vya Upinzani vinaangushana na kuiunga mkono CCM.

  Hata hivyo, alisisitiza kuwa hakutakuwa na wizi wa kura katika uchaguzi ujao na badala yake itaundwa Serikali ya Mseto na kwamba viongozi wakiwamo wabunge walioko madarakani watakaoendelea kufanya ufisadi na kutotenda haki kwa wanyonge, watashindwa vibaya katika uchaguzi huo.

  "Mwaka huu vifo vya watu mashuhuri vitaongezeka sana na kutakuwa na kukwama kwa viongozi wapenda rushwa na wale watakaosema ukweli bungeni bila kuficha kitu, watachanua katika uongozi na maisha kifedha," alisema.

  Sheikh huyo alimzungumzia pia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi, kuwa atajiunga na siasa mwakani na pia mgogoro wake na Waziri wa Mambo ya Ndani, Lawrence Masha, hauwezi kuendelea kwa kuwa herufi za majina yao ya pili ni M zikifuatiwa na herufi E na A ambazo kinajimu ni ndugu wa baba mmoja. Pia Mnajimu huyo alimtabiria Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuwa kati ya sasa na Aprili mwaka huu, atapata kazi kubwa duniani ambayo itaiacha dunia ikishangaa, hasa Watanzania.
   
 4. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #4
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Mkuu,

  Iwapo Shekh alitaja kabisa jina la Rginald Mengi hii itakuwa historia kwani mara nyingi huwa hataji jina. Shekh angesema kitu kama mfanyabisha maarufu, mwenye kipara kidogo, aliyetokea mkoa uliopo Kaskazini n.k Lakini kama ametaja jina basi tujua kwamba this round it will happen for sure..!!! lol
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Mkuu YY,

  Huwa SINA imani kabisa na ubashiri, siamini kama ubashiri wa Sheikh ni sahihi mpaka niyaone haya. From then nitamwamini.

  Kuhusu suala la JK kuchukua nchi kiulaini sina wasiwasi sana na hilo litawezekana ENDAPO wapinzani (vyama vya Upinzani) watabakia kama tunavyowaona.

  Kuhusu Mkapa I doubt amechemka, huenda yuko sahihi lakini binafsi siamini kuna jukumu KUBWA kwa kiwango hicho... Labda awe Katibu mkuu wa UN!

  Let's wait n see
   
 6. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #6
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  LoL,

  Hili Jimbo inaelekea wengi tunalisarandia... Wakuu tupeane mikakati kwenye PM tusije haribiana bure, nitajitolea kumpigia kampeni yeyote from JF :)
   
 7. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Mwezi wa nne sio mbali...
   
 8. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Huyu mganga wa kienyeji nae aacha kuwadanga Watanzania. Imani za kipumbavu kama hizi ndio zinaendelezwa na vyombo vya habari na mwishowe tunakuta Maalbino wanauwa kwa upuuzi kama huu. Huu ni utabiri gani .. eti watu mashuhuri watakufa.. hali ya uchumi itakuwa mbaya.. mbona haya mambo hayahitaji hata utabiri? Huyu ni tapeli anayeganga mlo wake wa kila siku na hakuna cha utabiri wala nini... upuuzi mtupu...
   
 9. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #9
  Jan 8, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Sheikh ni mjanja sana , hakuna utabiri pale ni kuona alama za nyakati na ku-extrapolate.
  1. Uchumi-nani asiyejua kuwa dunia nzima ina matatizo, watu Ulaya tena matajiri,wanajiua kutokana na matatizo hayo!
  2. JK atashinda tu na hii ni baada ya kutegua wingu zito la mafisadi, JK hapo kacheza chess, vinginevyo in-action juu ya
  suala hili lingempa matatizo makubwa kisiasa.
  3. Viongozi mashuhuri kufa-cheki line up ya viongozi kiumri, wengi ni wazee,na mkumbuke wadau kuna sakata la ukimwi,
  Mwaka huu tu tumepoteza watu wengi.
  4. Mengi kuingia kwenye siasa - tayari huyu jamaa yuko mstari wa mbele katika siasa, ameform pressure groups za
  kushinikiza serikali(cif MOAT).Tatizo waTanzania wengi wanafikiri siasa ni kuwa bungeni tu.
  Wadau naomba kutoa hoja.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,754
  Likes Received: 82,732
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kamba zake kuhusu mgogoro wa Mengi na Masha si umeziona. Mengi kishatamka hadharani kwamba kamsemehe Masha kwa kuwa hajui asemalo sasa hapo mgogoro utaendeleaje!!!!?....LOL! Haihitaji kuwa Sheikh Yahya ili kulijua hilo.
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Halafu ubashiri huu kajifunga kwelikweli; yani kayaweka bayana kabisa.

  Aprili si mbali kama alivyotanabaisha Kibs, let's wait n see
   
 12. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #12
  Jan 8, 2009
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  ...mwezi wa tano ukiingia atakuambieni mambo ya probability!!
   
 13. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #13
  Jan 8, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,349
  Trophy Points: 280
  Wakuu kwani hamkumbuki mara Kikwete aliposhika madaraka "alitabiri" eti kutakuwa na kuundwa kwa serikali ya mseto??? Iko wapi hiyo serikali???
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Jan 8, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,091
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 160
  Macho umenivunja mbavu,

  Anyway, ngoja kwanza niende karakana kisha nitarejea na JF mpya kiasi :)
   
 15. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #15
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Shehe (Mzee) Yahya acha uongo na upotovu....
   
 16. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #16
  Jan 9, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Ndio uzuri wa JF, huwa sio rahisi kumaliza kuhesabu vichwa, huyu Sheikh Yahaya, amepitwa na wakati, na sijui amewahi kulifanyia nini hasa taifa letu on the positives na hizi nyepesi zake?

  - Ingawa mnyonge mnyongeni, ninakumbuka zamani sana nikiwa mdogo kwenye banda lake uwanja wa maonyesho ya Saba saba alikuwa ni mbongo wa kwanza kuweza kuonyesha TV/Video hadharani, alitupata sana na video za Orch. Mangelepa na Super Mazembe, katika uwanja mzima ni kwenye banda lake tu na banda la West Germany ( ambako kulikuwa na video ya mipira ya World Cup, ya the then Zaire ikila magoli 11 na Yugoslavia), ndio kulikuwa na video show, ninamkumbuka sana for this,

  Lakini otherwise, ya utabiri ni waste of time kumsikiliza ingawa pia hamlazimishi mtu kumsikiliza, lakini miaka mingi niliyowahi kuishi majuu sikuwahi kumsikia mzungu mtabiri maarufu kama yeye, ila nimewasikia kina Edison waliovumbua umeme.
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Sheikh Yahya Hussein:

  Kuna tabiri ambazo naweza kumpa credit.

  (a) Mwishoni mwa mwaka 2002 alisema kuwa Saadam Huessin atatolewa madarakani kwa nguvu mwezi Machi mwaka 2003. Ni kweli ilitokea hivyo

  (b) Mwaka huo huo alisema kuwa kungetokea ajali ya chombo kikubwa sana cha anga; ni kweli Space Shuttle Columbia ilipasukia angani mwezi Januari mwaka huo wa 2003.


  Lakini tabiri zake nyingi hazina ukweli.

  (a) Wakati anasem Saddam atatolewa madarakani, alisema pia kuwa Osama bin Laden angeshikwa, kufariki au kuuwawa; lakini Bin Laden amekuwa anatoa kanda zake kila kukicha.

  (b) Alisema kuwa rais wa Tanzania baada ya Mkapa angekuwa mwanamke. Sielewi kama huyu Kikwete (ambaye huko mitaani akina mama hawapumui) kweli ni mwanamke,

  (c) Nadhani mwaka 1973 au 74 hivi alitabiri kuwa timu ya Yanga ingekuwa bingwa lakini ubingwa huo ulichukuliwa na Simba (au kinyume chake)
   
 18. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 9, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu bwana ni muongo na anawadanganya wanaoamini uchafu wake, kama anajua ya mbeleni, siku anakamatwa na polisi wakati ule wa tafrani ya bucha za nguruwe, angelijua kuwa polisi wanakuja na kulala mbele mapema.
   
 19. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #19
  Jan 9, 2009
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Nathani alikuwa wa kwanza pia kumiliki Range Rover ya Milango sita yenye TV ndani...!!!
   
 20. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #20
  Jan 9, 2009
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa alisema 2005 raisi lazima awe mwanamke. Ilipotokea JK akasema yeah utabiri umetimia si mnaona wenyewe JK ana haiba ya kike!!!!!!!!!
   
Loading...