Sheikh yahya awaonyesha njia watoto wa babu seya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh yahya awaonyesha njia watoto wa babu seya

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by eRRy, Feb 24, 2010.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Sheikh Yahya (aliyeketi katikati) akiwakabidhi Francis (kulia) na Mbangu kitita cha 100,000/= muda mfupi baada ya kuwasili nyumbani kwake.​


  Akizungumzia utabiri wake dhidi ya hukumu iliyotolewa hivi karibuni katika Mahakama ya Rufani jijini Dar es Salaam, Shekh Yahya alisema, alijua wazi kwamba tatizo hilo lingetokea lakini alidai kuwa lilitokana na sababu za kimila (za akina Babu Seya).

  Alisema, anachokiona yeye ni upuuzwaji wa matambiko, kisomo au dua za kikwao, zilizotakiwa kufanywa na Babu Seya zamani, ndiyo matokeo ya mateso wanayoyapata hivi sasa huko gerezani.

  Alitawaka watoto hao kutafakari kwanza maisha ya gerezani huku wakiziacha akili zao zitulie, kabla ya kuingia katika hatua ya pili ya kuhangaikia baba na ndugu yao watoke gerezani.

  Alisema, baba yao anatoka katika ukoo wa kifalme ambao hutumia jina la Mbangu, lakini kuna mambo muhimu kufuatana na familia na mila za Kabila lao, ambayo mzee wao (Babu Seya) alitakiwa kuyakamilisha zamani, lakini hakufanya hivyo.

  “Hakuna mbaya wa tatizo hili, kuna mambo ambayo mzee wenu aliyapuuza katika ukoo wenu, kwahiyo jambo kubwa kwenu kwasasa ni kumuombea na siyo kumuombea yeye tu bali ni kujiombea wote pamoja.
  “Mnapaswa kumfanyia sadaka, msome kisomo kabla hajatoka, kwa mila za kwenu. Msije mkasema labda tatizo ni dansi, maana kama ni dansi mmeanza kuimba miaka mingi kabla, ila tatizo ni hilo la kusahau au kupuuza mila.

  “Nimefurahi kuwaona, pumzikeni kwanza, halafu siku zijazo nitawaita na kuwaelekeza vizuri juu ya jambo hilo,” alisema Shekh Yahya.
  Aidha mtabiri huyo aliwapatia vijana hao fedha kiasi cha shilingi laki moja kwa ajili ya kuwasaidia katika mahitaji yao.
  Juni 25, 2004, Babu Seya na wanaye, walihukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kukutwa na hatia ya kuwaingilia kimwili watoto wadogo kumi.
   
 2. RayB

  RayB JF-Expert Member

  #2
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 27, 2009
  Messages: 2,754
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Atawachanganya tu vijana wa watu huyu mzee
   
 3. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  ina maana Shekhe Yahya anathibitisha Babu Seya hawana hatia???????????????
   
 4. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #4
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=axj2tvrENbs"]http://www.youtube.com/watch?v=axj2tvrENbs[/ame]
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Feb 24, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  anawasaidia hao vijana kisaikolojia watulie...........................
   
 6. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Wizi mtupu.anazidi kuwaongezea majini ya kuwachanganya zaidi.Poleni zenu akina nguza,naona kama mmeingia choo cha kike.
   
 7. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #7
  Feb 24, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,378
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  badala ya kwenda kanisani kumshukuru Mungu kwa kuwatendea huo muujiza, nyie mnaenda kuyashukuru na kuongea na majini ya shekh yahya, utafuteni uso wa Mungu kwanza oooohooo!
   
 8. Noname

  Noname JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 1,269
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  huyu Shekhe Yahya ana abudu majini sio?
   
 9. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  yap!
   
 10. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  vijana mtafuteni mungu acheneni na huyo kizeee atawachanganya na maneno mengi ata hizo hela alizo wapa kueni makini kwani akikupa na mkono wa kulia anachukua na mkono wa kushoto usanii mtupu
   
 11. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Aaah wacheni wamuaminio huyu babu wazifuate njia zake!!
   
 12. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,037
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  sheikh yahya hawezi kuonyesha njia kwa mtu yeyote.................sote tunajua kuwa YESU ndio njia ya kweli na uzima na mtu hawezi kumwona mungu bila kupitia kwa yesu....................bora hao watoto waokoke wamjue yesu watafanikiwa
   
 13. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 12,037
  Likes Received: 3,872
  Trophy Points: 280
  nasikitika kwamba mpaka sasa bado kuna watu wanaomwamini huyu sheikh feki ambaye waislamu wamempinga vikali
   
 14. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Jile79 nakubaliana na wewe,but suluhisho si kuokoka tuu,hawa watoto nawashauri wasitetereshwe kiimani,wasimame kwenye imani yao kwani Mungu anasikiliza maombi ya kila amwaminie sio tuu walokole,kuhusu huyu babu nahisi yuko mbioni kufungua dhehebu lake,sababu kila kukicha atataka kuwalisha imani wale wenye imani haba!!
   
 15. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Wamepewa laki watatoa milioni. Subiri uone.
   
 16. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2010
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,512
  Likes Received: 3,032
  Trophy Points: 280
  huyu mzee kashajifanya mungu mtu
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  na atawachanganya si kidogo ...maji na mafuta havitangamani hata kidogo
   
 18. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2010
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,708
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ujumbe mzuri sana kaka!! ila avator inakulet down m2 wangu. Yule jamaa noma
   
 19. SHUPAZA

  SHUPAZA JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2010
  Joined: Aug 4, 2009
  Messages: 548
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yote ni yote chamsingi wametoka kama ni nani au nani poa ilimradi watoke wote kwa sasa nampa big -up aliweza kuwasaidia hawa madogo kutoka jela wakili nguli mzee marando na wengine wote walioonyesha way foward much respect buddy!
   
 20. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #20
  Feb 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  mhhhhhhhhh kweli kuacha asili ngumu sana, wasipoangalia watarudi kulekule, masharti ya hawa sangoma ndio yaleyale..............
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...