TANZIA Sheikh Suleiman Kilemile afariki dunia

Innalillahi wainna ilayhi rajiun

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Asalaam Alaykum wana Jf.
Miezi mitatu hii imekuwa ya misiba mikuu nchini Tanzania ,ikiwemo bara na visiwani.

Leo tena tarehe 6/5/2020 , Shekh wetu muadham Shk. Suleiman Amrani Kilemile katutoka.Shk. ni imamu wa msikiti wa Tandika ,mkaazi wa Kimara Baruti na Mwalimu wa madaris mabali mbali mjini Dar es Salaam ,Jana usiku alifariki duni Kinondoni katika Hospitali ya Dr, Mvungi baada ya kuzidiwa na Sukari akiwa Nyumbani kwake.

Shk. amehudumu katika Daawa ya kiislamu kwa miaka mingi tokea miaka ya 80 ,akisomesha na kutowa mihahara ya kiislamu katika miskiti mbali mbali.

Skh. Ni imamu wa Msikiti uliopo Tandika Maghorofani uliopakana na shule ya Maarifa Tandika Secondari .
Marehemu amezikwa leo Saa saba Mchana katika eneo la shule hiyo ya Maarifa Secondari School.
kwa vile Shk. ni Muasisi wa Shule hiyo na ni mjenzi wa Msikiti uliopo karibu na shule hiyo ya Maarifa, ambao tangia uanzishewe mwishoni mwa miaka ya 90 uko chini ya uongozi waki .

Tunamuombea Allah amuweke mahali pema peponi -Amin na amuepushe na adhabu ya Moto wa Jahannam. Amsamehe makosa yake na amkubalie mema yake yote na kuyaongeza daraja Amin.

Aidha wiki iliyopita Nchini Zanzibar
Sheikh Habib Allly Kombo alifariki dunia akiwa Nyumbani kwake kwa uzee.
SHK. Aliwahi kuwa Chif Kadhi wa Zaniziba na alisomesha wanafunzi wengi elimu ya Kiislamu.
Shk. habib alikuwa na fani zisizopungua 16 za kislamu na kwa kuwa alikuwa mwalimu mzuri sana , wengi walijifunza kwake ,
Shk Alikuwa Mfasiri mzuri wa Qur-an tukufu na alikuwa mweledi wa Lugjha ya kiswahili katika kutafsiri Qur-an , Alikuwa bobezi katika fani ya Mirath na kuandika baadhi ya vitabu katika fani hiyo.
Pengo lake kwa sasa si rahisi kupata mbadala wake Allah amweke mahala pema peponi -Amin.

Aidha
Miezi miwili iliopita Shk Nyundo naye alitutoka Ghafla.
Kifo chake kilileta mshituko mkubwa kwa Vijana na Kina mama ,ambao wengi wao waliguswa sana namawaidha yake yenye miguni ya kibabe na ukali wa kiaina yake.
Tukikumbuka Shk. Nyundo staili yake ya kutoa mawaidha na kugogoteza kwa mbwembwe ziliwavuta sana vijana,na kina mama
na kwa upande wa kina mama ,alikuwa akiwaasa sana kuachana na mambo machafu na watulie kwenye ndoa zao ,na kuwataka kukubali kuwa na uke wenza ,kwani si kasoro kuwa na mwenzio kwenye ndoa,
SKH. Nyundo alizikwa kwao Kizimkazi huku mazishi yake yakihudhuriwa na Maelfu ya waumini wa Rika zote.

TUNAMUOMBA ALLAH AWASAMEHE MAKOSA YAO NA AWAKUBALIE MEMA YAO NA AWAINGIZE PEPONI
AMIN.
Amin amin thumma amin

Al marhum Habib Ally Kombo.

اللهم اغفر له وارحمه، وعافه ،واعف عنه ،وأكرم نُزُله ، ووسع مُدخلهُ ، واغسله بالماء والثلج والبرد ، ونقه من الخطايا كما ينقى الثوب الأبيض من الدنس ، وأبدله داراً خيراً من داره ، وأهلاً خيراً من أهله وزوجاً خيراً من زوجه، وأدخله الجنة ،وأعذه من عذاب القبر ومن عذاب النار.
امين امين ثم امين

"رمضان كريم وصوم مقبول"
 
Back
Top Bottom