Sheikh Ponda na uchaguzi wa Rais 2010

Sheikh Ponda na uchaguzi wa Rais 2010

Hoja yangu pamoja na historia hiyo jee kwa muktadha wa leo yaani hatupo tena kwenye kudai uhuru je ni sahihi kwa wao kuendelea kujiingiza kwenye siasa tena kwa kushawishi waumini kuchukua mirengo ya kisiasa?
Masheikh wapo kwaajili ya watu na siasa ni kwaajili ya watu hauwezi penye hofu na mtafaruku lazima viongozi wa dini wasimame maana wapo kwaajili ya watu na watu wana dini.
 
Nchi yetu ukiwa na vyeo viwili halafu ukawa unaongea "UKWELI (HAUPIGI MAPAMBIO), basi huwezi na usitegemee kuthaminika hata kidogo, ukiwa "SHEIKH au ASKOFU".

Mfano, Askofu Bagonza na Sheikh Ponda, ila ukiwa kama Sheikh Wa Dar (Mzee Wa Kula Bata Dubai) basi kiti chako ni uhakika mpaka 2020.
Ukweli
 
Rais wa muhula mmoja ni JK? Maana useme wazi. Sababu hata risasi alipigwa kipindi cha awamu ya nne. Tuwe wakweli, nani anayewaonea waislamu? Mbona ni kama kila siku anatafutwa mchawi?
Kinachoendelea hakileti uhai wa kitaifa kinaleta mgawanyiko mimi ni mkiristo ila siku zote napenda haki isimame.

Ponda kama ana makosa apelekwe mahakamani sheria ichukue mkondo wake
 
Ndugu yetu wanataka kumuangusha (. )? Nimeongea na ndugu zetu (. ) Ndugu zetu Ni Nani?
 
Kinachoendelea hakileti uhai wa kitaifa kinaleta mgawanyiko mimi ni mkiristo ila siku zote napenda haki isimame.
Ponda kama ana makosa apelekwe mahakamani sheria ichukue mkondo wake
Wewe ni mkiristo sio mkristu. Acha kutuzuga Ila hili la kubebana sababu ya dini halikubaliki. Tujaziwe vilaza kisa dini zi balance? Hakunaga hiyo kitu popote duniani!
 
Kumbe 2010 alimpigania rais muislamu mwenzake ila waislamu hawakupata faida yeyote,sasa kaona bora kumpigania rais asiye muislamu.
 
SHEIKH PONDA ISSA PONDA NA UCHAGUZI WA RAIS 2010

Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nilikuwa naishi Tanga na ikawa nimekuja Dar es Salaam.

Nimekutana na Sheikh Ponda Msikiti wa Manyema baada ya Sala ya Alasiri.

Muda mrefu tulikuwa hatujaonana tukawa tumesimama pembeni tunazungumza.

Namwangalia Sheikh Ponda namuona kadhoofu na mikono yake imejaa alama ndogo ndogo za upele.

Nikamuuliza kulikoni hali ile.

Sheikh Ponda akaniambia kuwa yeye haumwi lakini amekuwa akizunguka nchi nzima kumfanyia kampeni mgombea mmoja wa urais.

Aliponitajia jina la mgombea na chama anachotoka hakika nilipatwa na mshtuko nikataka kujua habari zile zaidi.

"Kuna njama zimesukwa dhidi ya ndugu yetu kumwangusha ili awe rais wa kipindi kimoja na mpinzani wake anaungwa mkono na watu wenye nguvu sana wengine ndani ya chama chake."

Taratibu Sheikh Ponda akanieleza hali inayomkabili huyu ndugu yetu.

"Natembea kijiji kwa kijiji nazungumza na ndugu zetu nawaeleza uamuzi tuliofikia na kuwaomba wabadilishe upigaji kura wao tumsaidie huyu ndugu yetu asifedheheshwe kwani kuanguka kwake ndiyo kuanguka kwetu."

Sheikh Ponda akaniambia alikuwa huko vijijini kwa muda mrefu anazunguka nchi nzima akibebwa kwenye baiskeli kutoka kijiji kimoja kwenda kingine na akilala misikitini.

Huku kulala kwenye hii misikiti ya vijijini ndiyo sababu ya kuumwa sana na mbu.

Nimeinamisha kichwa changu chini sina la kusema.
Wapi mtu utapata la kusema unapopambana hila kama hizi?

Nimeingiwa na simanzi kwani naujua umasikini wa watu hawa wanaompokea Sheikh Ponda lakini najua pia ari zao ndani ya dhiki zao.

Niliponyanyua kichwa changu nikamuuliza kama hao anaowafanyia kampeni wanafahamu hizi juhudi zake.

Sheikh Ponda akatingisha kichwa huku anatabasamu akaniambia kuwa hawakuwa wanajua chochote.

"Sheikh Ponda unawafanyia hisani kubwa sana hawa jamaa na In Shaa Allah ndugu yetu atapita lakini sisi hali yetu itabakia vilevile," nilimweleza Ponda.

"Hilo si kama silijui lakini kesho nitakuwa na majibu ya kumjibu Allah kuwa nilisimama na ndugu yangu pale alipokabiliwa na maadui zake kumdhuru"

Baada ya uchaguzi Sheikh Ponda alipambana na masahibu mengi na mwisho akapigwa risasi ya bega Morogoro.

Huwezi kummaliza Sheikh Ponda kwani ana mengi.View attachment 1504843

😀😂😂😂😂. Alama gani ya uadilifu? Hapo pana namna..anapambana wale wenzake waachiwe. Kwani shida hasa ni nini? Amepewa ahadi ambayo sidhani kama itatekelezeka
 
Mzee wangu usisubiri kilakitu kuwe historian ndio utujuze, ingawa najua wewe ni habari la historia,
Ingependeza uandike ya sheikh Ponda na siasa za 2020. Ili tuelewe vizuri msimamo wako juu ya sheikh Ponda nasi tufanye maamuzi sahihi kabla Jua halijachwa.
 
Kumbe 2010 alimpigania rais muislamu mwenzake ila waislamu hawakupata faida yeyote,sasa kaona bora kumpigania rais asiye muislamu.

Na hata sasa amejiunga kambi ambayo imeahidi kuwaachia huru wale walioko ndani, ambao ni rafiki zake kweli kweli. Najiuliza ni kwanini wako ndani?
 
Back
Top Bottom