Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,282
- 33,880
SHEIKH PONDA ISSA PONDA NA UCHAGUZI WA RAIS 2010
Wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 nilikuwa naishi Tanga na ikawa nimekuja Dar es Salaam.
Nimekutana na Sheikh Ponda Msikiti wa Manyema baada ya Sala ya Alasiri.
Muda mrefu tulikuwa hatujaonana tukawa tumesimama pembeni tunazungumza.
Namwangalia Sheikh Ponda namuona kadhoofu na mikono yake imejaa alama ndogo ndogo za upele.
Nikamuuliza kulikoni hali ile.
Sheikh Ponda akaniambia kuwa yeye haumwi lakini amekuwa akizunguka nchi nzima kumfanyia kampeni mgombea mmoja wa urais.
Aliponitajia jina la mgombea na chama anachotoka hakika nilipatwa na mshtuko nikataka kujua habari zile zaidi.
"Kuna njama zimesukwa dhidi ya ndugu yetu kumwangusha ili awe rais wa kipindi kimoja na mpinzani wake anaungwa mkono na watu wenye nguvu sana wengine ndani ya chama chake."
Taratibu Sheikh Ponda akanieleza hali inayomkabili huyu ndugu yetu.
"Natembea kijiji kwa kijiji nazungumza na ndugu zetu nawaeleza uamuzi tuliofikia na kuwaomba wabadilishe upigaji kura wao tumsaidie huyu ndugu yetu asifedheheshwe kwani kuanguka kwake ndiyo kuanguka kwetu."
Sheikh Ponda akaniambia alikuwa huko vijijini kwa muda mrefu anazunguka nchi nzima akibebwa kwenye baiskeli kutoka kijiji kimoja kwenda kingine na akilala misikitini.
Huku kulala kwenye hii misikiti ya vijijini ndiyo sababu ya kuumwa sana na mbu.
Nimeinamisha kichwa changu chini sina la kusema.
Wapi mtu utapata la kusema unapopambana hila kama hizi?
Nimeingiwa na simanzi kwani naujua umasikini wa watu hawa wanaompokea Sheikh Ponda lakini najua pia ari zao ndani ya dhiki zao.
Niliponyanyua kichwa changu nikamuuliza kama hao anaowafanyia kampeni wanafahamu hizi juhudi zake.
Sheikh Ponda akatingisha kichwa huku anatabasamu akaniambia kuwa hawakuwa wanajua chochote.
"Sheikh Ponda unawafanyia hisani kubwa sana hawa jamaa na In Shaa Allah ndugu yetu atapita lakini sisi hali yetu itabakia vilevile," nilimweleza Ponda.
"Hilo si kama silijui lakini kesho nitakuwa na majibu ya kumjibu Allah kuwa nilisimama na ndugu yangu pale alipokabiliwa na maadui zake kumdhuru"
Baada ya uchaguzi Sheikh Ponda alipambana na masahibu mengi na mwisho akapigwa risasi ya bega Morogoro.
Huwezi kummaliza Sheikh Ponda kwani ana mengi.