Sheikh Ponda Issa Ponda kashinda rufaa ya Serikali

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,903
30,243
SHEIKH PONDA ISSA KASHINDA RUFAA
Mohamed Said December 18, 2017 0

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.
Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake.

Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu.
Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi.


Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.
Hakika wewe ni kiongozi.

Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.
Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.
Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda.
Allah akuhifadhi kiongozi wetu.
Amin.''

Wakili Juma Nassoro


Sheikh Ponda na Wakili Juma Nassoro wakiwa Mahakamani


Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika pingu Mahakamani

Ilikuwa katika semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania mwaka wa 1988 ndipo kwa mara ya kwanza nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam kutokea nchini. Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe.

Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na wengine wakapata ulemavu wa maisha. Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. Kosa lao likiwa ni kuihami Qur'an ya Allah isichezewe. Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi ya Kurwa Shauri aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine.

Katika hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu. Kulikuwa na pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika vyombo hivyo.

Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968. Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho. Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali.

Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa. Nini kilisababisha nakma hii? Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi.

Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979. Huu uwanja wa Waislam ndiyo Sheikh Ponda alipouchukua kuurudisha mikononi kwa Waislam ndipo alipokusudia kujenga msikiti na kuupa jina la Sheikh Hassan bin Amir na ni katika uwanja huu ndipo alipokamatwa na kushitakiwa.
 
SHEIKH PONDA ISSA KASHINDA RUFAA
Mohamed Said December 18, 2017 0

''Allah ni Mjuzi Allah na ni Mbora wa kulipa.
Sheikh Ponda utayakuta malipo yako kwa Allah yakiwa makubwa kwa subra na ustahamilivu kwa ajili ya dini yake.
Hukuwa tayari kuuza uhuru wako kwa matakwa ya wenye kudhulumu.
Muda wote ulitutia moyo mawakili wako kila tulipokutana na vitimbi.


Mara nyingi sisi mawakili tulikuwa kama wateja na wewe ndiye wakili.
Hakika wewe ni kiongozi.
Umma huu wa Waislam wa Tanzania utaishi kwa mfano wako.
Alhamdulilah leo uko huru baada ya miaka miwili na miezi mitatu jela ukiwa na jeraha kubwa la risasi.
Allah anayo siri kubwa katika maisha yako Sheikh Ponda.
Allah akuhifadhi kiongozi wetu.
Amin.''

Wakili Juma Nassoro


Sheikh Ponda na Wakili Juma Nassoro wakiwa Mahakamani


Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa katika pingu Mahakamani

Ilikuwa katika semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania mwaka wa 1988 ndipo kwa mara ya kwanza nilipofahamiana na Sheikh Issa Ponda. Ninachokumbuka kwa Sheikh Ponda ni kuwa alitusalisha sala moja na niliusikia usomaji wake mzuri wa Qur'an. Nilimpenda kutoka siku hiyo. Semina hii ilikuja baada ya mambo mengi dhidi ya Uislam kutokea nchini. Kulikuwa na sakata la Sophia Kawawa kutaka Qur'an ibadilishwe. Hii ilitokea mwezi Mei 1988. Baada ya kauli hiyo palifanyika maandamano makubwa Zanzibar kumpinga Sophia Kawawa na Waislam walishambuliwa, baadhi wakauliwa na wengine wakapata ulemavu wa maisha. Sheikh Said Gwiji mshtakiwa namba moja na wenzake walishitakiwa na wakafungwa jela miezi 18. Kosa lao likiwa ni kuihami Qur'an ya Allah isichezewe. Kulikuwa na vita vikipigwa dhidi ya vazi la hijab na kesi maarufu ilikuwa ya Fikira Omari mfanyakazi wa Kiltex. Kulikuwa na kesi ya Kurwa Shauri aliyeshitakiwa kwa ''uchochezi'' na mambo mengine. Katika hayo kulikuwa na tatizo la Mchungaji Christopher Mtikila aliyekuwa akimbughudhi Rais Mwinyi na kuwashambulia Waislam hasa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu. Kulikuwa na pia na ''Christian Lobby,'' mtandao wa siri katika vyombo vya habari vilivyokuwa vikiwapiga vita Waislam waliokuwa katika serikali ya Rais Mwinyi achilia mbali kuupiga vita Uislam wenyewe wakitumia nafasi zao katika vyombo hivyo.

Historia ya Waislam wa Tanzania itakapokuja kuandikwa jina la Sheikh Ponda Issa Ponda litaunganishwa na jina la Mufti Sheikh Hassan bin Amir kwa kitu kimoja nacho ni ardhi ya Chang'ombe Dar es Salaam ambako Waislam chini ya uongozi wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) walikusudia kujenga Chuo Kikuu mwaka wa 1968. Katika uwanja huu ndipo Rais wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere akishuhudiwa na Tewa Said Tewa na Mufti Sheikh Hassan bin Amir aliweka jiwe la msingi la chuo hicho. Chuo hakikujengwa na EAMWS ikapigwa marufuku na serikali. Mambo hayakuishia hapo. Sheikh Hassan bin Amir akakamatwa na kufukuzwa nchini akarudishwa ''kwao'' Zanzibar. Serikali ikaunda BAKWATA na Chuo Kikuu cha Waislam hakikujengwa. Nini kilisababisha nakma hii? Waliokuwa karibu na Sheikh Hassan bin Amir wanasema katika siku zake za mwisho kila alipotajiwa ule mradi wa chuo kikuu alikuwa akilia na kusema ilikuwa hamu yake kujenga chuo Kikuu kama Azhar ya Misri na akifika hapo alikuwa akibubujikwa na machozi. Wakati ule Sheikh Hassan bin alikuwa na miaka zaidi ya 90 na aliishi na simanzi hizi hadi alipokufa mwaka 1979. Huu uwanja wa Waislam ndiyo Sheikh Ponda alipouchukua kuurudisha mikononi kwa Waislam ndipo alipokusudia kujenga msikiti na kuupa jina la Sheikh Hassan bin Amir na ni katika uwanja huu ndipo alipokamatwa na kushitakiwa.
Allah atamlipa ujira wake In Shaa Allah
 
Hakika Mungu yupo juu yupo juu ya kila kitu na Muweza wa yote. Khila na ghilba za mabazazi zina mwisho. Ipo siku mwanga utaangaza kwa kila kiumbe na kuughafirisha ubaya.
 
Back
Top Bottom