Sheikh Ponda anaendelea kushikiliwa Polisi. Inasemekana yupo Kituo cha Magomeni

Mkuu unazungumzia Waislamu WA Nchi gani?.. Tanzania hii ? Ni waoga KULIKO wanafanyiwa mangapi wameufyata?.. Wazee WA uamsho walipigwa kimya wafuasi wapo kimya hawajali wala nn!.. na How viongozi wao Hawaishi kugonha chears na vigogo.. zungumza Waislamu wa Palestina huko na Somalia Hao ndo Vidume,,Takbiriiiiii

Tofautisha kuwa "Reactionary" na kuwa "Cool headed"

Ukimya wa Waislamu na subira ni kwa ajili ya Amani ya nchi hii, na kutumia njia zote za amani kudai haki zao nchini, Ikishindikana hiyo utaona pressure yao ikiongezeka kidogokidogo mpaka mifumo kandamizi dhidi yao itakapobomolewa.

Hakuna kundi la kijamii nchini linaloweza kusimama barabarani mbele ya askari wenye mabomu na mabunduki na kusema "Hapana " bila woga, ni kundi la Waislamu.

By nature uislam na Dhulma ni incompatible (havichangamani), ndiyo maana wazee wa Kiislamu akina Abushiri bin Sultan, Mwinyikheri, Mkwawa, Kinjekitile, Wazee wa TANU walisimama kutaka dhulma Tanganyika iondoke!.
Sasa moyo na spirit kama hiyo vimo ndani ya waislamu, Hawa siyo watu waoga, kwanza kwenye Uislamu kuwa muoga ni upungufu wa Imani!

Subira yao isihesabike ni udhaifu!

Amani siyo udhaifu bali ni faida ya wote!
 
Kuliko kuwa na mwembechai nyingine ni bora huyo Ponda arudishwe kwao unajua hawa majirani zetu watu wao wanatuletea matatizo sana angalia huyu ndugu yake wa ACT wazalendo matusi kejeli na kutishia watu kuwaroga
Kwao ni wapi?
 
‘Siasa bila dini ni uendawazimu’

Na Lilian Nyenza

Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.

Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.

Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Source ya chapisho?
 
hili jambo lichukuliwe kwa tahadhari lisije kuleta mpasuko ktk nchi yetu, maana Tanzania ni nchi yetu sote hatuna nchi nyigine hivyo nawaomba watwnzania tuishi kwa kuvumiliana kama tulivyo zoea,
tusiingize ushabiki....haitotusaidia,
 
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa na Jeshi la Polisi siku nane zilizopita (Julai 9, 2020) yuko Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa amekuwa akihamishwa kituo kimoja hadi kingine lakini akipelekwa Kituo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa kila alfajiri.

Soma hapa Sheikh Ponda anaendelea kushikiliwa na Polisi – Siku ya 8
Magomeni ipi ?acha kuleta habari za uongo .
 
Huyu alimsumbua sana kikwete huyu jamaa akome au aisomee abladili serikali basi
 
Mkuu, ukitetea mtu mtetee kwa kuwa ana haki Kama mtanzania mwenzetu na wapenda haki wengi wataungana nawe. Usifanye hivyo kwa kushambulia dini zingine.

"Umoja Ni nguvu, utengano Ni udhaifu". Ukidai haki huku unagawa watu kwa misingi ya dini hufiki kokote.. hapo unasaidia watawala waovu na doctrine yao ya "divide and rule".

Huyo askofu Niwemugizi unayemsema, alipoombwa vyeti vya kuzaliwa vya babu, bibi, baba, mamaake, nk wakati hata jiwe hana hivo vyeti, hukusikia?

Na huyo Gwajima alipowekwa korokoroni na kupimwa mkojo hukusikia? Na mifano ya hivyo ni mingi tuu..

Au nikuulize, uchomaji moto wa makanisa awamu ya Mwinyi na awamu ya Kikwete unazungumzia vipi? Mbona wachomaji hawakukamatwa??
Mkuu, Usihangaike kujibishana na hawa watu wanaokuwa miili tu huku akili zikidumaa kila uchao. Huyu kijana anachofanya hapa ni kuongea hisia zake na si uhalisia.

Anachokiamini yeye ni kuwa waumini wa imani ya kiislam wananyanyaswa wazi wazi kimfumo na waumini wa dini ya kikristo wanapendelewa kimfumo..... So haina haja kumuelekeza. Achana naye
 
Jamani hizi chokochoko za nini?!! Tena kipindi hiki tunaelekea kwenye uchaguzi?!
Malumbano haya hayana mshindi yoyote.
Vyombo vyetu vya ulinzi vishughulikie Kwa umakini mambo haya
 
Waislamu siyo waoga hata kidogo

Ni Waislamu waliomface Mkoloni kuanzia vita vya majimaji na hata kwenye harakati za kudai uhuru wao walikuwa msitari wa mbele.

Waislamu ni majasiri wa kumueleza mtawala ukweli, isipokuwa wana uungwana sana na subira sana.

Nakuhakikishia kundi pekee nchini ambalo likisema kuwa linaingia barabarani kudai haki yao katika nchi hii ni waislamu ndo wenye ujasiri huo. Na serikali inalijua hilo ndiyo maana siku zote imejitahidi kuwaweka masheikh wenye ushawishi kwenye "payroll" yake. Na BAKWATA ilianzishwa specifically ili kuwa "watchdog" wa waislamu, kwa sababu inawajua kuwa waislamu wakiamua lao huwezi kuwazuia.

Isipokuwa sasa serikali lazima iwatendee haki, isiabuse ukimya wao, hawa wana subira sana, lakini ikivuka mipaka, inakuwa inatengeneza bomu linalosubiri kupasuka!

Tusitengeneze Mwembechai nyingine!
Acha mikwara wewe. Hao unaowaita waislam ni taifa, jamii, jinsia, kundi maalumu au ni kitu gani?!

Ungekuwa mzungu nina uhakika ungekuwa supremacist na bigot wa damu.

Unaonekana umebebelea kwenye kichwa chako fikra za ubaguzi na kutambua sera na maoni ya kidini kwanza kabla ya Uraia, uzalendo na taifa lako.

Elimu ya uraia ni muhimu sana...... Naona vijana siku hizi mnajifunza vitu potofu sana juu ya taifa lenu.

Wewe aliekuambia waislam ndio walipigania uhuru ni nani?! Ukipreach uongo ukweli utabatilisha hiyo nadharia yako. Waliotafuta uhuru kipindi hicho walikuwa ni watu weusi wanapigana na watu weupe period. Haikuwa vita ya kupigania dini bali vita ya kupigania uhuru wa mtu mweusi.

Sasa wewe unataka kutuambia habari mnazopeana huko masjid baada ya kupiga dufu na kushiba pilau la maulid hebu acha utoto na ujuha muda mwingine.
 
Tofautisha kuwa "Reactionary" na kuwa "Cool headed"

Ukimya wa Waislamu na subira ni kwa ajili ya Amani ya nchi hii, na kutumia njia zote za amani kudai haki zao nchini, Ikishindikana hiyo utaona pressure yao ikiongezeka kidogokidogo mpaka mifumo kandamizi dhidi yao itakapobomolewa.

Hakuna kundi la kijamii nchini linaloweza kusimama barabarani mbele ya askari wenye mabomu na mabunduki na kusema "Hapana " bila woga, ni kundi la Waislamu.

By nature uislam na Dhulma ni incompatible (havichangamani), ndiyo maana wazee wa Kiislamu akina Abushiri bin Sultan, Mwinyikheri, Mkwawa, Kinjekitile, Wazee wa TANU walisimama kutaka dhulma Tanganyika iondoke!.
Sasa moyo na spirit kama hiyo vimo ndani ya waislamu, Hawa siyo watu waoga, kwanza kwenye Uislamu kuwa muoga ni upungufu wa Imani!

Subira yao isihesabike ni udhaifu!

Amani siyo udhaifu bali ni faida ya wote!
Hizi itikadi za mapambano ndizo hasa zinagonga alarm kwa wenye mamlaka kuwashughulikia.

Hata mimi ningekuwa serikali nisingewabakiza.

Hapana. Matokeo ya hizi itikadi kali ni ugaidi na instability.
 
Fair treatment kwa makundi yote ya jamii lazima iwepo.

Askofu wa Rulenge, Niwemugizi alitoa kauli ya kupinga kuwaachia watu kwenda kusali kwenye mijumuiko ya wengi kipindi cha korona alikamatwa?

TEC wametoa nyaraka za kutaka haki za watu na demokrasia viwepo nchini, umewahi kusikia wanawekwa ndani?

Walutheri nao walitoa waraka wao, kuna askofu alikamatwa?

Askofu Bagonza naye huwa anatoa misimamo kuhusu haki za raia umewahi kusikia anaitwa hata Central?

Gwajima anatoa kauli kuwa Wasukuma waungane wamsaidie msukuma mwenzao, umewahi kusikia akiwekwa ndani hata siku moja kwa uchochezi?

Waislamu siku zote hizo wako kimya, hawajatoa waraka hata mmoja

Leo nao wanatoa wa kwao, unaohusu mustakbali wa nchi na maslahi yao then serikali inamtia ndani msomaji tu wa Taarifa ya maimamu, kama hii siyo double standard ni kitu gani?

Serikali lazima iheshimu makundi yote ya kijamii siyo kundi moja inaheshimu viongozi wake na kundi jingine inakamata na kuweka ndani viongozi wake!

Leo hii kuna Masheikh kibao wako jela, hawajatibitika kuwa na kosa lolote mbele ya sheria lakini wako wanaozea jela!

Serikali hii imesamehe hadi wabakaji waliofungwa kifungo cha maisha lakini haiachii huru masheikh ambao imeshindwa kuthibitisha makosa yao mbele ya mkono wa sheria.

Acha maneno yako wewe, fikiria sana ksbla ya kucomment mitandaoni.

Waislamu hawapendi treatments za nsmna hii!
Tofautisha mambo na utawala wa Kanisa na imani yako Sir
 
Back
Top Bottom