Sheikh Ponda anaendelea kushikiliwa Polisi. Inasemekana yupo Kituo cha Magomeni

Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa na Jeshi la Polisi siku nane zilizopita (Julai 9, 2020) yuko Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa amekuwa akihamishwa kituo kimoja hadi kingine lakini akipelekwa Kituo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa kila alfajiri.

Soma hapa Sheikh Ponda anaendelea kushikiliwa na Polisi – Siku ya 8
Wacha amalize mwaka akitoka atakuwa amejifunza shughuli za kueneza dini na sio siasa.
 
Haya umewahi kuwaambia maaskofu wa TEC na nyaraka zao?

Ponda ni mjumbe tu, Waraka ni wa shura ya maimamu.

Serikali imuachie huru sheikh Ponda, hana kosa
Wewe na jina lako mbandia ndio unataka kutwambia alichosema Ponda? Serikali hii haiongozwi na wajinga kama walioiweka nchi yetu kwenye uchumu mbovu tangu tujitawale. Jaribu kupata ukweli kabla ya kubwatuka.
 
Sheikh Ponda ameshafikishwa Tabora...hali yake sio nzuri sana kiafya...amekataa kula toka juzi...lolote tunaweza sikia juu yake ..huenda wala mu-masoud
 
Wewe na jina lako mbandia ndio unataka kutwambia alichosema Ponda? Serikali hii haiongozwi na wajinga kama walioiweka nchi yetu kwenye uchumu mbovu tangu tujitawale. Jaribu kupata ukweli kabla ya kubwatuka.

punguza chuki mkuu, hazikusaidii

Mbona maaskofu walipotoa waraka wa kutaka demokrasia iwepo nchini hakuna askofu hata mmoja aliyekamatwa na polisi na wewe hujawahi kuishauri serikali iwaweke ndani?

Acha udini!
 
Wewe ndio upunguze chuki na jibu hoja bila kutafuta sympathy. Maaskofu wanaingiaje hapo? Unataka kubadili issue? Aliyeshikwa ni Ponda. Wacha wivu!

khe khe khe Kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee mimi niwe na chuki kwa Ponda kwa lipi hasa? Udini ni wewe ambaye unawaingiza Maaskofu haya twambie makosa yao chacha?
 
Wewe ndio upunguze chuki na jibu hoja bila kutafuta sympathy. Maaskofu wanaingiaje hapo? Unataka kubadili issue? Aliyeshikwa ni Ponda. Wacha wivu!

Fair treatment kwa makundi yote ya jamii lazima iwepo.

Askofu wa Rulenge, Niwemugizi alitoa kauli ya kupinga kuwaachia watu kwenda kusali kwenye mijumuiko ya wengi kipindi cha korona alikamatwa?

TEC wametoa nyaraka za kutaka haki za watu na demokrasia viwepo nchini, umewahi kusikia wanawekwa ndani?

Walutheri nao walitoa waraka wao, kuna askofu alikamatwa?

Askofu Bagonza naye huwa anatoa misimamo kuhusu haki za raia umewahi kusikia anaitwa hata Central?

Gwajima anatoa kauli kuwa Wasukuma waungane wamsaidie msukuma mwenzao, umewahi kusikia akiwekwa ndani hata siku moja kwa uchochezi?

Waislamu siku zote hizo wako kimya, hawajatoa waraka hata mmoja

Leo nao wanatoa wa kwao, unaohusu mustakbali wa nchi na maslahi yao then serikali inamtia ndani msomaji tu wa Taarifa ya maimamu, kama hii siyo double standard ni kitu gani?

Serikali lazima iheshimu makundi yote ya kijamii siyo kundi moja inaheshimu viongozi wake na kundi jingine inakamata na kuweka ndani viongozi wake!

Leo hii kuna Masheikh kibao wako jela, hawajatibitika kuwa na kosa lolote mbele ya sheria lakini wako wanaozea jela!

Serikali hii imesamehe hadi wabakaji waliofungwa kifungo cha maisha lakini haiachii huru masheikh ambao imeshindwa kuthibitisha makosa yao mbele ya mkono wa sheria.

Acha maneno yako wewe, fikiria sana ksbla ya kucomment mitandaoni.

Waislamu hawapendi treatments za nsmna hii!
 
Fair treatment kwa makundi yote ya jamii lazima iwepo.

Askofu wa Rulenge, Niwemugizi alitoa kauli ya kupinga kuwaachia watu kwenda kusali kwenye mijumuiko ya wengi kipindi cha korona

TEC wametoa nyaraka za kutaka haki za watu na demokrasia nchini ziwepo

Walutheri nao walitoa waraka wao

Askofu Bagonza naye huwa anatoa misimamo kuhusu haki za raia.

Gwajima anatoa kauli kuwa Wasukuma waungane wamsaidie msukuma mwenzao, umewahi kusikia akiwekwa ndani hata siku moha kwa uchochezi?

Waislamu siku zote hizo wako kimya, hawajatoa waraka hata mmoja

Leo nao wanatoa wa kwao, unaohusu mustakbali wa nchi na maslahi yao then serikali inamtia ndani msomaji tu wa Taarifa ya maimamu, kama hii siyo double standard ni kitu gani?

Serikali lazima iheshimu makundi yote ya kijamii siyo kundi moja inaheshimu viongozi wake na kundi jingine inakamata na kuweka ndani viongozi wake!

Leo hii kuna Masheikh kibao wako jela, hawajatibitika kuwa na kosa lolote mbele ya sheria lakini wako wanaozea jela!

Serikali hii imesamehe hadi wabakaji waliofungwa kifungo cha maisha lakini haiachii huru masheikh ambao imrshindwa kuthibitisha makosa yao mbele ya mkono wa sheria. Kama huu siyo udini uliokubuhu ni nini?

Acha maneno yako wewe, fikiria sana ksbla ya kucomment mitandaoni.

Waislamu hawapendi treatments za nsmna hii!
Pumba tupu hapo juu. Mimi sifahamu kosa lake Je, wewe mwerevu unaweza kutuwekea hapa makosa yake na ushahidi? Au ndio majungu yenyewe? Serikali haiongozwi kwa majungu!
 
Wewe ndo ulisema awekwe ndani mwaka mmoja!, na mimi nakuuliza kwa kosa gani?
Kwa hiyo unakubali pumba ulizoandika hapo juu na sasa unabadili gia angani? Polisi ndio wenye dhamana ya kumuweka mtu ndani sasa wewe unalialia nini?

Mbona wengi tu wanawekwa ndani na baada ya siku tunaambiwa waliwekwa ndani kwa makosa gani nk? Wewe na jina lao la bandia ndio mwerevu kumbe hata makosa hufahamu, ndio upimbi wenyewe huo. Mwache asote huko jela.
 
Katibu Mkuu wa Shura ya Maimamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda aliyekamatwa na Jeshi la Polisi siku nane zilizopita (Julai 9, 2020) yuko Kituo cha Polisi Magomeni jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa amekuwa akihamishwa kituo kimoja hadi kingine lakini akipelekwa Kituo Kikuu kwa ajili ya kuhojiwa kila alfajiri.

Soma hapa Sheikh Ponda anaendelea kushikiliwa na Polisi – Siku ya 8
Je wakiendelea kumshikilia ule waraka utabadilika au kufutika?
 
Fair treatment kwa makundi yote ya jamii lazima iwepo.

Askofu wa Rulenge, Niwemugizi alitoa kauli ya kupinga kuwaachia watu kwenda kusali kwenye mijumuiko ya wengi kipindi cha korona alikamatwa?

TEC wametoa nyaraka za kutaka haki za watu na demokrasia viwepo nchini, umewahi kusikia wanawekea ndani?

Walutheri nao walitoa waraka wao, kuna askofu alikamatwa?

Askofu Bagonza naye huwa anatoa misimamo kuhusu haki za raia umewahi kusikia anaitwa hata Central?

Gwajima anatoa kauli kuwa Wasukuma waungane wamsaidie msukuma mwenzao, umewahi kusikia akiwekwa ndani hata siku moha kwa uchochezi?

Waislamu siku zote hizo wako kimya, hawajatoa waraka hata mmoja

Leo nao wanatoa wa kwao, unaohusu mustakbali wa nchi na maslahi yao then serikali inamtia ndani msomaji tu wa Taarifa ya maimamu, kama hii siyo double standard ni kitu gani?

Serikali lazima iheshimu makundi yote ya kijamii siyo kundi moja inaheshimu viongozi wake na kundi jingine inakamata na kuweka ndani viongozi wake!

Leo hii kuna Masheikh kibao wako jela, hawajatibitika kuwa na kosa lolote mbele ya sheria lakini wako wanaozea jela!

Serikali hii imesamehe hadi wabakaji waliofungwa kifungo cha maisha lakini haiachii huru masheikh ambao imeshindwa kuthibitisha makosa yao mbele ya mkono wa sheria.

Acha maneno yako wewe, fikiria sana ksbla ya kucomment mitandaoni.

Waislamu hawapendi treatments za nsmna hii!
Udhaifu na uoga wa waislamu ndio unawagharimu, na mtaendelea kunyayaswa mpaka mtakaporejea kwenye mafundisho ya mtume wenu
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom